Na Je, Ikiwa watakucheka? Na Je, Ikiwa utakataliwa? Na kadhalika. Unatambua mtindo huu wa mawazo? Na Je, Ikiwa ni njia nyingine ya kujaribu kutatua kila kitu kwa “kuwaza na kuwazua.”
Mawazo haya hutujia na kufuatwa na fi kra nyingi ambazo hutupa picha mbaya. Na Je, Ikiwa hutupeleka hadi siku ya kesho na kutupa hofu ya mambo ambayo hayajatendeka, na labda hayatatendeka ila tuyasababishe kutendeka kupitia kwa ya hofu yetu. Na Je, Ikiwa huleta kuchanganyikiwa sawa na vile Kama Ingalikuwa huleta kuchanganyikiwa. Hizi ni aina mbili za fi kra ambazo hatufai kujiingiza kwazo. Zote zinapatikana katika 2 Wakorintho 10 na zimejumuishwa katika, “kanuni na mawazo” (AMP) na “madhanio”, yote, ambayo yanafaa kuangushwa chini.
Hebu nikupe mfano wa kile ninachomaanisha. Wakati mmoja huduma yetu ilikuwa ikihitaji jengo la kufanyia mikutano yetu ya mafundisho kila wiki. Jengo tulilokuwa tukitumia kwa miaka mitano lilikuwa litabomolewa baada ya miaka miwili ili maduka yajengwe pale. Tulianza kutafuta mahali pengine ambapo pangetosheleza mahitaji yetu kama vile kuwa na mikutano yetu kila wiki, mahali pa kanisa la watoto, mahali pa kutuliza watoto wachanga wakati wa mahubiri, nafasi ya afi si zetu, na nafasi ya kutosha kupokea watu zaidi kadri huduma yetu itakavyokua, na kadhalika. Tulihitaji pia nafasi 300 za kuegesha magari. Sasa wengine wetu tunaweza kufi kiri eti kupata mahali kama hapo ni jambo rahisi; bali halikuwa rahisi kama tungelitaka kufi kiri. Tulikuwa tumetafuta kwa miaka miwili. Tulikuwa tumejaribu kila kitu tulichojua.
Ilionekana kama tulikuwa tumefi kia mwisho. Shetani alitutupia mishale ya moto kama: “Na Je, Ikiwa” miaka hii miwili itapita kabla hamjapata jengo?” Au mshale mwingine wa moto ulitupwa kwetu ukiwa na ujumbe kama huu: “Kama mngalichukua mahali pale pengine awali wakati bei yake ilikuwa chini hamngekuwa na shida hii sasa. Na Je, Ikiwa hamkumsikia Mungu vizuri? Kama mngalijua zaidi kuhusu mambo haya pengine mngejua la kufanya. Na Na Je, Ikiwa mtanunua rasilimali halafu mkose kupata vyeti mnavyohitaji? Je, Ikiwa mtanunua mahali halafu mpate mahali pengine pazuri zaidi na pa bei nafuu zaidi?”
Ninamshukuru Mungu kwa sababu alikwisha kunipa uhuru kutokana na kifungo cha kuwaza na kuwazua kabla ya jambo hili la kuhitaji jengo kuja kwetu. Kama tungalipata shida hii awali, ningejihuzunisha, ningechanganyikiwa na hata kuhofu kwa sababu ya kujaribu kutatua mambo haya yote.
Sasa nimeweza kuamini kwamba, hatua zetu zinaimarishwa na BWANA. (Zaburi 37:23) Bado tungali tunaomba na kumwamini Mungu, na tunataka mapenzi yake yafanyike. Kwa hivyo, atatuongoza na kutuonyesha mahali pazuri kwa wakati unaofaa.
Mungu haji mapema, lakini hachelewi kamwe. Tulikuwa na mipango tofauti ambayo tulijaribu kuifwatilia zamani ambayo haikufaulu, hata tulipotia bidii yote. Lakini kwa wakati mwema Mungu alitupa mahali pazuri pa kukodisha, na atazidi kutupa msaada katika kila hatua. Sasa ninaweza kutazama mambo tofauti na kuona kwamba hayangekuwa sawa. Lakini wakati huo ilionekana kana kwamba nilikuwa ninatia bidii nyingi kupata mahali lakini hakuna chochote kilichofanyika. Hakuna chochote kitakachotendeka ikiwa tuko nje ya wakati wa Mungu, tukijaribu kujifanyia mambo yatendeke. Hakika Mungu anajua anachofanya. Amesimamia yote. Ninaweza kupumzika na kujua kwamba hata nisipojua la kufanya, ninamjua Yule anayejua. Je wewe? Unamfahamu Yesu? Ikiwa unamjua, basi unamjua Mjua-yote, Jabari, na Aliye kila mahali kila wakati – Yule aliye na nguvu zote, ajuaye yote, na aliyeenea kila pahali wakati wote. Tulia! Na Je, Ikiwa utawaza na kuwazua mpaka udhani umeelewa kila kitu, halafu Mungu akushangaze kwa kufanya jambo hilo kwa njia usiyoitarajia?
Muda huo wote utakuwa umeharibiwa. Si kufikia sasa umeuharibu muda wa kutosha katika mawazo ya kuchanganyikiwa? Hapa nina ushawishi kwako: Na Je, Mbona usitulie na kumwacha Mungu awe Mungu?
No comments:
Post a Comment