"Wanawake wengi walioolewa wanajua kwamba kubadilisha jina kunahitaji mazoea. Ulikuwa unaitwa Yasinta Makokoto, lakini sasa unaitwa Yasinta Mapunda. Ulikuwa waitwa Sally Edward, lakini sasa unaitwa Sally Joseph. Inachukua muda kuweza kuzoea jina jipya, lakini kumbuka, Paulo alikuwa anakabiliana na tatizo lililokuwa zaidi ya mabadiliko ya jina— Paulo alikuwa anapokea mabadiliko ya moyo na pia asili. " -Nukuu
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. 2 Wakorintho 3:1
“Kuna mambo matatu ambayo ni magumu sana: chuma, almasi, na kujitambua mwenyewe.” —Jimmy J
Mabadiliko si rahisi—hata mabadiliko mazuri yanagharimu mazoea. Mungu anapotubadilisha, huchukua muda ndipo tukaweza kuamini kabisa kwamba kweli tumebadilika. Mtume Paulo alilifahamu hilo kuwa kweli. Tunapomfikiria Paulo, tunapata mtu aliyekuwa na imani kubwa sana, mwandishi wa sehemu kubwa ya Agano Jipya.
Mtu anaposimama kanisani na kusema, “Hebu natusome yale aliyosema Paulo katika Warumi,” au “Kama alivyosema Paulo katika kitabu cha Wagalatia...” hakuna anayepinga. Lakini kuna wakati Paulo alikuwa mtu aliyeshukiwa na kila mtu. Hakuwa mtume mkuu kabisa; alikuwa ni mwanadamu tu mwenye jina jipya na sifa mbaya: Alikuwa Farisayo wa Mafarisayo. Alikuwa mtesi wa kanisa la kwanza.
Mtu asiyeweza kuaminiwa. Kwa hiyo nashangaa ikiwa kulikuwa marekebisho—wakati ambapo Paulo alihisi yeye ni Sauli zaidi kuliko Paulo. Nashangaa ikiwa ilimchukua Paulo muda kumwacha Sauli. Nashangaa ikiwa alimsalimia mtu kwa mkono na kusema, “Habari gani. Naitwa Sauli... er...um...Yaani, Paulo. Naitwa Paulo.”
Wanawake wengi walioolewa wanajua kwamba kubadilisha jina kunahitaji mazoea. Ulikuwa unaitwa Yasinta Makokoto, lakini sasa unaitwa Yasinta Mapunda. Ulikuwa waitwa Sally Edward, lakini sasa unaitwa Sally Joseph. Inachukua muda kuweza kuzoea jina jipya, lakini kumbuka, Paulo alikuwa anakabiliana na tatizo lililokuwa zaidi ya mabadiliko ya jina— Paulo alikuwa anapokea mabadiliko ya moyo na pia asili.
Hebu mfikirie akisema “Habari gani. Naitwa Paulo. Sasa mimi ni mfuasi wa Yesu. Ningependa kukwambia habari zake.” Lazima watu walimtazama huyu mtesi wa WakristoFarisayo-aliyegeuka na kuwa mhubiri na kujisemea Ngoja kidogo. Huyu ndiye yule jamaa aitwaye Sauli. Nimesikia habari zake. Yeye huwakamata na kuwatesa Wakristo... Simwamini na naona vigumu kuamini ikiwa kweli amebadilika! Hata ingawa tunaweza kubahatisha jinsi watu mtaani walivyouchukulia utambulisho mpya wa Paulo, Biblia inatwambia namna wanafunzi walivyochukulia jambo hilo—hawakukubali.
Hawakushawishika kwamba Paulo alikuwa mtu mpya. Matendo 9:26 inasema: “Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.” Ni kwa sababu tu Barnaba alisimama mbele ya wanafunzi na alitetea tabia ya Paulo ndipo wakakubali kumpokea.
Bila shaka, tunajua kwamba hatimaye walimpokea, na sehemu ya hadithi iliyosalia ni historia ya Biblia. Lakini kuna kirai kimoja katika kifungu kilichotangulia ninachotaka kuwaonyesha: “Wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.” Kitu cha pekee ambacho kingefanya kirai hicho kiwe kibaya zaidi ni kama kingesema: Paulo hakuamini kwamba kweli alikuwa ni mwanafunzi. Unajua, Paulo hangeweza kudhibiti yale waliyowaza wanafunzi. Ilibidi Barnaba aongee na wanafunzi, na ilibidi Mungu aibadilishe mioyo yao. Hayo ni mambo ambayo hayakuwa chini ya uwezo wa Paulo.
Kitu cha pekee ambacho aliweza kukidhibiti ni mtazamo . Ukweli usemwe, yamkini haikujalisha watu walikuwa wanaamini nini. Kilichokuwa muhimu ni kile alichoamini Paulo. Kama hangekubali vile alivyo mtu mpya ndani ya Kristo, basi hangeweza kuifikia hatima yake maishani.
Hebu fikiria Paulo anatembea mitaani huku akijisemea Natamani ningeweza kusafiri na kulihubiri Neno la Mungu. Hilo ndilo jambo la kutenda lililo moyoni mwangu. Lakini nilikuwa mtesi wa kanisa. Nitakuwa Sauli wakati wote. Au kama angefikiria Nilianza maisha yangu kuchelewa. Hakuna vile ninaweza kufanya mambo yote niliyotamani kumfanyia Mungu. Nilikuwa Sauli kwa muda mrefu.
Kama huo ungelikuwa ndio mtazamo wake, Paulo angekuwa mtu wa kusikitisha, na hangetimiza yote aliyopangiwa na Mungu. Lakini Mungu alipoanza kufanya kazi maishani mwake, Paulo alielewa kwamba hakuwa Sauli tena, kwa hiyo akaacha kuishi kama Sauli. Hakufikiria tena kama Farisayo, hakuongea tena kama Farisayo, au kutenda kama Farisayo. Mambo yalikuwa tofauti sasa.
Alikuwa amebadilishwa. Alikuwa amepewa matumaini. Na akachagua kuishi hivyo. Ni Paulo, ambaye kwa pumzi ya Roho Mtakatifu, aliandika: Hata imekuwa, mtu akiwa [ameunganishwa] ndani ya Kristo (Masihi) amekuwa kiumbe kipya (kabisa); ya kale [ile hali ya zamani ya kiroho na kimaadili] yamepita, tazama! Yamekuwa mapya! 2 Wakorintho 5:17 (imeongezwa msisitizo) Kwa sababu kutahiriwa [sasa] si kitu, wala kutotahiriwa, ila [tu] kiumbe kipya [ambayo ni matokeo ya kuzaliwa mara ya pili na asili mpya katika Kristo Yesu, Masihi]. Wagalatia 6:15 (imeongezwa msisitizo) Paulo alijaa matumaini, na alisisimka juu ya maisha yake kwa sababu “mapya kabisa” yalikuwa yamemfikia—sasa alikuwa na asili mpya katika Kristo Yesu.”
Paulo hakutembea tena huku akiwaza, kuongea, kuwa na wasiwai, akifanya kazi, na kutenda kama Sauli. Alikuwa amebadilishwa. Paulo alipokea mambo mapya ambayo Mungu alikuwa anafanya katika maisha yake, fursa mpya zilizokuwa mbele yake, na yule mtu mpya ambaye Mungu alikuwa amepanga awe.
No comments:
Post a Comment