Shangazi yangu aliniambia kuwa baada ya mjomba wangu kufa, wakati mwingine alilia usiku huku akipiga mto wake na kusema, “Kwa nini uliniacha?” Alijua katika nia yake kwamba hakumwacha kimakusudi, lakini hiyo ilikuwa ni sauti ya hisia zake.
Tunahitaji kujua kuwa hisia zetu zina sauti, na wakati zinapokuwa zimeumia, basi zinaweza kuitikia hali tunayoipitia kama mnyama aliyeumia. Wanyama walioumia wanaweza kuwa hatari, na hisia zilizoumia zinazweza kuwa hivyo pia tukizifuata na kuzitii. Wakati mtu ana msiba, ni muhimu asiache hisia zilizoumia zimfanye kuwa mwenye chuki na uchungu moyoni.
Wakati pigo linakuwa ni talaka, ni rahisi kumchukia yule aliyesababisha utengano au hata kujaribu kulipiza kisasi. Usiharibu maisha yako kwa kuendelea kuwa na uchungu moyoni. Badala yake, mwamini Mungu kuwa anaweza kuchukua yale ambayo yametukia na kukufanya uwe mtu bora zaidi. Jambo hilo hilo linalokuumiza linawafinya wengi pia. Mwombe Mungu achukue “majivu” yako na akupe “uzuri” badala yake.
Mwombe akuwezeshe kuwasaidia wengine wanaopitia maombolezo na upweke kama wewe. Hata wakati mpendwa anapokufa unaweza kuwa na wakati ambapo una hasira kwake kwa sababu amekuacha peke yako.
Unaweza kuwa unasema katika mawazo yako, “Kama ungejaribu sana, hungelikufa,” au, “Unawezaje kuniacha niwalee watoto pekee na nibebe majukumu haya peke yangu,Kwanini Umeniacha katika Hali hii?” Hata ingawa mawazo kama haya yanaweza kuonekana kama mzaha kwa mtu ambaye haupitii msiba nyakati za kawaida, msiba unapoingia ghafula na huzuni kutuzingira, kuna uwezekano wa “kuwalaumu” wengine kwa sababu ya uchungu tunaouhisi. Mawazo na hisia zinaweza kubadilika -badilika.
Wakati mmoja unaweza kuwa na hasira dhidi ya Mungu, wakati mwingine hasira juu yako mwenyewe, na wakati mwingine juu ya shetani na juu ya mtu aliyesababisha pigo au msiba huo. Mwenendo huu unaweza kurudiwa tena na tena hata uanze kumchanganyisha mwenye msiba. Wakati tunapoumia moyoni, njia ya kawaida ya kibinadamu ni kukasirika na kujaribu kujiondoa mbali na uchungu tunaoupitia. Hii ndio maana ni muhimu kuelewa kipindi cha kuomboleza na kufahamu kuwa kuna hisia ambazo huambatana na kipindi hiki. Katika nyakati zilizopita wengi wetu tulifundishwa kutothamini hisia zetu - kuzichukua kama jambo lisilo la maana. Baada yako kupatwa na pigo au msiba katika maisha yako, huo si wakati wa kukataa hisia zako au kujiingiza katika mambo mengine ambayo yatakutia dhiki au uchungu zaidi. Badala yake, unafaa kukabiliana na hisia zako na uzitulize.
Hakuna suluhisho katika kujaribu kuzizuia hisia zako, bali jambo la busara ni kuzitambua na kuzikabili kama ipasavyo.
GetYourHopesUp .
Jimmy J.
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment