Monday, 28 May 2018

JE,UMECHOKA KUNGOJA....?


Kama umekuwa ukingoja kwa muda mrefu na hujaona ukipiga hatua za kwenda mbele, haikosi unaanza kuwa mchovu  sana kwa kungoja. Nataka kukutia  moyo kufanya upya nia yako kuhusu kungoja.

Katika  Marko 4:20-27 Biblia inasema kwamba yafaa tuwe na subira kama mkulima awekaye mbegu yake kwenye ardhi kisha anaingoja mvua ya awali na ya baadaye. Neno linaendelea kusema kwamba aingojeapo mbegu  kumea, yeye  huamka na kulala, na  mwishowe  mbegu ile  humea.  Naye, mkulima  hajui inavyotendeka. 


Mungu amenifundisha kupitia kwa andiko hili kuendelea kuishi maisha  niliyo nayo sasa  nikiwa ninayangojea mambo  niliyo nayo moyoni kuja kuoenekana na kutimia. Tunaweza kuwa tumetilia mkazo sana kujaribu kuzalisha kilicho mbele yetu kiasi cha kwamba tunasahau kuchunga na kufurahia tulicho nacho mkononi. Mimi  nilikuwa na maono  kutoka kwa Mungu miaka kumi kabla sijaanza  kuyaona yakitimizwa.  Katika muda  wa miaka hiyo, naamini  nilikosa  furaha nyingi  huku nikijaribu kuzalisha kitu hicho nje ya wakati ulioteuliwa na Mungu.
Tuseme mwanamke aliye na watoto watano atunge  mimba na kuwa  mja mzito. Kama angelijaribu  kumzaa yule  mtoto  wa sita katika  mwezi wa kwanza wa mimba ile, hilo lingeonekana  jambo la kipumbavu.

Na je, kama angejishughulisha  sana kumzaa yule mtoto kiasi cha kukosa kuwachunga ipasavyo wale wengine watano alio nao tayari? Tunaweza kuona kwa urahisi na wazi upumbavu wa kitendo kama hicho.

Ukweli ni kwamba, watu mara nyingi hufanya jambo sawa na hilo katika hali zingine. Furahia  mahali  uliko  ukingojea  kufika  mahali  unataka  kwenda!  Biblia inaposema  kwamba mkulima  huamka  na  hulala, naamini inamaanisha yeye huendelea kuishi maisha yake ya kwaida kila siku, huku akingoja shamba lake lijae mimea iliyochipuka jinsi anavyotarajia.

Siku moja, mchungaji fulani alitupokea katika  uwanja wa ndege uliojaa umati wa watu. Kazi aina mbali mbali zilikuwa zinaendelea kila mahali. Vifaa vya kupanda ngazi vilikuwa na milolongo, na mikahawa ilikuwa na milolongo. Ilionekana kana kwamba popote tulipogeuka tulikuwa tunangoja tu. Nikaona kwamba  mchungaji  yule alikuwa ameanza  kuudhika na hali hiyo. Mara tu alinigeukia na kusema,  “Nadhani unaweza kuona kwamba singojei vyema.” Wakati wowote hatujangojea vyema, matokeo ni wazi, sio tu katika mienendo yetu inayojidhihirisha katika  hisia zetu, bali pia katika miili  yetu. Kungojea  ni sehemu  kubwa sana  ya maisha,  na kama kungojea kila mara huleta masumbuko moyoni, matokeo yake ni kwamba huleta wasiwasi  ambayo mwishowe  huidhuru miili yetu na yenye uwezo wa kuleta magonjwa.  Mchungaji huyo ambaye hakuwa “anangoja vyema” alikuwa mgonjwa sana wakati huo na ugonjwa amabao dakatri alisema ulikuwa umeletwa na miaka mingi ya kuishi na wasiwasi  nyingi.  Fanya upya nia yako  kuhusu kungoja, nawe hutauona ugumu kungoja. Kusema kweli  sisi hutumia muda mwingi maishani mwetu tukingojea kuliko muda tunaotumia kupokea. Baada ya kupokea tulichokuwa tukingojea, tutaanza kungojea kitu kingine.

Kama unaweza kuona ninachomaanisha, utaona kwa haraka kuwa kungojea ni sehemu kubwa ya maisha. Tuseme  kwa mfano  upate nyongeza ya mshahara,  kisha uanze kungoja nyingine.
Unangoja kupata mtoto, kisha unaanza kungoja mtoto huyo awache kutumia nepi na aanze kutumia surwali ndefu, na muda si muda unaanza kungoja aanze kujinunulia surwali ndefu zake yeye mwenyewe! Unangoja kununua nyumba, kisha unaanza kungoja kununua vyombo vya nyumba ile ambayo huingojei tena. 

Kisha unangoja kumpata msichana  wa kazi ya nyumbani  kukusaidia  kusafisha  nyumba  na  vyombo  vyako ulivyongojea kupata. Je unaelewa ninachomaanisha? Jifunze kufurahia kungoja, ukifahamu ya kwamba kungoja ndiko kutakakokufikisha  ndoto  yako.  Yafaa  niseme  kuwa  “kungoja vyema”  ndiko  kutakaokufikishia  kwenye  ndoto  yako.  Kutimizwa kwa ndoto hiyo, bila shaka kunatoka kwa Mungu, lakini kungoja ni  kama  kijana  yule  anayetumwa  kufikisha  ujumbe  mahala  fulani. Wakati  mwingine, mtu huanza kungojea jambo fulani kutimika, lakini  wakati  kijana  yule  anyetumwa  kumfikishia  ujumbe anapofika,  tiyari  wameshaondoka  na  kwenda  kuanza  jambo lingine,  na huenda wasiwepo kuona kutimilika  kwa jambo hilo jipya pia. Watu wasio na subira mara nyingi  huwa hawatulii kiasi cha kutosha kuona mwisho wa mambo makuu kweli, maana mambo makuu huchukua muda mrefu kutimia kikamilifu.
Rafiki yangu kila mara husema,  “Cha haraka ni dhaifu, cha pole pole ni kizima kama  kigongo.”   Kama kitu kimefanywa kwa haraka kuwafaa wale wasio na subira na wasio na uwezo wa “kungoja vyema”, huenda hakitadumu. 

Lakini ikiwa watu wako tayari kungojea wakati ulioteuliwa na Mungu, kitu hicho  kitaundwa sawa  sawa na kitadumu na kudumu kwa muda mrefu. Mara kwa mara sisi huona “nyota zinazofyatuka” katika huduma watu  ambao  hutokea  ghafla,  kutoka  mahali  ambapo  hapajulikani na muda si muda wanajulikana ulimwengu mzima, mara nyingi kwa sababu waliweza kuingia katika  kikundi cha watu ambao waliwafungulia  milango. Huduma kama hizi nadra husitawi.

Mara nyingi hizo huwa na matatizo ya kifedha au ya kitabia kwa sababu utu wema hujengwa katika nyakati  zile ngumu za kungojea, lakini wao  hawakupitia wakati huo  wa kujenga tabia na utu wema. Kama  mtu  akiepuka nyakati zile  ngumu  na  kufyatuka mara  moja, kwa kawaida  hatadumu.  Marko  4:5, 6 husema  kwamba mbegu ile inayoota kwa haraka kana kwamba ni kwa usiku mmoja huungua jua  linapozuka.  Mwishowe  tunapofikia  kiwango  cha  kukubali na kuheshimu nyakati  za kungoja, Mungu huanza kufanya  kazi murua  kwa makini  kabisa ndani  yetu. Na  hata ingawa hatuoni ni nini kinachotendeka, mambo yatakayo  tufurahisha baadaye yanaendelea sasa hivi bila ya kuonekana.

No comments:

Post a Comment