Wednesday, 30 May 2018

KIUMBE KIPYA ALIYE NA TUMAINI LA SIKU ZA USONI


  •  Biblia inatufundisha kuwa tunapozaliwa mara ya pili kwa kumpokea Kristo kama mwokozi wetu, sisi hufanyika viumbe vipya. 2 Wakorintho 5:17 inatueleza: Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefi ka. Inasisimua kutambua kuwa wakati tunapozaliwa mara ya pili, hali yetu ya kale ya kiroho na kitabia huondolewa na kupita kabisa, na tunapata nafasi ya mwanzo mpya. Mimi hufananisha maisha haya mapya kama udongo wa kiroho.  

Nafasi tuliyo nayo ya kuwa na maisha ya ajabu haina kipimo. Hata hivyo inatupasa kushirikiana na Roho Mtakatifu kutimiza mpango wake katika maisha yetu. Itatubidi kujifunza mengi, lakini la kusisimua ni kuwa maisha yetu ya kale yamezikwa na  Yesu, nasi tumefufuliwa katika maisha mapya pamoja naye. Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende. Waefeso 2:10
Kama viumbe asili vya Mungu, tulikuwa bila hatia yoyote.  Lakini tulidanganywa na kuharibiwa na shetani.  Habari njema ni kwamba tunafanywa upya katika Kristo  Yesu. Mpango wa Mungu kwetu ni kwamba tufanye matendo mema, na tuwe wawakilishi wake duniani.

 Haya ndiyo maisha aliyokuwa ametupangia tangu mwanzo, na alikataa kumkubalia shetani atuangamize. Mungu hutupa moyo na nia mpya ili tufanye matendo mema kwa sababu ya upendo wetu kwake, si kama wajibu fulani.  Anataka tuishi maisha mema, na tayari ametupangia maisha ya aina hii. Tunachohitajika kufanya ni kutembea kwayo kwa imani. Ninakutia moyo uamini kuwa unaweza kuishi maisha mema katika siku za usoni. Maisha yako ya kale yamepita na ukikataa kuyapa nafasi, hayatatawala siku zako za usoni. Pengine hukuwa na mwanzo mzuri maishani, lakini mpendwa unaweza kuwa na mwisho wa ajabu! Tunapompokea Kristo, utu wa Mungu wenyewe hudumu ndani yetu, na tunaanza kufanya mambo kwa njia tofauti kabisa.  Tunajifunza kuwaza na kuzungumza kwa njia tofauti. Malengo, nia, motisha na matendo yetu huanza kubadilika. 

1  Yohana 3:9 inasema hivi: Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu. Maandiko haya hayamaanishi kuwa hatutawahi kutenda dhambi au kukosea tena.  Yanamaanisha kwamba kwa kuwa sasa utu wa Mungu (hali mpya) uko ndani yetu, hatuwezi kuendelea kutenda dhambi kwa makusudi, tukiwa na ufahamu kwamba tunafanya dhambi na bado kuendelea kuifanya, wala kufanya dhambi kwa 

uzoefu. Hatufanyi dhambi tena kwa sababu hatutamani kutenda dhambi tena. Utu wetu umebadilika. Unaweza kusema ni kana kwamba tumefanyiwa upasuaji wa kutupatia moyo mpya. Mungu ameiondoa mioyo iliyokuwa migumu ya mawe, na kutupa mioyo miororo inayoitikia kuguswa na kubadilishwa naye. (Taz Ezek 11:19).

 Tunapofanya dhambi, tunahisi moyo wetu ukituhukumu kuhusu kosa lile, na inatufanya tutamani kubadilika. Inatufanya kutafuta msamaha wa Mungu na kumwomba atuwezeshe kuishi maisha matakatifu. Kama nilivyosema mbeleni, bado tutakosea na kufanya dhambi – na hali hii itakuwa nasi hadi tutakapokufa – lakini pia tutahisi tamaa ya kutaka kubadilika na kupata ushindi katika maeneo ya maisha yetu yenye udhaifu.  Tunapolisoma neno la Mungu kwa uadilifu, tunabadilishwa “kutoka utukufu hadi utukufu” (2  Wakorintho 3:18).

 Mungu hutubadilisha—Roho wake hutufundisha ukweli na kutuongoza tuishi katika ukweli huo (Taz  Yohana 16:13). Siku ya kuokolewa kwetu, Roho Mtakatifu huanza kazi njema ndani yetu, naye huiendeleza hadi siku ya kurudi kwa Kristo (Wafi lipi 1:6).  Tunaanza kufanana na  Yesu katika mwenendo wetu. Tunapompokea Kristo, yeye hutupa mioyo mipya na kuzifanya upya roho zetu. Mienendo yetu hubadilika tunapofanya bidii ya kuweka mabadiliko hayo katika uzoefu maishani mwetu kila siku. 

Hebu tazama  Wafi lipi  2:12-13. Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.  (Union).

Kwa mara nyingine tena, tunaona katika maandiko kwamba Mungu huanza kazi njema ndani yetu, lakini inatubudi tushirikiane na Roho Mtakatifu kuikamilisha. Hatuifanyi kazi hii kwa nguvu zetu wenyewe; tunamtegemea Mungu, tunamwegemea, na tunaamini kuwa anafanya kazi ndani yetu na kutusaidia tupate kutimiza mapenzi yake mema. Iwapo umempokea  Yesu kama Mwokozi wako, ninakutia moyo utambue kuwa sasa wewe ni kiumbe kipya.  Amka kila siku na ujitolee kumwishia. Unapokosea, kiri makosa yako na umwombe Mungu akusamehe.  Yeye ni mwaminifu wa kuendelea kukutakasa kutoka kwa kila dhambi. Katika Wafi lipi 3:12-14 Mtume Paulo alisema kwamba yeye alikuwa akikaza mwendo ili afi kie utimilifu. Hata hivyo, alisema pia kwamba alikuwa hajafi kia hali hiyo ya utimilifu.  Aliyaacha na kuyasahau maisha yake ya kale na kila siku alijitolea kukaza mwendo na kuyafi kia yaliyokuwa mbele. Ninakuhimiza uipokee nia hii mpya na uifanye iwe ndio nia yako maishani.

No comments:

Post a Comment