“Nilikuamini, na kukutegemea, na kuwa na uhakika ndani Yako, Ee Bwana. Nilisema, Wewe ndiwe Mungu wangu. “Nyakati zangu zimo mikononi mwako; nikomboe kutoka kwa mikono ya adui zangu na wale wanaonifuatia na kuniletea dhiki.” Zaburi 31: 14,15 AMP Katika sura hii, mwandishi wa Zaburi ansema kwamba alimtumainia Mungu kumkomboa, na alimtegemea kufanya hivyo kwa wakati uliofaa. Kumtumainia Mungu kunahitaji tuseme, “Nyakati zangu zimo mikononi Mwako.”
Nimejifunza kwamba tegemeo linatuhitaji kukubali kwamba kuna maswali mengine ambayo yatabaki yakiwa hayana majibu na hivyo basi kuweka nyakati zetu mikononi mwake Mungu – tukiamini kwamba japo hatuyajui majibu yote, Yeye ayajua. Anao wakati unaofaa kikamilifu kwa kila jambo maishani mwetu.
Sote huwa tunatamani na kuamini kwamba mambo mazuri yatendeke maishani mwetu, SASA – si baadaye! Tunavyoendelea kukomaa katika maisha yetu ya Kikristo, tunajifunza kuaminia vitu sio SASA, lakini katika wakati mwafaka wa Mungu. Waiberania 11:1 inasema, “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Wakati wowote tunaweza kuwa na imani ‘sasa’, lakini sio kila wakati tutaweza kuona udhihirisho wa yale tunayoyaaminia sasa. Kumtumainia Mungu mara nyingi kunahitaji kutofahamu jinsi Mungu atakavyo timiza yale yanayohitaji kutimizwa na pia kutofahamu ni lini atakavyofanya hivyo.
Sisi husema, “Mungu hachelewi,” lakini mara nyingi yeye haji mapema pia. Kwa nini? Kwa maana Yeye hutumia nyakati hizo kuimudu imani yetu ndani yake, na kutufanya tukakua wakati wa kungoja. Mojawapo wa wale watumishi wa huduma ya kifedha kila mwezi hivi maajuzi alijipata na haja ya kifedha ili aweze kulipa kodi zilizotokea ghafla, hakuzitarajia. Kodi zenyewe ilipasa zilipwe kufikia taerehe 15 Aprili. Mume na mke huyo walitoa sadaka maalum kwa huduma ya Ujenzi kanisani kwetu wakiamini Mungu awape muujiza waliohitaji. Tarehe 14 Aprili walipata pesa za kulipa kodi ile. Mbona muujiza haukuwafikia tarehe 1 au 5 Aprili? Ni kwa nini mara nyingine Mungu hungoja mpaka siku au dakika ya mwisho kabisa? Sababu ni kwamba yeye anatufundisha masomo kuhusu kumtumainia na kumtegemea.
Kutumainia hakupokelewi kama urithi, huja kwa kujifunza. Tunajifunza kumtumainia Mungu kwa kupitia mabo yanayohitaji kumtegemea.Tunapouona uaminifu Wake mara moja hadi nyingine, tunawacha kujitegemea na taratibu tunaingia kwenye pumziko la Mungu na kuweka imani yetu ndani Yake.
Tukiitazama hivi, ni rahisi kuona ni vipi wakati mwafaka unavyotimiza jukumu muhimu katika kujifunza kumtumainia Mungu. Kama Mungu angefanya kila kitu tunachomuomba mara moja, hatungeweza kukua na kukomaa. Wakati unaofaa na kutumainia ni mapacha. Wanafanya kazi bega kwa bega.
GetYourHopesUp
No comments:
Post a Comment