Monday, 23 July 2018

Ushuhuda wa Annah

"baba  yangu  alinidhulumu  mimi  kingono  kwa  miaka mingi na  matendo yake ya  uovu yaliharibu roho  yangu  na  kuniacha nimejeruhiwa  na  siwezi kufanya  kazi  kama  kawaida  hadi Yesu aliponiponya. Kusahau yale aliyonifanyia na kuweza kumsamehe kabisa lilikuwa jambo  gumu  kabisa.  Kwanza,  nilifanya  uamuzi nisimchukie  tena  kwa  sababu Mungu alinifanya  nifahamu kwamba kumpenda  Yeye na kumchukia  baba  yangu  mzazi  hakungekaa katika moyo mmoja."

"Nilimpokea Yesu kama Mwokozi  wangu  nikiwa  na umri  wa miaka tisa, lakini  sikuelewa nilichokuwa nacho  ndani Yake  au jinsi ya  kuwa  na uhusiano Naye kungebadili  maisha  yangu  kwa  sababu sikuwa na “elimu  ya kuendelea”  katika maswala  ya  kiroho. Nyumba niliyolelewa haikuwa ikifanya kazi. Baba yangu alikuwa mlevi, asiye mwaminifu  kwa  mama  yangu   huku akiwa  na wanawake wengi, na alikuwa mtu  mkali  mwenye  fujo  na hasira. Kama nilivyotaja  hapo awali, pia alinidhulumu  kingono kila mara.Annah
"Orodha hii  inaendelea, lakini  nina hakika umeipata picha hiyo. Annah anaendelea kusema "  Nilimpenda  Mungu na  nilitaka  kujifunza,  kwa  hivyo nikajiunga na masomo ambayo hatimaye yaliniruhusu kuthibitishwa katika dhehebu na kwenda kanisani kila mara.  


Nilijifunza  kuhusu upendo  wa  Mungu na neema, na vile  vile  nikajifunza imani mbali mbali za kikanisa ambazo ni muhimu kwa msingi wa imani. Nilipofika umri wa  miaka  thelathini na  miwili, Nilijipata nimetatizika  sana  kwa  sababu Ukristo wangu  haukuonekana kunisaidia katika  matendo  yangu  ya  kila  siku maishani.
Niliamini ningekwenda mbinguni  wakati nitakapokufa,  lakini nilikuwa na haja  sana  na  msaada  ili niweze  kuendelea  kila  siku duniani kwa amani na furaha.   Roho  yangu   ilijazwa  na uchungu kutokana  na kudhulumiwa  nilipokuwa mtoto  na niliuongeza  uchungu huo kila siku katika  fikra  zangu  na kutokuwa  na uwezo wa  kudumisha uhusiano mwema."

Neno la  Mungu latuambia  kwamba  ikiwa  tutamtafuta  Mungu kwa bidii tutampata (angalia MIT 8:17). " Nilianza kumtafuta Mungu mimi mwenyewe kwa  chochote  nilichokosa,  na  nilikutana  naye na hiyo  ikanifanya  niwe karibu Naye.  Mara  moja  alionekana  kuwepo sana  katika  maisha  yangu  ya  kila siku na  nikaanza   kuchunguza kwa  bidii  ili Nimjue  vyema  zaidi.  Ilionekana  kuwa  kila mahali nilikogeuka, nilisikia kuhusu imani. Nilijifunza  kwamba  ningetumia  imani  katika hali nyingi, ambazo zingefungua mlango kwa Mungu kuhusika na kunisaidia. Niliamini   na moyo wangu  wote  kwamba  mambo niliyojifunza yalikuwa  sawa,  lakini bado nilipata  matatizo  makuu kwa  sababu  Nilikuwa nimepata  ufanisi  mkubwa,  lakini  bado nilihisi  katika moyo wangu kwamba  kuna kitu  kilichokosekana,  kwa hiyo kwa mara nyingine tena nikaanza kumtafuta  Mungu  kwa  bidii  zaidi. Kupitia kumtafuta kwangu  na  kuchunguza  kwa  undani zaidi nilijifunza  kwamba nimekosa  funzo kuu  ambalo  Yesu alikuja kutufunza: kumpenda Mungu,  kujipenda  sisi  wenyewe, na kuwapenda wengine  (angalia MAT 22:36-39).  Nilijifunza  mengi kuhusu  imani nilivyokuwa nikitembea  na Mungu, lakini  sikuwa nimejifunza  kuhusu  nguvu ya upendo....."

Biblia inasema kwamba  Mungu  alitununua  kwa gharama  kubwadamu ya  Mwanawe,  Yesu  Kristo  (angalia  1  KOR 6:20,  1  PET  1:19, UFU  5:9).
Kitendo  hiki  cha  kushangaza  cha  uzuri kiliondoa uovu wa  shetani aliofanya  na kufungua njia kwa  watu wote kusamehewa dhambi zao  na  kufurahia  uhusiano wa  kibinafsi na  Mungu. Kama nilivyoeleza, baba  yangu  alinidhulumu  mimi  kingono  kwa  miaka mingi na  matendo yake ya  uovu yaliharibu roho  yangu  na  kuniacha nimejeruhiwa  na  siwezi kufanya  kazi  kama  kawaida  hadi Yesu aliponiponya. Kusahau yale aliyonifanyia na kuweza kumsamehe kabisa lilikuwa jambo  gumu  kabisa.  Kwanza,  nilifanya  uamuzi nisimchukie  tena  kwa  sababu Mungu alinifanya  nifahamu kwamba kumpenda  Yeye na kumchukia  baba  yangu  mzazi  hakungekaa katika moyo mmoja.* Nilimuuliza  Mungu  anisaidie  na akaniondolea chuki kutoka  moyoni mwangu.  Hata  hivyo, bado  sikutaka  kufanya mambo mengi na baba yangu na nilikaa mbali sana naye.
Afya  ya  akili ya  mama  yangu  iliendelea  kuzorota  kwa  miaka kadhaa   alikuwa  na  ugonjwa wa  akili  kutokana  na  kujua  kile ambacho  baba  yangu  alinifanyia na bila  kujua  jinsi ya  kukabiliana  nacho.  *Alimfumania akinidhulumu wakati nilipokuwa  na  umri wa  miaka  14,  lakini kama  nilivyosema, hakujua kile  anachoweza  kufanya,  kwa  hiyo hakufanya  kitu.

Kutofanya kitu kuligeuka  kuwa uamuzi mbaya  kwetu sote. Kwa miaka miwili,  alitibiwa matatizo ya mshutuko wa akili  na matibabu hayo yaliondoa mawazo  ya kukumbuka matendo ya kudhulumiwa kingono niliyofanyiwa  na sikutaka  kufanya  kitu ambacho kingelisababisha akumbuke  tena, kwa hiyo ingawa ilikuwa  vigumu kwangu kuwa karibu  na baba yangu, familia  yangu ilinitembelea wakati wa  likizo  na wakati mwingine  ambao  tungepaswa  kufanya hivyo tu. Hatimaye wazazi  wangu  waliondoka  mjini  na  kurejea katika mji mdogo  ambako  waliendelea kuishi. Ulikuwa karibu umbali wa maili mia mbili  kutoka  mahali  nilikokuwa  nikiishi  na nilifurahi kwa sababu kuondoka  kwao  kulimaanisha  singewaona  sana. Nilifaulu kumsamehe baba  yangu  kwa  kiasi fulani katika  miaka  hiyo,  lakini sikuwa nimemsamehe kabisa.

Nilisoma kila maandiko niliyopata  kuhusu  kuwapenda adui zako, kuwa  mkarimu kwa  wengine na  kuwafanyia  hisani.  Hii ilinigusa kweli:
Bali wapendeni adui zenu, tendeni  mema, na  kukopesha msitumaini kupata  malipo,  na  thawabu yenu  itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa  wana  wa  Aliye juu, kwa  kuwa  Yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. (LK 6:35).
Kifungu  hiki chasema  tusifikirie  kuwa  tumepoteza  kitu na kukata tamaa kuhusu chochote. Kabla nielewe jambo hili, niliangalia utoto wangu kama miaka iliyopotea,  sasa  Mungu  alikuwa akiniuliza niione kama  ujuzi nilioupata  ninaoweza  kuutumia kwa wengine.

Luka  pia  alisema  twapasa  kuuliza baraka  kwa  wengine na kuwaombea  wale wanaotudhulumu  na kututumia  vibaya  (angalia LK 6:28). Hii  inaonekana si haki, lakini  tangu  hapo  nimejifunza kwamba  ninaposamehe  ninajifanyia hisani mimi  mwenyewe. Wakati ninapo-  samehe, najiweka huru kutokana  na matokeo yote ya uongo niliyofanyiwa na kisha Mungu  anaweza kukabiliana na hali  yote  hiyo.  Ikiwa  adui yangu  hajaokoka,  huenda nikanunua roho.

Baba  yangu  alishangazwa  mno na ukarimu tuliomfanyia mimi na mume wangu. Miaka  mitatu baada  ya  kufanya kile Mungu alichotuuliza  tufanye,  baba  yangu  alitubu kwa  machozi na akamkubali Yesu kuwa  Mwokozi wa  maisha  yake. Lilikuwa ni jambo  la  kushangaza.  Alilianza  jambo  hili yeye mwenyewe. Alituomba  tuje nyumbani kwake, na  akaomba  msamaha..
Mwandishi
Jimmy J.

No comments:

Post a Comment