June Big event Imefanya kitu,Wakati wengine wakifanya Sherehe kubwa ya kuzaliwa Binafsi,wao waliamua katika siku hiyo maalum kwao watafanya kitu kwaajili ya kusaidia wenye uhitaji na kuleta mageuzi ya Upendo.Wengi wa watu hawaitikii kwa namna moja. Kila mmoja anaingiwa na huruma wakati anapoona hali ambapo watu wanaishi katika hali mbaya katika vijiji vya mashambani nchini Tanzania au sehemu nyingine za ulimwengu. Wengi hulia, na wengi hutikisa vichwa na kufikiria hali hizi ni mbaya, lakini wote hawaamui kufanya kitu kubadili hali hizi. Wengi huomba Mungu afanye kitu na wanafurahi kwamba huduma ya June Big Event inayoongozwa na Samwel Shan'ga,jimmy John pamoja na Judith Mbondo inafanya kitu, ilhali hawafikirii kumtafuta Mungu kwa bidii kuhusu kile wanachoweza kufanya wao wenyewe. Ningependa kusema wengi hurejea nyumbani, na kujishughulisha na maisha yao tena, na mara husahau kuhusu kile walichoona.
- Lakini namshukuru Mungu kundi la June Big June Event na baadhi yao ambao wamejitolea kutafuta njia za kuleta mabadiliko. Kumbuka: kutoleta mabadiliko ni kisingizio, bali upendo hutafuta njia. Kila mmoja anaweza kufanya kitu!
Kulala kwenye kochi au kuegemea kwenye kiti maalum kumuuliza Mungu alinde kila kitu kinachohitaji kufanywa ni rahisi, lakini inatuwacha tusiwe na la kufanya na kutozaa matunda na kutuweka wazi kushambuliwa na muovu. Ikiwa akili zetu hazina mawazo mazuri, shetani anaweza kuzijaza mambo mabaya kwa urahisi. Ikiwa tu walegevu na hatufanyi lolote, anaweza kutujaribu kufanya makosa na hata mambo machafu.
![]() |
June Big Event. |
Paulo aliendelea kusema kwamba baadhi ya wajane ambao bado wangali vijana kwa kutokuwa na lakufanya tayari walikuwa wameanza kumgeukia shetani. Ina umuhimu gani kuendelea kuwa imara? Ninaamini maandiko ya Paulo yanathibitisha kwamba ni muhimu. Kwanza, katika maandiko Mungu anatuhimiza sisi tusiwe watu wa kutokuwa na lakufanya. Nyakati za Agano la Kale, wakati mtu alipofariki wana wa Israeli waliruhusiwa kuomboleza mpendwa wao kwa siku thelathini (angalia KUM 34:8). Kwanza, huenda ikaonekana kuwa si muhimu, lakini Mungu alifanya sheria hiyo kwa sababu alijua kwamba muda mrefu wa kuomboleza na kutokuwa na lakufanya unaweza kusababisha matatizo mabaya. Lazima tukae imara tusijihusishe kupita kiasi bali tujihusishe vyakutosha ili tuweze kuendelea katika mwelekeo ufaao. Kujipanga katika mambo tunayoyafanya ni muhimu.
Hatuwezi kutumia muda wetu wote kusaidia watu wengine, lakini kwa upande mwingine, kutotumia muda huo kulingana na mpango huenda kukasababisha matatizo. Ikiwa unaweza kumkumbuka mtu unayemjua asiyekuwa na lakufanya, na ambaye hajishughulishi na jambo lolote pengine pia utatambua kwamba hawana furaha kwa sababu kutojishughulisha na jambo lolote na kukosa furaha mambo haya mawili huwa pamoja. Miaka kadhaa iliyopita shangazi yangu alihitaji kuhamia katika makazi ya kupewa usaidizi. Kwa miaka mitatu au minne ya kwanza alitaka kukaa tu bila kufanya lolote. Alihuzunika kwa vile aliondoka nyumbani na hakuwa na nia ya kushiriki katika maisha mapya yaliyokuweko. Ingawa kulikuwa na shughuli nyingi na hata nafasi za kusaidia wengine, hakutaka kufanya lolote. Siku baada ya siku alikaa tu nyumbani kwake na alivunjika moyo. Alihisi vibaya mwilini na mara nyingine alikuwa na wakati mgumu kukabiliana na hali hii.
Hatimaye alifanya uamuzi kwamba hangeendelea kukaa tu bila kufanya lolote na akajihusisha na mafunzo ya Biblia na kutembelea wagonjwa katika hospitali iliyo karibu na makazi yake. Alicheza michezo, akahudhuria karamu, kukutana na marafiki wengi. Muda si muda alikuwa akinieleza kuwa ana furaha zaidi kuliko alivyokuwa maishani mwake na anahisi vizuri zaidi mwilini. Hali ya mtu mlegevu huanza kuwa mbaya hadi mbaya zaidi hadi ulegevu wake unapoanza kuathiri kila sehemu ya maisha yake. Yeye huruhusu kuyumbushwa huku na huko na mazingira yake na hali ilivyo.
Huwacha hisia zake zimuongoze, na kwavile hajihisi kufanya lolote, yeye hutazama tu na kulalamika huku maisha yake yakisambaratika. Anataka kufanya mambo mengi, ilhali amezongwa na hisia asizoweza kuzieleza.
Anahisi ulegevu na hana mawazo ya ubunifu. Anaweza hata kuanza kufikiria kuwa kuna kitu kilicho kasoro mwilini mwake na hiyo ndiyo sababu hana nguvu. Kwake yeye, maisha yamekuwa urithi wa matatizo mengi. Kujiruhusu kukaa tu bila kufanya lolote mara nyingi hutokea baada ya kupata pigo au msururu wa mambo ya kughadhabisha, au wakati mikasa inapotokea. Wakati mambo kama haya yanapotokea, huenda tukataka kukata tamaa, lakini tunapofanya hivyo, shetani anasubiri kuingia na kuchukua fursa ya hali ilivyo. Hatuwezi kwa sababu yoyote kuruhusu ulegevu kumpa nafasi adui aingie katika maisha yetu.
Je, unaamini kuwa ulimwengu umejaa maovu? Je, unafikiri jambo fulani linapaswa kufanywa kwa watoto wanaokabiliwa na njaa? Je, mtu fulani anapaswa kuwasaidia watu milioni 1.1 ambao hawana maji safi ya kunywa? Je, watu wanapaswa kuishi barabarani na chini ya pango za daraja? Je, familia ambayo umekuwa ukienda nayo kanisani kwa miaka kadhaa na kisha halafu ipatwe na mkasa ni sawa isipopigiwa simu na mtu yeyote kujua ni kwa nini hawajakuwa wakienda kanisa kwa muda wa miezi mitatu? Ikiwa kanisa la dhehebu lingine katika mji wako limeteketea, je, ni sawa kuliombea tu na kutofanya jambo lolote kulisaidia? Je, unaamini mtu fulani anapaswa kufanya kitu kuhusu maovu yaliyoko? Ninafikiri umeyajibu maswali haya yote vizuri, kwa hiyo nina swali moja la mwisho. Utafanya nini? Je, utakuwa “mtu fulani” anayefanya kinachohitajika kufanywa? Ninapouliza kile utakachofanya, pengine unahisi hofu kwa sababu unashangaa “kile utakachofanya” kitakavyohitaji? Ninaelewa hisia za hofu ya namna hii. Kwanza, ikiwa nitaamua kujisahau mimi mwenyewe na kuanza kujaribu kusaidia, ni nini kitafanyika kwangu? Ni nani atakayenijali mimi ikiwa sitajijali mwenyewe? Mungu alisema Atakujali, kwa hiyo nafikiri tunapaswa kutafuta ikiwa kweli anamaanisha kile anachosema. Kwanini tusistaafu kutokana na hali ya “kujijali” na kuona ikiwa Mungu anaweza kazi bora kuliko uliyofanya. Ikiwa tutajali kazi Yake, ambayo ni kuwasaidia watu wanaoteseka, Ninaamini Atatujali.
Mungu awabarikiwi Kundi La June Big Event kwa Kufanya Mageuzi ya Upendo.Wacha niseme tena: Ninaamini kikamilifu tunahitaji Mageuzi ya Upendo. Sote tumejaribu uchoyo, kuvunjika moyo na kujisikitikia na tumeona matunda yake. Ulimwengu umejaa matokeo ya mambo haya. Tuungane kwa kukubaliana kwamba tutaishi maisha ya njia ya Mungu. Kujali kuwa baraka kwa wengine (angalia GAL 6:10). Weka upendo (angalia KOL 3:14). Inamaanisha kuwa imara kwa lengo la kuwafikia wengine. Tazama na omba upate nafasi; kuwa jasusi wa Mungu! Yesu aliinuka kila siku na akafanya mambo mema (angalia MDO 10:38). Inaonekana ni rahisi mno. Ninashangaa jinsi tulivyoukosa wakati huu wote.Endeleeni Kusonga Mbele.
Mwandishi Jimmy J.
Asante kwa ku share habari hii mtumishi...Barikiwa sana.
ReplyDeleteUbarikiwee mtumishi,nimejifunza kitu.
ReplyDelete