Huenda unasoma sura hii na unafahamu kwa uchungu ni mara ngapi umekosea wakati ulipokuwa unachukua hatua hapo zamani. Huenda kulikuwa na wakati ulipata nafasi ya kuchukua hatua huku ukiwa na malengo makubwa, na ari ya kuchukua hatua kwa ujasiri na kutimiza jambo fulani, lakini mambo yakaenda mrama. Ikiwa hivyo ndivyo unavyohisi, ninaweza kuelewa kule unakotoka. Mara nyingi nimejaribu kufanya kadri nilivyoweza, lakini badala ya kuyafanya mambo kuwa mazuri zaidi, nilihisi kana kwamba niliyaharibu mambo kabisa.
Nadhani sote tumewahi kupitia siku kama hizo. Lakini hatupaswi kuruhusu kushindwa kwetu wakati wa nyuma kutuzuie kujaribu tena siku zijazo. Mungu anajua kwamba tunayo mapungufu na udhaifu. Kushindwa kwetu hakumshangazi, na hakumzuii kufanya kazi katika maisha yetu. Kusema kweli, mara kwa mara Mungu hutumia mapungufu yetu kudhihirisha nguvu zake. Niliwahi kusoma hadithi moja inayoonyesha vizuri vile ninavyosema:
- Mchukuzi wa maji huko India alikuwa amebeba mitungi miwili mikubwa na ilikuwa inaning’inia mwishoni wa ufito alioubeba shingoni mwake. Mmoja wa mitungi hiyo ulikuwa hauna kasoro na haudondoshi maji yoyote mwishoni mwa safari ndefu kutoka mtoni hadi nyumbani kwa bosi wake. Ule mtungi mwingine ulikuwa una ufa, na kufikia wakati wa kufika kule ulikokuwa unapelekwa, ulikuwa umejaa nusu tu. Hali ilikuwa hivyo kila siku kwa kipindi cha miaka miwili. Yule mchukuzi wa maji alifikisha kwa bosi wake mtungi mmoja uliojaa maji na mwingine uliojaa nusu. Bila shaka, ule mtungi mzuri ulijivunia mafanikio yake—ulikuwa mkamilifu hadi mwisho wake ambao ulifinyangwa kwa huo. Maskini ule mtungi uliokuwa na ufa uliona aibu kwa sababu ya mapungufu yake na mateso kwamba uliweza kutimiza nusu tu ya kazi uliyofinyangiwa. Baada ya miaka miwili ya ule mtungi usiokuwa mkamilifu kuona unashindwa vibaya, ulimwambia yule mchukuzi wa maji na kusema, “Ninaona aibu na ningependa kukuomba msamaha.” Yule mchukuzi akauliza, “Kwa nini? Unaona aibu kwa nini?” Mtungi ukasema, “Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, nimeweza kubeba maji nusu kila siku kwa sababu huu ufa ulio ubavuni mwangu unadondosha maji wakati wote, maji yanavuja hadi nifike nyumbani kwa bosi wangu. Kwa sababu, ya kasoro zangu, huna budi kufanya kazi hii yote bila kupata faida inayoendana na bidii zako.” Yule mchukuzi wa maji aliusikitikia ule mtungi wenye ufa, na katika huruma zake akasema, “Tunapokwenda nyumbani kwa bosi wetu, nataka utazame uone maua mazuri kandoni mwa njia.” Na kweli, walipokwea mlima, ule mtungi wenye ufa uliyaona yale maua mazuri ya mwituni kando ya njia. Lakini walipofika mwisho wa safari, bado ule mtungi uliumia maana nusu ya maji yalikuwa yamevuja tena. Kisha yule mchukuzi wa maji akauambia ule mtungi, “Je, umegundua kwamba kulikuwa na maua upande wako wa njia tu na si upande mwingine wa mtungi? Ni kwa sababu nilijua kasoro yako na nikatumia fursa hiyo kupanda maua upande wako wa njia. Kila tulipokuwa tukitembea kutoka mtoni, ulimwagia maji ile mbegu, na kwa muda wa miaka miwili nimekuwa nikichuma maua haya mazuri na kuipamba meza ya bosi wetu.
Bila wewe kuwa jinsi ulivyo, bosi hangekuwa amepata maua haya yote ya kupambia nyumba yake.”1 Wewe pia, kama ule mtungi, unaweza kukamilisha mambo mazuri sana. Haijalishi kuwa wewe una kasoro na mapungufu. Usiache kile unachokiona kuwa udhaifu kikuzuie kupiga hatua za ujasiri zinazochochewa na matumaini. 2 Wakorintho 12:10 inasema: “... Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” Je, hilo halifariji sasa? Hata wakati unapokuwa dhaifu, ndipo ulipo na nguvu kwa sababu Mungu yuko pamoja nawe. Anatumia kila sehemu ya maisha yako—hata nyufa—ili kuumba kitu cha kupendeza.
No comments:
Post a Comment