![]() |
Ni Kazi Ya Nani?? |
Hii ni hadithi niliyoisikia miaka kadhaa iliyopita kuhusu watu wanne waitwao Kila mtu, Mtu fulani, Mtu yeyote, na Hapana Mtu... Kulikuwa na kazi muhimu ya kufanywa na Kila Mtu alikuwa na uhakika Mtu fulani angeifanya. Mtu yeyote angeliifanya, lakini Hapana Mtu aliyeifanya. Mtu Fulani akakasirika kuhusu hayo kwa sababu ilikuwa kazi ya Kila Mtu. Kila Mtu alifikiri Mtu yeyote angeliifanya, lakini Hapana Mtu aliyetambua kwamba Kila Mtu hangeliifanya. Mwishowe, Kila Mtu alimlaumu Mtu fulani wakati Hapana Mtu aliyefanya kile kile Mtu yeyote angelifanya.
Wakati fulani nilisoma kuhusu kisa cha kushangaza kinachoonyesha mambo muhimu ya hadithi hii ya kusikitisha ya ukweli. Mnamo mwaka 1964 Catherine Genovese alidungwa kisu na kufariki katika kipindi cha dakika thelathini na tano ilhali majirani thelathini na nane wakitazama. Hatua waliyochukua ilielezewa kuwa baridi na ya kutojali, matokeo ya ubaguzi wa mijini.
Baadaye, utafiti uliofanywa na Latane na Darley ulionyesha kwamba hakuna mtu aliyesaidia kwa sababu kulikuwa na watu wengi walioshuhudia kwa kuangalia tu. Watu hao waliangaliana ili wapate mwongozo kuhusu kile wanachopaswa kufanya. Kwa vile hakuna aliyefanya lolote, walibaini kwamba hakuna anayepaswa kufanya lolote. Watu huenda wasipate msaada wakati wanapouhitaji huku idadi ya wapita njia ikiongezeka.
Mwanafunzi mmoja aliyekuwa na maradhi ya kifafa alisaidiwa kwa asilimia 85 wakati mpita njia mmoja alipokuwa karibu, lakini wakati watu kadhaa waliposimama karibu naye na kutazama alipokea msaada wa asilimia 31 pekee.
Ufatifi huu unadhihirisha kwamba kadiri watu wengi zaidi wanapokosa kufanya jambo, watu zaidi hawatafanya lolote, bali ikiwa hata kundi dogo la watu waliojitolea litaanza kuwasaidia watu wengine kwa kuwatunza na kuwapenda, kutabasamu na kuwakubali, kuwaheshimu na kadhalika, kundi hilo linaweza kukua. Utafiti umethibitisha kwamba tunaathiriwa sana na kile watu walio karibu nasi hufanya. Tunaangaliana ili kupata mwelekeo hata wakati tusipofahamu kwamba tunafanya jambo hilo. Watu wengi watakubaliana na maoni ya wengi hata ikiwa kweli hawakubaliani na maoni hayo. Hufanya hivyo ili wawe sehemu ya kundi.
Ikiwa tunataka kuwa sehemu ya Mageuzi ya Upendo, sisi kama Wakristo lazima tuwe mfano kwa wengine badala ya kujiunga kwenye mfumo wa ulimwengu. Mtu fulani mwenye ujasiri wa kutosha angetokea kuchukua hatua au kuwa na upendo mwingi wa kusaidia, maisha ya Catherine Genovese yangeokolewa.
No comments:
Post a Comment