Kinachohitajika kuwezesha uovu kupata ushindi ni watu wema kutulia na kutofanya chochote. Jimmy J.
Kutofanya lolote ni rahisi, lakini pia ni hatari sana. Mahali ambapo hakuna pingamizi ya kuzuia uovu, uovu huongezeka haraka. Sote mara nyingi huangukia mtego wa kulalamika kuhusu mambo yaliyo kasoro katika jamii yetu na maishani, lakini kulalamika hakufanyi kitu isipokuwa kutuvunja moyo hata zaidi. Hakubadilishi kitu, kwa sababu hakuna uwezo ufaao ndani yake.
Hebu fikiria ulimwengu ungekuwa vipi iwapo yale Mungu aliyofanya ni kulalamika kuhusu kila kitu kilicho kasoro tangu alipouumba. Lakini Mungu halalamiki. Yeye anaendelea kuwa mzuri na kutekeleza haki. Anajua anaweza kushinda uovu na uzuri! Uovu una nguvu kwa kweli, lakini uzuri una nguvu zaidi.
Twahitaji kukoma na kutambua kwamba Mungu anafanya kazi kupitia watu Wake. Ndio, Mungu ni mzuri wakati wote. Lakini Amechagua kufanya kazi hapa duniani kupitia watoto wake.. wewe na mimi. Ni jambo la kunyenyekeza kutambua kwamba anaweza kufanya mengi iwapo tungejitolea kupenda na kufanya mambo mazuri wakati wote.
Tunahitaji kukumbuka kwamba maagizo ya Yesu’ katika Mathayo 5:16: “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”