Wednesday, 11 July 2018

Uchoyo ni Chaguo

Wengi wetu hutumia muda  mwingi kufikiria, kuongea  na  kufanya mipango yetu wenyewe. Ingawa  ninafunza kwamba  twapaswa kujipenda  sisi  wenyewe katika njia ya uwiano, siamini  kuwa tunapaswa  kujipenda sana  hivi kwamba  tuwe katika  ulimwengu wetu na  kujali tu kile  tunachotaka  tupate. Kwa  njia zote  lazima tujitunze   kwa  sababu sisi  ni  wa  thamani kuu  kwa  mpango wa Mungu hapa  duniani.

Alitupa uhai kwa  hivyo  lazima  tuufurahie (angalia  Yohana  10:10). Kwa  hivyo tunahitaji  kuutafuta,  lakini lazima  tusikose kutambua  kwamba  njia ya  kweli ya  kupata  furaha ni kuyatoa  maisha  yetu kuliko  kujaribu kujiwekea  maisha  hayo  sisi wenyewe. Yesu anasema  kwamba ikiwa  tunataka  kuwa  Wanafunzi wake,  lazima  tujisahau,  tukose kujionea sisi wenyewe na  maslahi yetu yote  na  tumfuate Yeye (angalia  Marko  8:34).  Sasa  nakubali kuwa hili  ni  wazo  la kutisha, lakini  nina  nafasi maana  nimeishi  kwa muda mrefu  wa  kuweza  kulijaribu na  nimegundua  kuwa  linafanya kazi. 


Yesu kadhalika  anasema  kwamba  ikiwa  tutayatoa  maisha  ya “chini”  (maisha  ya  uchoyo) tutapata  maisha  ya  “juu”  (maisha  yasiyo ya  uchoyo), lakini tukiyaweka maisha  ya  chini tutapoteza  maisha ya juu  (angalia Marko 8:35). Anatupatia chaguo kuhusu  jinsi tutakavyoishi. Anatuambia kile  kitakachotufaa  na kisha kutuacha tuamue iwapo  tutafanya  au  la.  Ninaweza  kuendelea kuwa  mchoyo na pia wewe  waweza kufanya hivyo, lakini  habari njema  ni  kwamba si lazima  tufanye hivyo.
Tuna nguvu ya  Mungu ya  kutusaidia kuyapita  mambo yetu na kuishi  maisha ya kuwafanya watu wengine waishi maisha bora.

Safari
Uchoyo  si tabia  ya  kujifunza, tunazaliwa  nayo.  Ni sehemu ya maumbile yetu.  Biblia inautaja  uchoyo  kuwa  “maumbile ya  dhambi.” Adamu na Hawa  walifanya  dhambi kwa  Mungu kwa  kufanya  kile alichowaamuru wasifanye na  dhambi kuu waliyoifanya  ilipitishwa kwa  kila mtu ambaye  alizaliwa.  Mungu  alimtuma Mwanawe  Yesu afe kwa ajili  ya dhambi, na kutukomboa kutokana  na dhambi  hiyo. Alikuja kutangua  kile  ambacho  Adamu alikifanya.  Tunapomkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yetu, Yeye huingia na kukaa pamoja nasi katika  roho  zetu na ikiwa tutaruhusu  sehemu hii iliyofanywa upya katika  nafsi zetu ili  kuyatawala  mawazo  yetu, twaweza kuishinda  dhambi ambayo imo milini  mwetu.

Dhambi huwa haiendi mbali, lakini Yule mkuu anayeishi ndani yetu hutusaidia kuishinda kila siku (angalia  Wagalatia  5:16).  Hii haimaanishi kwamba  hatufanyi dhambi, lakini tunaweza  kuimarika na  kupata ufanisi katika maisha yetu. Siwezi kusema kabisa  kabisa  kwamba  nimeushinda uchoyo,  na sidhani kama  kuna mtu yeyote  ambaye ameushinda  kabisa  uchoyo. Kusema hivi ni  kama  kusema kwamba  hatufanyi dhambi, kwa sababu dhambi yote inaanzia na aina  fulani  ya uchoyo. Sijashinda uchoyo  kabisa  kabisa,  lakini nina matumaini ya  kuimarika kila  siku. Niko safarini na ingawa  huenda  sitawasili, nimejitolea kwamba wakati  Yesu atakapokuja  kunichukua kurudi nyumbani,  atanipata ninaendelea kusukuma lengo hili (angalia Wafilipi 3:12-13). Mtume  Paulo alisema maneno  yafuatayo: “Nimesulubiwa pamoja  na Kristo; lakini ni  hai; wala  si  mimi  tena, bali Kristo yu hai  ndani yangu;  na  uhai nilio nao  sasa  katika  mwili, ninao katika imani ya  Mwana  wa  Mungu,  ambaye alinipenda akajitoa  nafsi yake kwa  ajili yangu  (Wagalatia  2:20).  Paulo  alimaanisha  kwamba  haishi tena kwa  ajili  yake mwenyewe na mapenzi yake, bali kwa  Mungu na  mapenzi ya  Mungu. Nilitiwa moyo  sana  siku moja  wakati nilipogundua kupitia mafunzo ambayo Paulo alisema maneno haya  miaka  ishirini  baada  ya  kuokoka  kwake.  Kujifunza kuishi bila uchoyo ndiyo iliyokuwa  safari  yake, kama  ilivyo kwa  kila mmoja wetu. Paulo pia alisema “Nina kufa kila siku  (ninakabiliwa na kifo kila siku na kufa ndani yangu).”  (1 Wakorintho  15:31). Kwa  maneno mengine kuwatanguliza  wengine kwanza vilikuwa vita  vya  kila siku na kulihitaji uamuzi wa  kila siku.

Kila mmoja  wetu lazima  aamue  jinsi tutakavyoishi na  kitakachotufanya tuishi kwacho,  na  hakuna  wakati bora  wa  kufanya  hivyo  kuliko sasa.  Wewe na  mimi tuna  wakati  mmoja  wa  kuishi na  uhai  mmoja wa  kutoa,  kwa   hivyo swali ni: “Je, tutaishi vipi?”  Ninaamini kabisa kwamba ikiwa kila mmoja wetu atafanya sehemu yake kuyatanguliza maslahi  ya  watu wengine kwanza  basi  twaweza  kuona  na  kuwa sehemu ya mageuzi yenye uwezo wa kubadili ulimwengu.
Mtumishi.

No comments:

Post a Comment