Sunday, 3 June 2018

MSIMU MWAFAKA

Mambo  Ya  Walawi  26:4  inasema,  “Nitazinyezesha mvua  zenu kwa nyakati zake.” Wagalatia 6:9 kwa tafsiri ya  AMP  inasema ni lazima  “…tusife moyo  na kuwa wachovu  na kuzimia katika kutenda kiungwana  na kutenda yaliyo ya haki, maana kwa wakati wake na kwa msimu ulioteuliwa tutavuna,  kama tusipouachilia na kupunguza ujasiri wetu na hapo kuzimia.”

Na katika 1 Petro 5:6  tunatiwa moyo  “kujinyenyekeza chini  ya mkono  wa  Mungu wenye nguvu, ili wakati wake ufaao utakapotimia” atatuinua. Msimu  mwafaka  au wakati  ufaao  ni  lini?  Naamini  ni wakati Mungu anajua  kuwa tuko tayari, wakati ambapo  kila mtu  anayehusika ako tayari na wakati  jambo hilo linaingia vizuri katika  mpango mkuu wa Mungu unaojumlisha mabo yote.  Mungu anao mpango wa kipekee  kwa maisha yetu  binafsi, lakini  pia  anao mpango wa jumla kwa ajili ya ulimwengu wote.

1 comment:

  1. Waaaoh safi sana mtumishi wa bwana mungu akutie nguvu nyingi

    ReplyDelete