- "Nilidhulumiwa kingono na baba yangu mzazi kwa miaka mingi. Nilijaribu mara mbili tofauti kumwambia mtu fulani kilichokuwa kikitendeka kwangu na kwa vile hawakunisaidia, niliendelea kuteseka peke yangu hadi nikawa mtu mzima na hatimaye nikaanza kuzungumza hadithi yangu na watu wengine na nikapokea. uponyaji kutoka kwa Mungu."
Chanzo cha jambo ndio mwanzo wake, na msaada wake. Mizizi kawaida huwa chini ardhini. Na kwa sababu hiyo mara nyingi twapuuza na kuzingatia tu kile tunachokiona juu ardhini. Mtu anayeumwa na jino mara nyingi anahitaji kujua chanzo cha jino linavyouma. Mzizi wa jino hilo umeoza na lazima uchunguzwe bila hivyo jino lote halitakoma kuwa na uchungu. Mzizi wa jino hauwezi kuonekana, lakini unajua uko hapo kwa sababu uchungu ni mwingi.
Ulimwengu una uchungu, na uchungu huo hautakoma hadi pale tutakapojua chanzo cha matatizo yanayowakumba watu binafsi na jamii. Ninaamini kwamba chanzo ni uchoyo. Nimejaribu kufikiria juu ya tatizo ambalo halianzii na uchoyo, na sijapata hata moja.
Watu hawajali juu ya kuharibu maisha ya wengine ili kupata kile wanachohitaji au kile wanachoonelea ni bora kwao. Nimejaribu kufikiria juu ya tatizo ambalo halianzii na uchoyo, na sijapata hata moja. Kwa neno kamili, uchoyo ndio chanzo cha matatizo yote ulimwenguni.
Uchoyo Una Maelfu ya Sura
Uchoyo una Maelfu ya Sura, na pengine hiyo ndiyo sababu hatuutambui ni nini. Tunauona kwa watoto ambao hulia wakati wasipopata kile watakacho na kwa watoto ambao huchukua vikaragosi vya kuchezea vya watoto wengine.
Hii ni dhahiri katika mawazo yetu kuonekana tuko hali bora kuliko wengine au kufanya vyema kuliko wanavyofanya. Uchoyo ni kuhusu kuwa wa kwanza katika kila jambo, na ingawa hakuna makosa ya kutaka kufanya vyema zaidi, ni makosa kufurahia kuwaona wengine wakikosa kufaulu ili sisi tufaulu.
Ninaamini kwamba uchoyo wa aina yote ni mbaya na kwamba unasababisha matatizo. Katika sehemu hii, nataka niyalete mawazo yako kwa aina tatu maalum za uchoyo ambao kwa kawaida unapatikana katika ulimwengu wa leo na matokeo mabaya yanayotokana na uchoyo huo.
Dhuluma za kingono:
Ann ana umri wa miaka kumi na mitatu. Baba yake humwambia yeye ni mwanamke sasa na kwamba wakati umefika kwake kufanya yale ambayo wanawake hufanya. Anapomaliza kumuonyesha kile anachomaanisha kuwa yeye ni mwanamke, yeye huona haya, huwa na hofu na kujiona mchafu. Ingawa baba yake humhakikishia kwamba kile anachofanya ni jambo zuri, yeye hushangaa ni kwa nini humtaka aliweke jambo hilo kuwa siri na ni kwa nini linamfanya ahisi vibaya. Huku miaka ikiyoyoma na baba yake akiendelea kumdhulumu na kumbaka, Ann hufunga hisia zake kwa hiyo hahitaji kuhisi uchungu tena. Baba yake Ann ameuiba utoto wake, ubikira wake, uhalali wake, na bila ya mwingilio kutoka kwa Mungu, ataiba maisha yake ili kupata kile alichokitaka. Twachukizwa mno na visa vya kina-baba kuwabaka watoto wao na visa vya watu wa familia kujamiiana tunavyosikia, lakini ukweli ni kwamba asilimia 90-95 ya visa hivyo haviripotiwi.
Nilidhulumiwa kingono na baba yangu mzazi kwa miaka mingi. Nilijaribu mara mbili tofauti kumwambia mtu fulani kilichokuwa kikitendeka kwangu na kwa vile hawakunisaidia, niliendelea kuteseka peke yangu hadi nikawa mtu mzima na hatimaye nikaanza kuzungumza hadithi yangu na watu wengine na nikapokea. uponyaji kutoka kwa Mungu.
"Baba yangu alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na sita bila ya kuadhibiwa kwa uhalifu alionitendea. Watu aliofanyakazi nao na aliohudhuria nao karamu na dhifa mbali mbali hawakujua alikuwa akimbaka bintiye tangu alipokuwa msichana mdogo."Jesca..
Twaona yale watu wanayofanya na kuwa haraka kuwahukumu, lakini tunajua chanzo cha tabia zao? Wanawake wengi tunaowahukumu kuwa “matatizo katika jamii” ni wahasiriwa wa kubakwa na baba zao au watu wa familia zao.
Kwa mfano,
•Asilimia 66 ya makahaba wote ni wahasiriwa wa dhuluma za kingono walipokuwa watoto.
•Asilimia 36.7 ya wanawake walio gerezani nchini Tanzania walidhulumiwa walipokuwa watoto.
•Thuluthi moja ya watoto walio dhulumiwa na kutelekezwa baadaye huwadhulumu na kuwatelekeza watoto wao wenyewe.
•Asilimia 94 ya wahasiriwa wa dhuluma za kingono huwa chini ya umri wa miaka kumi na miwili wanapodhulumiwa. Uchungu unaosababishwa na visa vya kina baba kuwabaka watoto wao na watu wa familia kujamiiana na dhuluma za kingono ulimwenguni ni mkubwa mno na yote yalianza kwa sababu watu ni wachoyo na hawakujali ni nani atakayeumia ilimradi wamepata kile wakitakacho.
Ndio, pengine hutaua, hutaiba, hutadanganya, wala kutenda vitendo vya dhuluma dhidi ya watoto, lakini kuna uwezekano kwamba u mchoyo katika njia fulani. Ikiwa tutakuwa na msamaha wa uchoyo wetu kwa kuwaelekezea kidole cha lawama wale ambao uhalifu wao ni mbaya kuliko wetu, hatutafaulu kukabiliana na matatizo haya katika jamii hivi leo. Kila mmoja wetu lazima achukue jukumu la kukabiliana na tabia yetu ya uchoyo, haijalishi ni wa kiwango gani au kwa njia ipi tunayoueleza. Ulafi: Uchoyo mara nyingi huchukua njia ya ulafi. Ulafi ni roho ambayo hairidhiki na kila mara inataka zaidi. Jamii yetu hivi
leo imezoea kutumia mambo yaliyoko. Nilishangaa nilipokuwa nikiendesha gari na kuona majumba ya ukahaba yaliyoko na yale yanayojengwa. Uchafu, uchafu, na uchafu mbaya zaidi na yote si mambo ya kweli. Yanaahidi maisha rahisi na furaha zaidi, lakini kwa watu wengi yote yanayobuniwa ni deni la unyanyasaji. Shinikizo na majaribu ya kununua zaidi na zaidi ili kutufanya tuingie katika uchoyo.
Lakini habari njema ni kwamba twaweza kubadilika ikiwa kweli twataka kufanya hivyo. Hebu tujifunze kununua kile tunachohitaji na baadhi ya yale tunayotaka na kisha tujifunze kutoa sehemu ya mali yetu, hasa yale ambayo hatuyatumii tena kwa mtu ambaye anahitaji. Hebu tujizoeshe kutoa hadi pale litakapokuwa jambo la kwanza na la kawaida tufanyalo kila siku za maisha yetu. Kwa watu wengi hii kweli itakuwa njia ya kugeuza maisha yao. Biblia inasema kwamba kupenda fedha ndicho chanzo cha maovu (angalia 1 TIM 6:10). Sababu ya pekee ya watu kupenda pesa na watafanya chochote kupata ni kwamba wanafikiri pesa zitawafanya wapate kila watakacho.
Wanaamini zinaweza kununua furaha. Watu kila mara huua, kuiba na kudanganya ili wapate pesa na haya yote chanzo chake ni ugonjwa huu wa uchoyo. Hivi majuzi nilisoma taarifa fulani ya mcheza sinema mmoja mashuhuri aliyesema watu wanaamini kwamba ikiwa wana vitu vyote wanavyohitaji basi watakuwa na furaha, lakini ni ahadi ya uongo. Aliendelea kusema kwamba alikuwa na kila kitu mwanaume alichopaswa kuwa nacho na aligundua kuwa bado hakupata furaha kwa sababu wakati mtu anapotimiza lengo lake la kumiliki kila kitu kipatikanacho duniani bado amesalia yeye mwenyewe.
Ndoa Kuvunjika:
Uchoyo pia ni chanzo cha Ndoa kuvunjika. Watu mara nyingi huoana wakiwa na mawazo tofauti ya vile ndoa inavyopaswa kuwa. Wengi wetu huamua kwamba mume au mke wetu ni mtu anayepaswa kutufanya kuwa na furaha, na wakati jambo hili lisipotendeka, vita huanza. Ni toafuti ipi ambayo ingelitokea iwapo tungeoa au kuolewa na kuweka akili zetu kufanya tutakalofanya ili kuwawafanya waume au wake zetu kuwa na furaha! Kwa sasa hivi huenda unafikiria, sitafanya hivyo kwa sababu najua mtu atachukua fursa ya mambo yalivyo. Katika miaka yangu ya mwanzo ningelikubali. Lakini baada ya maisha marefu ninaamini Biblia ni ya ukweli. Inafundisha kuwa upendo haushindwi (angalia 1 KOR 13:8). Pia inasema kwamba kile mtu apandacho ndicho atakachovuna (GAL 6:7). Ikiwa ninaamini Biblia na ndivyo ninavyoamini, basi ninaamini kwamba ninasimamia mavuno ninayopokea katika maisha yangu, kwa sababu yanategemea mbegu ninazopanda. Ikiwa tunapanda huruma tutavuna huruma, ikiwa tunapanda ukarimu tutavuna ukarimu.
Yesu alikuja ili kufungua milango ya gereza na kuwafanya walio kifungoni kuwa huru (angalia ISA 61:1). Ameniweka huru kutokana na mambo mengi, lililo kuu zaidi ni mimi mwenyewe. Nimewekwa huru kutokana na mimi! Ninaendelea kukua kila siku katika uhuru huu, lakini nina shukuru kutambua kwamba furaha halisi haipatikani kwa mambo yangu kwenda vizuri kila wakati. Pengine kama vile mimi, wewe pia ulikuwa na mifano mibaya maishani na unahitaji kuondoa mambo ambayo ulikuwa umejifunza katika miaka yako ya mwanzo. Kuwa mwaminifu. Je, utafanya nini usipopata kile ukitakacho? Utakasirika? Utanung’unika na kulalamika? Unaweza kumwamini Mungu akulinde au unaishi katika hofu ambayo ikiwa hutajilinda mwenyewe, hakuna atakayekulinda? Kuamini kuwa ni lazima ujilinde wewe mwenye kusababisha uchoyo, unaosababisha maisha yasiyokuwa na furaha.
Ninakuhimiza ujiepushe na uchoyo hivi leo na uanze kuthamini, kulinda na kuwapenda kwa ukweli watu wengine. Uchoyo ni Chaguo Wengi wetu hutumia muda mwingi kufikiria, kuongea na kufanya mipango yetu wenyewe. Ingawa ninafunza kwamba twapaswa kujipenda sisi wenyewe katika njia ya uwiano, siamini kuwa tunapaswa kujipenda sana hivi kwamba tuwe katika ulimwengu wetu na kujali tu kile tunachotaka tupate. Kwa njia zote lazima tujitunze kwa sababu sisi ni wa thamani kuu kwa mpango wa Mungu hapa duniani. Alitupa uhai kwa hivyo lazima tuufurahie (angalia Yohana 10:10). Kwa hivyo tunahitaji kuutafuta, lakini lazima tusikose kutambua kwamba njia ya kweli ya kupata furaha ni kuyatoa maisha yetu kuliko kujaribu kujiwekea maisha hayo sisi wenyewe. Yesu anasema kwamba ikiwa tunataka kuwa Wanafunzi wake, lazima tujisahau, tukose kujionea sisi wenyewe na maslahi yetu yote na tumfuate Yeye (angalia Marko 8:34).
Sasa nakubali kuwa hili ni wazo la kutisha, lakini nina nafasi maana nimeishi kwa muda mrefu wa kuweza kulijaribu na nimegundua kuwa linafanya kazi. Yesu kadhalika anasema kwamba ikiwa tutayatoa maisha ya chini” (maisha ya uchoyo) tutapata maisha ya “juu” (maisha yasiyo ya uchoyo), lakini tukiyaweka maisha ya chini tutapoteza maisha ya juu (angalia Marko 8:35).
Anatupatia chaguo kuhusu jinsi tutakavyoishi. Anatuambia kile kitakachotufaa na kisha kutuacha tuamue iwapo tutafanya au lah. Ninaweza kuendelea kuwa mchoyo na pia wewe waweza kufanya hivyo, lakini habari njema ni kwamba si lazima tufanye hivyo. Tuna nguvu ya Mungu ya kutusaidia kuyapita mambo yetu na kuishi maisha ya kuwafanya watu wengine waishi maisha bora. Safari Uchoyo si tabia ya kujifunza, tunazaliwa nayo. Ni sehemu ya maumbile yetu. Biblia inautaja uchoyo kuwa “maumbile ya dhambi.”
Adamu na Hawa walifanya dhambi kwa Mungu kwa kufanya kile alichowaamuru wasifanye na dhambi kuu waliyoifanya ilipitishwa kwa kila mtu ambaye alizaliwa.
Mungu alimtuma Mwanawe Yesu afe kwa ajili ya dhambi, na kutukomboa kutokana na dhambi hiyo. Alikuja kutangua kile ambacho Adamu alikifanya. Tunapomkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yetu, Yeye huingia na kukaa pamoja nasi katika roho zetu na ikiwa tutaruhusu sehemu hii iliyofanywa upya katika nafsi zetu ili kuyatawala mawazo yetu, twaweza kuishinda dhambi ambayo imo milini mwetu. Dhambi huwa haiendi mbali, lakini Yule mkuu anayeishi ndani yetu hutusaidia kuishinda kila siku (angalia Wagalatia 5:16).
Mungu alimtuma Mwanawe Yesu afe kwa ajili ya dhambi, na kutukomboa kutokana na dhambi hiyo. Alikuja kutangua kile ambacho Adamu alikifanya. Tunapomkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yetu, Yeye huingia na kukaa pamoja nasi katika roho zetu na ikiwa tutaruhusu sehemu hii iliyofanywa upya katika nafsi zetu ili kuyatawala mawazo yetu, twaweza kuishinda dhambi ambayo imo milini mwetu. Dhambi huwa haiendi mbali, lakini Yule mkuu anayeishi ndani yetu hutusaidia kuishinda kila siku (angalia Wagalatia 5:16).
Hii haimaanishi kwamba hatufanyi dhambi, lakini tunaweza kuimarika na kupata ufanisi katika maisha yetu. Siwezi kusema kabisa kabisa kwamba nimeushinda uchoyo, na sidhani kama kuna mtu yeyote ambaye ameushinda kabisa uchoyo. Kusema hivi ni kama kusema kwamba hatufanyi dhambi, kwa sababu dhambi yote inaanzia na aina fulani ya uchoyo. Sijashinda uchoyo kabisa kabisa, lakini nina matumaini ya kuimarika kila siku. Niko safarini na ingawa huenda sitawasili, nimejitolea kwamba wakati Yesu atakapokuja kunichukua kurudi nyumbani, atanipata ninaendelea kusukuma lengo hili (angalia Wafilipi 3:12-13).
Mtume Paulo alisema maneno yafuatayo: “Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu (Wagalatia 2:20).
Paulo alimaanisha kwamba haishi tena kwa ajili yake mwenyewe na mapenzi yake, bali kwa Mungu na mapenzi ya Mungu. Nilitiwa moyo sana siku moja wakati nilipogundua kupitia mafunzo ambayo Paulo alisema maneno haya miaka ishirini baada ya kuokoka kwake. Kujifunza kuishi bila uchoyo ndiyo iliyokuwa safari yake, kama ilivyo kwa kila mmoja wetu. Paulo pia alisema “Nina kufa kila siku (ninakabiliwa na kifo kila siku na kufa ndani yangu).” (1 Wakorintho 15:31). Kwa maneno mengine kuwatanguliza wengine kwanza vilikuwa vita vya kila siku na kulihitaji uamuzi wa kila siku. Kila mmoja wetu lazima aamue jinsi tutakavyoishi na kitakachotufanya tuishi kwacho, na hakuna wakati bora wa kufanya hivyo kuliko sasa.
Wewe na mimi tuna wakati mmoja wa kuishi na uhai mmoja wa kutoa, kwa hivyo swali ni: “Je, tutaishi vipi?” Ninaamini kabisa kwamba ikiwa kila mmoja wetu atafanya sehemu yake kuyatanguliza maslahi ya watu wengine kwanza basi twaweza kuona na kuwa sehemu ya mageuzi yenye uwezo wa kubadili ulimwengu.
No comments:
Post a Comment