Nilipoyatafakari haya niliuliza Bwana anionyeshe ni kitu gani kinachosababisha kuchanganyikiwa. Akasema, “Waambie waache kujaribu kutatua kila kitu, na hawatachanganyikiwa tena.” Sasa nimegundua kwamba hii ndio sababu sichanganyikiwi tena. Ningali na mambo mengi maishani mwangu ambayo siyaelewi, lakini kuna tofauti kubwa sasa. Mungu ameniweka huru kutokana na kujaribu kutatua kila jambo. Ameniweka huru kutoka kwa “kuwaza na kuwazua” jinsi 2Wakorintho 10:5 inavyosema. Kwa hivyo sijaribu kutatua na kuelewa kila kitu maishani mwangu tena.
Inaonekana kama kazi rahisi, sivyo? Lakini kuna uhuru wa kweli kutoka kwa mateso ya utatanishi ikiwa tutakataa jaribio la kutatua mambo yote. Ukitulia na kutafakari maneno haya utaelewa ukweli maana vita hivi hufanyika mahali paitwapo “mawazoni.” Vita vya kiroho hufanyika katika mawazo yetu, na hapo ndipo tunashinda au kushindwa. “Mungu si mwanzilishi wa machafuko” (1Wakorintho 14:33) – bali ni Shetani.
Shetani hutupatia maoni na mawazo yasiyo sawa na neno la Mungu. 2 Wakorintho 10:4,5 (AMP) inasema mojawapo ya fi kra tunazohitaji kuondoa ili tushinde vita ni kuwaza na kuwazua. Mistari hii inasema: “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, (silaha za nyama na damu), bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,“(Mradi) tupinge mabishano na mafi kira na mawazo na kila kitu kilicho na kiburi, kilichoinuka, kijiinuacho juu ya (ukweli wa) elimu ya Mungu, na kuteka nyara kila fi kira ipate kumtii Kristo (aliye Masihi, Mpakwa mafuta wa Mungu).” 1 Wakorintho 10:4,5
- Ikiwa neno la Mungu linatufunza kutowaza na kutotatua kila kitu, basi inafaa tulitii. Na mawazo yakitujia, tunafaa kuyaleta chini yapate kumtii Kristo. Maandiko haya yanasema kwamba tu vitani, na vita vyetu, mapigano yetu, yamo mawazoni mwetu. Shetani huvamia mawazo yetu.
Kulingana na maandiko haya, tunapambana na uvamizi na fikra za shetani. Umewahi kuwaza mambo ambayo si kweli au kuona picha mawazoni mwako ambayo si njema? Fikra za kukisia ni aina ya njama na mawazo kuhusu jinsi ya kujitatulia shida zako.
Kuwazua ni kujaribu kutafuta majibu kwa maswali ambayo ni Mungu tu anayeweza kuyajibu. Kwa kukamilisha sura hii, wacha tuseme kuwa kuchanganyikiwa husababishwa na kule kujaribu kusuluhisha au kupata jibu kwa swala ambalo ni Mungu tu anayeweza kulitatua. Kwa sababu moja au nyingine Mungu pekee ndiye majibu lakini hamwambii yeyote.
No comments:
Post a Comment