Thursday, 31 May 2018

Nisaidie!Niko mpweke.

Shangazi yangu aliniambia kuwa baada ya mjomba wangu kufa, wakati  mwingine alilia usiku huku  akipiga  mto wake na kusema, “Kwa nini uliniacha?” Alijua katika nia yake kwamba hakumwacha kimakusudi, lakini hiyo ilikuwa ni sauti ya hisia zake.
Tunahitaji kujua kuwa hisia  zetu zina sauti, na wakati zinapokuwa zimeumia, basi zinaweza kuitikia hali tunayoipitia  kama mnyama aliyeumia. Wanyama walioumia wanaweza kuwa  hatari,  na hisia zilizoumia zinazweza kuwa hivyo pia tukizifuata na kuzitii. Wakati mtu  ana  msiba,  ni  muhimu  asiache  hisia  zilizoumia zimfanye kuwa mwenye chuki na uchungu moyoni.

Wakati pigo linakuwa ni talaka, ni rahisi kumchukia yule aliyesababisha utengano au hata kujaribu kulipiza kisasi. Usiharibu maisha yako kwa kuendelea kuwa na uchungu moyoni. Badala  yake, mwamini Mungu kuwa anaweza kuchukua yale ambayo yametukia na kukufanya uwe mtu bora zaidi. Jambo hilo  hilo  linalokuumiza  linawafinya  wengi  pia.  Mwombe  Mungu achukue “majivu” yako na akupe “uzuri” badala yake.

Hakuna Mwanaume ambaye ni Kisiwa

Nina hakika  umesikia  mstari maarufu  wa maneno  yaliyosemwa na  John Donne,  kwamba  “hakuna  mwanaume ambaye ni kisiwa.” Maneno haya ni njia ya kueleza ukweli kwamba watu wanahitajiana, yaani kila mmoja anamhitaji mwingine  na kumuathiri  mwingine kwa njia nzuri  au mbaya.  Kama vile  ambavyo maisha ya  ya huyu yaliniathiri mimi  kwa  njia mbaya  na  maisha  ya  Huyu yakaniathiri kwa  njia nzuri, maisha yetu yanaweza  kuwaathiri watu wengine.

Yesu  alituambia tupendane  kwa  sababu hiyo ndiyo njia pekee  ya ulimwengu kufahamu kuwepo kwake (angalia Yohana  13:34-35). “Amri  mpya  nawapa,  Mpendane.  Kama  vile nilivyowapenda  ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote  watatambua ya kuwa  ninyi  mmekuwa wanafunzi wangu,  mkiwa na upendo  ninyi kwa ninyi.”   Mungu  ni  upendo, na wakati tunapoonyesha upendo katika  maneno yetu na  vitendo,  tunawaonyesha  watu vile Mungu alivyo. Paulo alisema kwamba  sisi  ni  mablozi wa Mungu, waakilishi Wake, na kwamba Yeye Anauhimiza ulimwengu kupitia sisi (angalia 2 KOR 5:20).

Wednesday, 30 May 2018

Je, kuna tofauti gani kati ya unyakuzi na kurudi mara ya pili?

kunyakuliwa na ujio wa pili wa Kristo mara nyingi huchanganyishwa. Wakati mwingine ni vigumu kujua kama maandiko aya yanamaanisha kunyakuliwa au kuja mara ya pili. Hata hivyo, katika kusoma unabii wa Biblia wa nyakati za mwisho, ni muhimu sana kutofautisha kati ya haya mawili.

Unyakuo ni wakati Yesu Kristo atakaporudi kuondoa kanisa (waumini wote katika Kristo) kutoka duniani. Kunyakuliwa ni kama ilivyoelezwa katika 1 Wathesalonike 4:13-18 na 1 Wakorintho 15:50-54. Waumini waliokufa watapata miili yao itakayofufuliwa, pamoja na waumini ambao bado wanaishi, watakutana na Bwana hewani. Hii yote hutokea katika dakika moja, kufumba na kufumbua. Kuja mara ya pili ni wakati Yesu atakaporudi kumshindwa Mpinga Kristo, kuharibu maovu, na kuanzisha ufalme wake wa milenia. Kuja mara ya pili ni kama ilivyoelezwa katika Ufunuo 19:11-16.

KIUMBE KIPYA ALIYE NA TUMAINI LA SIKU ZA USONI


  •  Biblia inatufundisha kuwa tunapozaliwa mara ya pili kwa kumpokea Kristo kama mwokozi wetu, sisi hufanyika viumbe vipya. 2 Wakorintho 5:17 inatueleza: Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefi ka. Inasisimua kutambua kuwa wakati tunapozaliwa mara ya pili, hali yetu ya kale ya kiroho na kitabia huondolewa na kupita kabisa, na tunapata nafasi ya mwanzo mpya. Mimi hufananisha maisha haya mapya kama udongo wa kiroho.  

Nafasi tuliyo nayo ya kuwa na maisha ya ajabu haina kipimo. Hata hivyo inatupasa kushirikiana na Roho Mtakatifu kutimiza mpango wake katika maisha yetu. Itatubidi kujifunza mengi, lakini la kusisimua ni kuwa maisha yetu ya kale yamezikwa na  Yesu, nasi tumefufuliwa katika maisha mapya pamoja naye. Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende. Waefeso 2:10
Kama viumbe asili vya Mungu, tulikuwa bila hatia yoyote.  Lakini tulidanganywa na kuharibiwa na shetani.  Habari njema ni kwamba tunafanywa upya katika Kristo  Yesu. Mpango wa Mungu kwetu ni kwamba tufanye matendo mema, na tuwe wawakilishi wake duniani.

Monday, 28 May 2018

JE UMEZALIWA MARA YA PILI?

  

"Nilizaliwa mara ya pili nikiwa na umri wa miaka tisa na bado ninakumbuka sana nilivyojihisi kana kwamba nilisuguliwa ndani. Nilijihisi msafi , mwepesi, upya na mchangamfu ndani yangu."-jimmy

Inamaanisha nini kuzaliwa mara ya pili?  Katika kitabu cha  Yohana Mtakatifu 3:3   Yesu alisema, “Amini, amini, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”Nikodemo ambaye  Yesu alikuwa akimzungumzia hapa alisema “Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee?  Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” (Yohana Mtakatifu 3:4) Labda wewe pia unafi kiri vivyo hivyo.

Je mtu awezaje kuzaliwa ambaye tayari ameshazaliwa?  Yesu anazungumzia kuzaliwa kiroho. Hapo mbeleni nilisema wewe ni roho, una nafsi na unaishi katika mwili.   Mwili wako tayari umezaliwa lakini Biblia inafundisha kwamba roho na nafsi zetu zimekufa na zimejaa giza kwa sababu ya dhambi.
  • Unaweza kujitazama katika kioo, ukatingiza kichwa chako, mikono na miguu. Unavuta pumzi. Unaweza kusema uko hai. Lakini je, yule “wewe wa kweli” yuko hai?
  • Je uko hai na una nuru ya kutosha ndani  yako? Una amani? Je  nafsi yako ina amani na utulivu? Je unajipenda? Una furaha na tumaini?  Je unaogopa kifo? Haya ni maswali unayopaswa kujiuliza mwenyewe.

KUCHANGANYIKIWA HUSABABISHWA NA NINI?

Je, umechanganyikiwa?  Kuna kitu kinachotendeka maishani mwako sasa hivi ambacho hukielewi?  Pengine ni maisha yako ya kale, ambayo huelewi ni kwa nini yalikuwa jinsi yalivyokuwa.  Unaweza kuwa ukisema, “Kwa nini mimi, Mungu?  Ni kwa nini mambo hayakutendeka hivi au vile?  Ni kwa nini mambo yalitokea hivi?  Sielewi mimi!” Nilianza kuelewa kuwa watu wengi husumbuliwa sana na matatanisho au kuchanganyikiwa.  Nilishapitia haya katika maisha yangu ya kale kwa hivyo nilielewa jinsi utatanishi huwatesa watu. Nilianza kuwaza na kujiuliza ni kwa nini watu huchanganyikiwa na wanawezaje  kuepukana na kuchanganyikiwa?


Nilipoyatafakari haya niliuliza Bwana anionyeshe ni kitu gani kinachosababisha kuchanganyikiwa.  Akasema, “Waambie waache kujaribu kutatua kila kitu, na hawatachanganyikiwa tena.”  Sasa nimegundua kwamba hii ndio sababu sichanganyikiwi tena.  Ningali na mambo mengi maishani mwangu ambayo siyaelewi, lakini kuna tofauti kubwa sasa. Mungu ameniweka huru kutokana na kujaribu kutatua kila jambo.  Ameniweka huru kutoka kwa “kuwaza na kuwazua” jinsi 2Wakorintho 10:5 inavyosema.  Kwa hivyo sijaribu kutatua na kuelewa kila kitu maishani mwangu tena. 

NIA YA IMANI


  • Tunaweza kusema kwamba imani ni mafundisho au njia ya kupokea kutoka kwake Mungu.  Katika  Waefeso 2:8,9 tunaona kwamba tumeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani.   Waraka kwa  Waebrania 11:1(AMP) inasema, “Basi imani ni kuwa na hakika ya…mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” 

 
Tunaweza kueleza maana ya neno imani kwa njia tofauti lakini ninaamini kuwa njia rahisi ya kutazama imani, na hata kujichunguza kuona kama tuna imani ni kusema kwamba “imani ina nia.” Nia ya imani inatuleta katika pumziko.

"KUWAZA NA KUWAZUA "HULETA KUDANGANYA


Katika siku za leo, tegemeo letu moja la kutukinga kutokana na udanganyifu ni kujifunza kutembea kwa Roho Mtakatifu – kuongozwa na Roho, sio mwili.  Shetani anawatafuta  Wakristo wanaoongozwa na vichwa vyao, hisia na wosia zao badala ya kuongozwa na Neno, na Roho Mtakatifu.  Hatufai kutenda tendo kwa sababu tunajihisi kufanya hivyo tu. 


Ni lazima, kwa ajili ya ufalme wa Mungu na pia ili kujihifadhi, tutende matendo yaliyoongozwa na Roho Mtakatifu. Akili ya binadamu inapenda kuweka vitu kwa mpangilio fulani.  Inapenda kuweka kila kitu mahali pake ili kieleweke na kutunzwa.  Hatupendi kuwa na maswali yasiyojibika. 

Mojawapo ya vyombo ambavyo Roho Mtakatifu hutumia kusulubisha miili yetu ni maswali yasiyojibiwa.  Tusipojua  jibu, basi tunalazimika kumwamini Mungu, au kuwa na wasiwasi tukijaribu kutatua jambo hilo. Roho Mtakatifu ana kazi ya kumlea muumini kutoka wakati anapookoka hadi wakati anapokomaa. Muumini ambaye anaweza kumwamini Mungu wakati mambo hayaeleweki ni muumini aliyekomaa.

CHANZO CHA TATIZO


  • "Nilidhulumiwa  kingono  na  baba  yangu  mzazi  kwa  miaka  mingi. Nilijaribu mara  mbili  tofauti  kumwambia mtu fulani  kilichokuwa kikitendeka  kwangu  na kwa  vile  hawakunisaidia,  niliendelea kuteseka peke yangu  hadi nikawa  mtu mzima na  hatimaye nikaanza kuzungumza  hadithi yangu  na  watu wengine na  nikapokea. uponyaji kutoka  kwa  Mungu."


ULIMWENGU UMEPOTEZA LADHA YAKE



 
  • Nafikiri ni salama  kusema kwamba  vingi ya  vile  ambavyo ulimwengu hutoa  havina ladha…na  sizungumzi kuhusu  chakula. Kwa  mfano, nyingi ya  sinema zinazotayarishiwa  Hollywood  hazina ladha.  Maongezi mengi na picha  hazina  ladha  nzuri. Mara  nyingi wakati tunapoona  tabia  yoyote  isiyofaa  tunakimbilia “kuulaumu ulimwengu.”  Twaweza kusema  kitu  kama “Ulimwengu  unakwenda wapi?”  Ilhali neno “Ulimwengu linamaanisha  watu wanaoishi ulimwenguni.
Ikiwa  ulimwengu hauna  ladha,  ni kwa  sababu watu wamekosa  ladha katika fikra zao  na matendo. Yesu  alisema kwamba sisi ni chumvi ya  ulimwengu, lakini ikiwa  chumvi imepoteza  ladha yake (nguvu yake na ubora  wake), haifai (angalia  MAT. 5:13). Pia alisema kwamba  sisi ni nuru ya  ulimwengu na hatupaswi kuifunika nuru yetu (angalia MAT. 5:14).

Hebu  fikiria  hivi:  Kila  siku  unapoondoka nyumbani  kwako kwenda gizani,  ulimwengu usio na  ladha,  je,  unaweza  kuwa  nuru na ladha inayohitajika? Unewaza  kuleta furaha  kazini pako kwa kujitolea kuwa  na fikra  za  kiungu. Kupitia mambo madogo kama vile  kuonyesha  shukurani badala  ya  kulalamika kama vile  ambavyo watu  wengi hufanya,  kuwa  mvumilivu,  mwenye huruma,  kusamehe haraka  makosa,  kuwa  mkarimu, na  kuwa  mtu wa  kuwatia  moyo wengine.
Hata kuonyesha tabasamu kiasi na kuwa na urafiki  ni njia ya kuleta ladha nzuri  katika jamii iliyokosa  ladha.  Sijui  kuhusu wewe,  lakini mimi  sipendi  chakula  kisichovuti Rafiki yangu alikuwa  na  tatizo  la  tumbo wakati fulani na  daktari  akamshauri atumie chakula kisicho  na  ladha  nzuri kwa  siku chache.  Kama ninavyo  kumbuka,  wakati huo hakutaka  kula chakula.  Ingawa yeye si mtu anayependa kulalamika,  lakini katika  kila mlo, nilimsikia  akisema kila mara,  “Chakula hiki hakina ladha  kabisa.”  Kilihitaji  chumvi kidogo, viungo kiasi... na hivyo ndivyo ulimwengu unavyohitaji.
Bila  upendo na  ubora  wake wote,  maisha  hayana  ladha  na hayastahili  mtu kuishi. Nataka  wewe uyajaribu. Hebu fikiria: Ninaenda  katika ulimwengu  leo  na kurekebisha mambo.  Kisha jipange akilini mwako  kabla  ya  kutoka  kwenye mlango  wako  kwamba unaenda nje  kama  balozi wa  Mungu  na kwamba  lengo lako ni  kuwa mtoaji,  kuwapenda watu unaokutana  nao siku  nzima. Tabasamu ni ishara ya kukubaliwa na kuidhinishwa  jambo ambalo watu wengi ulimwenguni  wanahitaji.

Jiweke akiba  kwa  Mungu  na umwamini ili  akulinde  unapopanda  mbegu nzuri  kila mahali uendako kwa kufanya maamuzi yatakayokuwa baraka kwa wengine.         Mabadiliko Huanza na Wewe Ninatambua kwamba  huwezi kufanya kila kitu; Sidadisi  jambo hili kabisa.  Ni lazima  ukatae  mambo fulani ama  sivyo  maisha  yako yatajaa  mambo  mengi na  kukufanya  kuwa  mchovu wa  akili kila mara.



Siwezi kujitolea kuwapa  mafunzo watoto  au  kuwapa  mlo wakongwe, lakini ninafanya  mambo  mengine  mengi ili  kuleta tofauti ifaayo ulimwenguni. Nafikiri  swali ambalo  kila mmoja wetu lazima ajibu  ni, “Ni nini  nitakachomfanyia  mtu mwingine  ili  awe na maisha bora?”  Na pengine  swali bora zaidi ni,  Nimefanya nini  leo kumfanya  mtu mwingine aishi maisha  bora?”  Somo hili huenda likawa  gumu kukisoma  wakati mwingine kwa  sababu natumai kitaleta  maswali  yenye utata.  Lakini yanahitaji  kushughulikiwa na  kila  mmoja  wetu.  Hakuna  kizuri kinachotendeka  kiajali.  Ikiwa twataka  kuwa sehemu  ya Mageuzi, inamaanisha kuwa mambo lazima  yabadilike,  na  mambo  hayawezi  kubadilika  hadi  pale  watu watakapoyabadili. Kila  mmoja wetu lazima aseme:  Mabadiliko yanaanza na mimi!.

JE,UMECHOKA KUNGOJA....?


Kama umekuwa ukingoja kwa muda mrefu na hujaona ukipiga hatua za kwenda mbele, haikosi unaanza kuwa mchovu  sana kwa kungoja. Nataka kukutia  moyo kufanya upya nia yako kuhusu kungoja.

Katika  Marko 4:20-27 Biblia inasema kwamba yafaa tuwe na subira kama mkulima awekaye mbegu yake kwenye ardhi kisha anaingoja mvua ya awali na ya baadaye. Neno linaendelea kusema kwamba aingojeapo mbegu  kumea, yeye  huamka na kulala, na  mwishowe  mbegu ile  humea.  Naye, mkulima  hajui inavyotendeka.