Monday, 4 June 2018

Kwanini Mwili ni Mlegevu...?


Mtume Paulo  anafundisha  wazi  kwamba  mwili ni mlegevu, wenye tamaa,  na  matamanio  mengi ya  dhambi (angalia  RUM 13:14). Namshukuru  Mungu  kwa vile  tuko zaidi ya mwili.  Pia tuko na roho na sehemu  ya roho ya Mkristo ni  pale ambapo  maumbile ya  Mungu hukaa.  Mungu ni mwema na kwa  kuwa  Anakaa ndani  yetu inamaanisha  tuna wema ndani  yetu.

Kwa  roho zetu twaweza  kuunidhamisha  na kuutawala  mwili, lakini haihitaji juhudi.  Inahitaji ushirikiano na Roho Mtakatifu  Anayetupa nguvu sisi na kutuwezesha  kufanya  mambo mazuri. Paulo anasema hatuhitaji  kuuwekea  mahitaji  mwili na  ninaamini njia  moja  ambayo tumeuwekea mwili mahitaji ni kukaa bila kufanya kitu! Kukaa  bila kufanya chochote  ni  mazoea  mabaya. 
Kadiri tunavyokaa  bila kufanya  lolote,  ndivyo  tunavyotaka  kutofanya lolote. Nina hakika umewahi kukaa nyumbani siku  nzima na kupata  kuwa  kadiri unavyolala  hapo  kitandanii, ndivyo unavyohisi ugumu  kuinuka.  Unapoinuka kwanza,  kila kitu huwa kigumu  na kuhisi  uchovu, lakini unapoendelea  kujilazimisha kuondoka,  nguvu inakurudia. Leo niliamka nikiwa sina furaha.  Nilifanya  kazi juma zima kufanya  mkutano  na  bado  nahisi uchovu kiasi.
Vile vile,   nilipata kukasirika  kuhusu jambo  fulani ambalo  nilitarajia.  Nilihisi  nilale kwenye kochi na  kujisikitikia  siku nzima,  lakini kwa  vile kwa  miaka mingi nimefanya  hivyo na sijawahi  kufaulu,  nimeamua kufanya chaguo  lingine.  Niliamua  kuendelea  na kuandika mlango huu kuhusu matendo ninayofanya.  Ilikuwa njia yangu  ya  kupambana dhidi  ya njia ambayo mwili  wangu   ulihisi!  Kadiri ninavyoendelea kuandika, ndivyo ninavyohisi kuwa bora zaidi. Katika  hali ambayo miili  yetu inatujaribu tuwe walegevu, twaweza  kuanza  kushinda kwa  kumuuliza  Mungu atusaidie na kwa kufanya maamuzi muhimu   ya kuwa imara badala  ya kuwa mlegevu.

Kisha tunapoendelea  mbele  na kufanya kulingana  na maamuzi yetu, tutaona  kuwa  hisia zetu zinaanza  kuzoea.  Mungu amenipa roho ya  nidhamu  na kujizuia kwa  siku kama  ya  leo, lakini ni juu yangu  kuchagua  iwapo  nitumie  kile ambacho  Yeye amenipa au nifuate njia za mwili.
Paulo  pia  anaandika  kuhusu “Wakristo  mwili”  ambao  ni watu waliomkubali Yesu Kristo kuwa  mwokozi wao, lakini hawafanyikazi  na Roho  Mtakatifu kuendeleza  ukomavu wao  wa kiroho. Katika  1 Wakorintho 1 3:1-3,  Paulo anawaambia  Wakristo “Lakini, ndugu zangu,  mimi  sikuweza  kusema nanyi kama  na watu wenye tabia ya  rohoni, bali kama  na watu wenye tabia ya  mwilini, kama  na watoto  wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula;  kwa  kuwa mlikuwa  hamjakiweza.  Naam,  hata sasa  hamkiwezi, kwa  maana  hata  sasa  ninyi  ni  watu wa  tabia ya mwilini.  Maana  ikiwa kwenu  kuna husuda na fitina, je? Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenda kwa jinsi ya kibinadamu?” 

Paulo  aliwaambia  Wakristo  alihitaji  kuongea  nao  kama  watu wasio  wa kiroho bali wa  kimwili  ambao  maumbile  yao  ya kimwili yametawala.  Hangeweza  hata kuwafunza mambo ya nguvu bali alizingatia  kile  alichokiita  “jumbe  za  maziwa.”  Aliwaambia  si watu wa  kiroho kwa  sababu waliruhusu  mahitaji  ya  kimwili  yawathibiti. Je,  unaruhusu mahitaji  ya  kimwili  yakudhibiti?  Leo  nilijaribiwa kuwacha  mahitaji ya  kimwili yanidhibiti  na kusema  kweli, pengine nitahitaji  kuzuia jaribu hilo kwa  siku nzima kwa  kufanya  jambo ninaloamini kuwa  litazaa  matunda mema. Siwezi kufuata  mahitaji ya kimwili kwa sababu sina siku ya kupoteza. Hakuna Zawadi ya Kutofanya lolote Hakuna kati yetu anayeweza kupoteza  wakati wetu akikaa  bila kufanya  lolote.  Mungu hawezi kuzawadia  hali ya  kutofanya  lolote. Watu wasiofanya  kitu hawatumii  nafasi yao  kufanya  lile  wanalojua linafaa

Badala  yake,  wanasubiri kuhisi kana  kwamba  wanafanya kitu au  kutiwa  motisha  na  nguvu za  kiajabu kutoka  nje.  Wanatumai kitu kizuri  kitatendeka, hasa  kwao, na wamejitolea  kutofanya lolote ilhali wanasubiri kuona ikiwa kitu kitafanyika.  Mungu hafurahii tabia kama hii, kwanza ni hatari sana. Uamuzi wa  kutofanya  lolote bado  ni uamuzi, na ni uamuzi ambao  hutufanya  sisi tuwe wanyonge na wanyonge sana.  Unampa shetani  nafasi  ya  kutudhibiti zaidi  na  zaidi.  Mahali  patupu bado ni  mahali, na Neno  la Mungu  latufunza kwamba ikiwa shetani atakuja  na  apate utupu, yeye huujaza  mara  moja  utupu huo (angalia Mathayo 12:43-44). Kutokuwa  na lakufanya kwaonyesha kwamba tumekubaliana na kuidhinisha  chochote  kinachoendelea. Kwanza, ikiwa  hatufanyi lolote kuibadili  hali hiyo  basi lazima  tufikirie kwamba chochote kinachotendeka ni sawa.

No comments:

Post a Comment