Nilisikia hadithi moja kuhusu mwanaume mmoja aliyekwenda nchini Urusi akiwa na nia nzuri ya kuwaambia watu kuhusu upendo wa Yesu Kristo. Wakati wa ziara yake, watu wengi walikuwa wanakabiliwa na njaa. Alipopata foleni ya watu wakisubiri kwa matumaini ya kupata mkate wa siku, aliwafuata akiwa ameshika vijikaratasi vya habari ya injili mkononi na akaanza kutembea akifuata foleni hiyo akiwaambia kwamba Yesu anawapenda na kumpa kila mmoja kijikaratasi chenye habari ya ujumbe wa wokovu. Kwa kweli, alikuwa anajaribu kusaidia, lakini mwanamke mmoja akamwangalia machoni mwake na akasema kwa uchungu, “Maneno yako ni matamu, lakini hayajazi tumbo langu lililo tupu.”
Nimejifunza kwamba baadhi ya watu wanaumia vibaya mno kusikia habari njema kwamba Mungu anawapenda, ni lazima washuhudie upendo huo na njia moja bora ya jambo hilo kutendeka ni kupitia sisi ili kutimiza mahitaji yao kwa vitendo na vile vile kuwaambia kwamba wanapendwa. Ni lazima tujihadhari juu ya kufikiri kwamba maneno yanatosha. Yesu vile vile alihubiri kuhusu habari njema, lakini mahali alikokwenda alitenda mema na kuwaponya wote waliopondeka mioyo (angalia MDO 10:38).
Lazima tujihadhari juu ya kufikiri kwamba maneno yanatosha. Kuongea si ghali, wala hakuhitaji juhudi kubwa, lakini upendo halisi ni ghali. Ulimgharimu Mungu Mwanawe wa pekee na kuuruhusu upendo halisi kutiririka kwetu pia nasi twahitaji kugharamika. Pengine tutahitaji kuwekeza muda, fedha, juhudi au mali zetu… lakini utatugharimu!
Mungu Anatutegemea Sisi Nitaondoka nyumbani hivi karibuni kwenda kupata kikombe cha kahawa na marafiki zangu na baadaye twende kwa chakula cha mchana. Pengine tutatumia muda wa saa mbili na wakati huo takribani watoto 240 watakuwa wametekwa nyara na kuingizwa katika sekta ya ulanguzi wa kingono. Hii inamaanisha kuwa watoto wawili kila dakika maisha yao yataharibiwa na mtu aliye mchoyo na mlafi na ni hadi pale tutakapofanya jambo.
Twaweza kufanya nini? Twaweza kujali, twaweza kupata habari, twaweza kuomba na twaweza kuchukua hatua. Twaweza kusaidia huduma na mashirika yenye kumbukumbu zilizothibitishwa za kuwaokoa watoto na wanawake kutokana na hali hizi za kutisha, au ikiwa Mungu ametupatia mzigo huo twaweza hata kuchagua kufanya kazi katika maeneo haya.Ikiwa kazi ya kufanya kila siku haiwezekani, twaweza kufikiria kufanya mradi fulani au kufanya ziara fupi ya huduma ya umishenari.
No comments:
Post a Comment