- Tunaweza kusema kwamba imani ni mafundisho au njia ya kupokea kutoka kwake Mungu. Katika Waefeso 2:8,9 tunaona kwamba tumeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. Waraka kwa Waebrania 11:1(AMP) inasema, “Basi imani ni kuwa na hakika ya…mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
Tunaweza kueleza maana ya neno imani kwa njia tofauti lakini ninaamini kuwa njia rahisi ya kutazama imani, na hata kujichunguza kuona kama tuna imani ni kusema kwamba “imani ina nia.” Nia ya imani inatuleta katika pumziko.
Waebrania 4:3 inasema wale walioamini wataingia katika pumziko na raha yake. Sura hiyo pia inasema, yeyote atakayeingia pumziko au rahani mwake (kumbuka, imani ndio njia ya kupata pumziko na raha), ametoka katika uchovu na uchungu wa kazi za binadamu. (Mstari wa 10.) Kuwaza na kuwazua ni kazi inayoleta kuchanganyikiwa, wala si pumziko na raha.
Nia ya imani husema, nitatwika fadhaa zangu kwake maana yeye hujishugulisha sana kwa yale yanayonihusu. (1 Petro 5:7) inasema, si lazima nielewe na kujua kila kitu kinachoendelea.
Ninatosheka kumjua Yule ajuaye yote . (Maneno ya Ziada ya Mtumishi) Tumia wakati wako kumfahamu Mungu badala ya kujaribu kutatua kila kitu anachofanya. Nia ya imani haina wasiwasi, usumbufu au tafrani kuhusu kesho maana imani inaelewa kuwa mahali popote inapohitajika kwenda, hata ikiwa mahali pasipojulikana, Yesu ameshatangulia. Kumbuka Yeye ndiye Aliyeko, Aliyekuwako na Atakayekuja. Alikuwepo kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu.Alisaidia katika kazi ya uumbaji wa ulimwengu.
Alikujua kabla hujazaliwa. Alikuunga na mikono yake tumboni mwa mamako. Hakuwepo mwanzoni tu, bali Yeye ndiye Mwanzo, Yeye ni Alpha.
Na kuhusu kukamilisha je?Mungu huanza kazi halafu akaiwachia njiani? Lah! Yeye atakamilisha alichoanzisha. (Waebrania 12:2; Wafi lipi 1:6) Atakuwepo wakati wa mwisho. Yeye ndiye Mwisho, Yeye ni Omega. Ninapenda kusema hivi, “Yeye si Alpha na Omega, Mwanzo na Mwisho tu, bali Yeye ni kila kitu kati ya mwanzo na mwisho.” Ikiwa Yesu atakawia kurudi, wewe pamoja nami tuna “kesho” nyingi zinazotungoja. Ninafurahi na kutulizwa kwa sababu ninajua kwamba chochote kitakachonifanyikia kesho, Mungu ameniweka, pamoja na mambo ya kesho, katika vitanga vya mikono yake. (Isaya 49:16) Nia ya imani hutuwezesha kuishi siku moja hadi nyingine au hatua kwa hatua.
Get Your Hopes Up.
No comments:
Post a Comment