Monday, 28 May 2018

ULIMWENGU UMEPOTEZA LADHA YAKE



 
  • Nafikiri ni salama  kusema kwamba  vingi ya  vile  ambavyo ulimwengu hutoa  havina ladha…na  sizungumzi kuhusu  chakula. Kwa  mfano, nyingi ya  sinema zinazotayarishiwa  Hollywood  hazina ladha.  Maongezi mengi na picha  hazina  ladha  nzuri. Mara  nyingi wakati tunapoona  tabia  yoyote  isiyofaa  tunakimbilia “kuulaumu ulimwengu.”  Twaweza kusema  kitu  kama “Ulimwengu  unakwenda wapi?”  Ilhali neno “Ulimwengu linamaanisha  watu wanaoishi ulimwenguni.
Ikiwa  ulimwengu hauna  ladha,  ni kwa  sababu watu wamekosa  ladha katika fikra zao  na matendo. Yesu  alisema kwamba sisi ni chumvi ya  ulimwengu, lakini ikiwa  chumvi imepoteza  ladha yake (nguvu yake na ubora  wake), haifai (angalia  MAT. 5:13). Pia alisema kwamba  sisi ni nuru ya  ulimwengu na hatupaswi kuifunika nuru yetu (angalia MAT. 5:14).

Hebu  fikiria  hivi:  Kila  siku  unapoondoka nyumbani  kwako kwenda gizani,  ulimwengu usio na  ladha,  je,  unaweza  kuwa  nuru na ladha inayohitajika? Unewaza  kuleta furaha  kazini pako kwa kujitolea kuwa  na fikra  za  kiungu. Kupitia mambo madogo kama vile  kuonyesha  shukurani badala  ya  kulalamika kama vile  ambavyo watu  wengi hufanya,  kuwa  mvumilivu,  mwenye huruma,  kusamehe haraka  makosa,  kuwa  mkarimu, na  kuwa  mtu wa  kuwatia  moyo wengine.
Hata kuonyesha tabasamu kiasi na kuwa na urafiki  ni njia ya kuleta ladha nzuri  katika jamii iliyokosa  ladha.  Sijui  kuhusu wewe,  lakini mimi  sipendi  chakula  kisichovuti Rafiki yangu alikuwa  na  tatizo  la  tumbo wakati fulani na  daktari  akamshauri atumie chakula kisicho  na  ladha  nzuri kwa  siku chache.  Kama ninavyo  kumbuka,  wakati huo hakutaka  kula chakula.  Ingawa yeye si mtu anayependa kulalamika,  lakini katika  kila mlo, nilimsikia  akisema kila mara,  “Chakula hiki hakina ladha  kabisa.”  Kilihitaji  chumvi kidogo, viungo kiasi... na hivyo ndivyo ulimwengu unavyohitaji.
Bila  upendo na  ubora  wake wote,  maisha  hayana  ladha  na hayastahili  mtu kuishi. Nataka  wewe uyajaribu. Hebu fikiria: Ninaenda  katika ulimwengu  leo  na kurekebisha mambo.  Kisha jipange akilini mwako  kabla  ya  kutoka  kwenye mlango  wako  kwamba unaenda nje  kama  balozi wa  Mungu  na kwamba  lengo lako ni  kuwa mtoaji,  kuwapenda watu unaokutana  nao siku  nzima. Tabasamu ni ishara ya kukubaliwa na kuidhinishwa  jambo ambalo watu wengi ulimwenguni  wanahitaji.

Jiweke akiba  kwa  Mungu  na umwamini ili  akulinde  unapopanda  mbegu nzuri  kila mahali uendako kwa kufanya maamuzi yatakayokuwa baraka kwa wengine.         Mabadiliko Huanza na Wewe Ninatambua kwamba  huwezi kufanya kila kitu; Sidadisi  jambo hili kabisa.  Ni lazima  ukatae  mambo fulani ama  sivyo  maisha  yako yatajaa  mambo  mengi na  kukufanya  kuwa  mchovu wa  akili kila mara.



Siwezi kujitolea kuwapa  mafunzo watoto  au  kuwapa  mlo wakongwe, lakini ninafanya  mambo  mengine  mengi ili  kuleta tofauti ifaayo ulimwenguni. Nafikiri  swali ambalo  kila mmoja wetu lazima ajibu  ni, “Ni nini  nitakachomfanyia  mtu mwingine  ili  awe na maisha bora?”  Na pengine  swali bora zaidi ni,  Nimefanya nini  leo kumfanya  mtu mwingine aishi maisha  bora?”  Somo hili huenda likawa  gumu kukisoma  wakati mwingine kwa  sababu natumai kitaleta  maswali  yenye utata.  Lakini yanahitaji  kushughulikiwa na  kila  mmoja  wetu.  Hakuna  kizuri kinachotendeka  kiajali.  Ikiwa twataka  kuwa sehemu  ya Mageuzi, inamaanisha kuwa mambo lazima  yabadilike,  na  mambo  hayawezi  kubadilika  hadi  pale  watu watakapoyabadili. Kila  mmoja wetu lazima aseme:  Mabadiliko yanaanza na mimi!.

No comments:

Post a Comment