Wanyama mbalimbali huwa na silika tofauti wanapotishwa au wanapokabiliana na woga. Kushambuliwa na dubu, kupandwa na kuchakuro, kushtuliwa na paa anayekimbia, na fuko anayechimbua. Muitikio haya yote ya silika yanafanya kazi.
Lakini kuna mdudu mmoja ambaye huitikia kwa njia tofauti:huyu ni kifaurongo.
Kifaurongo ni mdudu ambaye hamkimbizi mtu, hapandi, hatoroki, au kuchimbua. Kifaurongo hujigandisha tu. Badala ya kufanya kitu, hujigandisha tu. Hujifanya amekufa— ndipo tunapata ule msemo wa Kiingereza unaosema “playing possum” (kujifanya kifaurongo)—na hutumaini kwamba kwa kujigandisha atakamilisha kitu fulani.
Nimeona hilo mara nyingi wakati watu wanapoumizwa au kutishwa, wanakuwa vifaurongo wa kiroho. Badala ya kufanya kitu, wanajigandisha tu.
Mambo yanapokuwa magumu, wanapokabiliana na uchungu fulani au kuvunjwa moyo, wanajigandisha. Wanaacha kusonga mbele. Je, hili ni jambo mnalolijua? Je, umewahi kujikuta katika hali ya kutulia mahali pamoja kwa sababu ya majaribu uliyokuwa huyatarajii au jambo la kuvunja moyo sana?
Je, umewahi kuwa katika hali fulani ambapo hujui ufanye nini, na hivyo ukaamua kuwa hutafanya kitu? Ikiwa umekabiliana na uchungu ambao umekugandisha njiani, basi fahamu kwamba sichukulii uchungu wako kuwa jambo dogo. Kusema kweli; nimepitia mambo mengi magumu ambayo yaliniumiza sana mpaka nikahisi kana kwamba siwezi kuendelea mbele.
Ninaelewa yale unayopitia, kwa sababu mimi pia nilihisi nimepoozeshwa na shida fulani. Lakini ningependa kukutia moyo kwamba katika uchungu unaopitia wakati mwingine jambo zuri zaidi la kufanya ni kuendelea kwenda mbele. Inawezekana bado huna majibu yote. Huenda ukashtushwa na hali hizo.
Huenda ukahisi kana kwamba ulimwengu umepasuka. Lakini katika hali hizo ngumu, ukiendelea kwenda mbele, itakusaidia ili usipoteze matumaini. Huenda hutaweza kuona mwanga wowote mbele, lakini ukimtwika Bwana fadhaa zako na uamini kwamba yuko pamoja nawe katika shida hii, utagundua uponyaji kadri unavyotembea pamoja naye. Hatimaye, si tu kwamba utaona mwangaza mbele yako, mwangaza huo utafukuzia mbali kitu chochote kilicho cha giza maishani mwako. Ninaelewa kwamba, kwa kutegemea ubaya wa hali unayokabiliana nayo, kutakuwa na siku ambazo utahisi kwamba hutaki kufanya kitu chochote. Ukipata hasara kubwa bila shaka ni jambo la kawaida kuanza mchakato wa kuomboleza unaojumuisha hatua mbalimbali.
Lakini kadri unapotia mchakato wa uponyaji, fahamu kwamba jibu la mwisho si kujitenga na kuishi maisha ukiwa umelemazwa na uchungu. Mungu anataka uendelee kupiga hatua ya imani, huku ukiamini kwamba atakuvusha salama kutokana na uchungu huo hadi kwenye kitu kizuri zaidi.
Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA... Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Zaburi 37:23-24
Fursa ya kumtumaini Mungu ni ya ajabu sana. Huturuhusu kuwa na matumaini wakati hakuna sababu yoyote ya kuwa na matumaini. Wakati inapoonekana kana kwamba umepoteza, unaweza kumtumaini Mungu aongoze hatua zako.
Nimeongea na rafiki ambaye amepitia kipindi kigumu cha kupambana na saratani. Amefikia mwisho wa matibabu sasa na yuko tayari kuanza kuishi maisha yake ya kawaida tena. Alisema, “Ninaona vigumu kujua jinsi ya kuendelea mbele kwa kuwa maisha yangu hayatakuwa kama vile yalivyokuwa awali.”
Pengine haya ni mambo unayoyajua vizuri. Huenda umefiwa na mpendwa wako na unashindwa utaishi namna gani bila mpendwa huyo. Huenda umefukuzwa kazi uliyoifanya kwa miaka na mwenyewe ulikuwa unaona utafanya kazi hiyo hadi ustaaafu. Utafanya nini sasa? Tambua hili hata ingawa hujui utafanya nini, Mungu anajua. Atakuongoza katika kila hatua utakayopiga.
Jimmy J.
Mtumishi.
No comments:
Post a Comment