Ni lazima, kwa ajili ya ufalme wa Mungu na pia ili kujihifadhi, tutende matendo yaliyoongozwa na Roho Mtakatifu. Akili ya binadamu inapenda kuweka vitu kwa mpangilio fulani. Inapenda kuweka kila kitu mahali pake ili kieleweke na kutunzwa. Hatupendi kuwa na maswali yasiyojibika.
Mojawapo ya vyombo ambavyo Roho Mtakatifu hutumia kusulubisha miili yetu ni maswali yasiyojibiwa. Tusipojua jibu, basi tunalazimika kumwamini Mungu, au kuwa na wasiwasi tukijaribu kutatua jambo hilo. Roho Mtakatifu ana kazi ya kumlea muumini kutoka wakati anapookoka hadi wakati anapokomaa. Muumini ambaye anaweza kumwamini Mungu wakati mambo hayaeleweki ni muumini aliyekomaa.
Kwa hivyo Mungu hatujibu maswali yetu yote wakati wote maana anatufunza tumaini. Walakini, ni lazima ukumbuke kwamba nia zako zinapingana na mpango huo wa Mungu. Nia zako hutokana na asili yako ya ubinadamu na ni sawa na mwili, hadi zitakapofanywa upya, ili zifunzwe kuwaza mawazo ya kiroho.
Wagalatia 5:17 (AMP) inasema, mwili hushindana na Roho, na Roho hushindana na mwili, na yote mawili hupingana na kugongana wakati wote. Turudi mpaka mwanzo wa sura hii tuliposema kwamba akili ya binadamu inapenda kuweka vitu kwa mpangilio fulani, kana kwamba katika vijisanduku, ambapo vitatoshea na havitatoka bila yetu kujua. Tulikuwa na vijisanduku vya barua afi sini mwetu wakati mmoja. Kila kijisanduku kilikuwa na jina moja la mfanyikazi. Nilipotaka kumtumia mfanyikazi fulani ujumbe au agizo, niliweka kijibarua katika kijisanduku chake. Wakati mwingine nilichohitaji kifanywe na mfanyikazi fulani hakikufanywa na nilipochunguza niligundua kwamba nilikuwa nimeweka barua ya mfanyikazi yule katika kijisanduku kisicho chake. Na wakati mwingine nilikuwa nimeweka barua katika kijisanduku kisicho na jina. Bwana alitumia vijisanduku hivi kunifunza fundisho ninalojaribu kukufunza. Alinionyesha kwamba kama tu nilivyoweka barua ndani ya kijisanduku tofauti pale afi sini, huwa ninaweka mambo katika kijisanduku kisicho sawa kichwani mwangu. Wakati wote nilitaka kuweka kila kitu mahali fulani mawazoni mwangu kama kifurushi kilichokamilika na kufungwa vizuri, yaani kisicho na hali yoyote itakayonihitaji kumtegemea Mungu. Nilikuwa na shida kubwa ya “kuwaza na kuwazua.”
Mara nyingi niliuliza, “Kwa nini, Mungu, kwa nini?”, na ndio sababu nilikuwa nimechanganyikiwa, na kuwa na wasiwasi, na kukosa amani na furaha. Bwana pia alinionyesha kuwa nilikuwa nimejidanganya maana wakati mwingine nilidhani kwamba nimetatua kila kitu kuhusu jambo fulani, na nilitenda au kutotenda lolote kulingana na fi kra zangu. Lakini baadaye niligundua baada ya kuharibu, ingawa nilidhani nilijua au nilielewa, au nilikwisha kutatua kila kitu, kwamba, nilikuwa nimeweka mambo yale katika kijisanduku tofauti mawazoni.
Mungu alitumia Mithali 3:7 (AMP) kutia nguvu somo hili kwangu. “Usiwe mwenye hekima machoni pako.” Bwana alinijulisha kwamba mimi si hodari kama nilivyodhani. Sisemi kuhusu uhodari wa akili.
Ninazungumzia jinsi tunavyojifi kiri – tunavyojitatulia mambo yote. Mithali 3:5-6 (AMP) inasema: “Mwegemee, mtegemee na kumtumaini BWANA kwa moyo wako wote na akili zako, wala usitegemee maarifa au fahamu zako. Katika njia zako zote mjue, mtambue na kumkiri Yeye, naye ataongoza na kunyosha mapito yako.” Mungu akinyosha njia zako, hutachanganyikiwa au kuwa na mashaka lakini ukiwaza na kuwazua, na ukijaribu kutatua mambo yote, utazunguka katika mizunguko na utakosa kujua ukweli. Mstari wa 7 (AMP) unasema, “Usiwe mwenye hekima machoni pako.” Hapa kuna njia mbili za kushughulikia jambo: moja ni sawa na nyingine si sawa; moja ni ya kiroho na nyingine ni ya kimwili. Tuseme kwa mfano, mtu anitolee unabii wa kibinafsi ambao siuelewi, au nione ndoto ya kiroho ambayo siielewi. Ninaweza kwenda kwake Baba na kusema, “Baba sielewi haya. Ningependa kuelewa, kwa hivyo ninakuomba unipe ufunuo. Nipe ufahamu.” Kisha ninaliweka jambo lile nisilolielewa dakani au kabatini. Yaani silifi kirii tena. Ninaliweka mikononi mwa Mungu. Wakati Mungu atakapokuwa tayari kunipa ufahamu, atayatoa dakani na kuyaleta mawazoni mwangu.
Yohana 14:26 inasema Roho Mtakatifu hutukumbusha mambo yote. Ataniwezesha kujua kupitia ufunuo wake, yale ambayo singeweza kutatua. Njia ya pili ninayoweza kutumia kushughulikia jambo hili ni kujaribu kufafanua ndoto na unabii huu kupitia ujuzi wangu. Ninaweza kuuliza watu wengi wanipe maoni yao. Hebu niseme kwamba wengi wao watanipa maoni tofauti tofauti ambayo yatanichanganya zaidi.
Mwishowe, nitakapofi kia kiwango cha kufi kiri kwamba nimelielewa jambo lile na kutatua ugumu wake nitaanza kutenda kulingana na vile ninavyoona. Ukweli ni kwamba ningalitulia na kufuata ukweli moyoni, itabidi niseme sina amani moyoni. Nikiendelea kujaribu kufanya kitu kitendeke kulingana na “maoni yangu” kuhusu ndoto hii, unabii au maono haya, mwishowe nitafanya uharibifu mkubwa sana. Kumbuka “kuwaza na kuwazua” huleta matatanisho. Sisemi kuwa hatufai kufi kiri juu ya mambo yatujiayo, lakini kuna tofauti kati ya kutafakari jambo kwa muda uliotosha ili upate ufahamu, na kujaribu kutatua jambo kwa nguvu zako zote mpaka unachanganyikiwa kabisa. Ukijihisi kama umechanganyikiwa, wacha iwe onyo kwamba unasuluhisha jambo kwa njia isiyo sawa.
No comments:
Post a Comment