Nina hakika umesikia mstari maarufu wa maneno yaliyosemwa na John Donne, kwamba “hakuna mwanaume ambaye ni kisiwa.” Maneno haya ni njia ya kueleza ukweli kwamba watu wanahitajiana, yaani kila mmoja anamhitaji mwingine na kumuathiri mwingine kwa njia nzuri au mbaya. Kama vile ambavyo maisha ya ya huyu yaliniathiri mimi kwa njia mbaya na maisha ya Huyu yakaniathiri kwa njia nzuri, maisha yetu yanaweza kuwaathiri watu wengine.
Yesu alituambia tupendane kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya ulimwengu kufahamu kuwepo kwake (angalia Yohana 13:34-35). “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.” Mungu ni upendo, na wakati tunapoonyesha upendo katika maneno yetu na vitendo, tunawaonyesha watu vile Mungu alivyo. Paulo alisema kwamba sisi ni mablozi wa Mungu, waakilishi Wake, na kwamba Yeye Anauhimiza ulimwengu kupitia sisi (angalia 2 KOR 5:20).
Kila wakati ninapofikiria juu ya maandiko haya mimi husema, “Kumbe! Hii ni nafasi kuu na wajibu mkuu.” Kati ya masomo niliyojifunza maishani ni kwamba singepata nafasi bila ya kuwajibika. Hiyo ndiyo moja ya matatizo katika jamii yetu hivi leo. Watu wanataka kile ambacho hawanuii kuwa nacho! Uchoyo unasema, “Nipe mimi. Ninataka na ninataka sasa.”Hekima yasema, “Usinipe mimi kitu chochote; sijakomaa vya kutosha kukisimamia.”
Ulimwengu kwa kiwango kikubwa hauna shukurani na, hivyo ni kwa sababu hatutaki tena kusubiri au kujitolea kwa chochote. Nimegundua kwamba mambo niliyo na shukurani nayo ni yale ambayo nimeyafanyia bidii na kusubiri kwa muda mrefu. Mambo tunayopata kwa urahisi kwa kawaida huwa hayana thamani kubwa kwetu....
No comments:
Post a Comment