Thursday, 5 July 2018

Yesu Ni Nani...??

Nimemtaja  Yesu mara kadhaa lakini sijakueleza kumhusu. Ni muhimu nikueleze kuhusu  Yesu kwani ni vigumu kuwa sawa na Mungu bila kumjua  Yesu. Ni vigumu kuzaliwa mara ya pili bila kumjua Yesu,Ninasema kwamba bado una uamuzi muhimu wa kufanya.
Kila jambo kuhusu uamuzi huo linategemea ufahamu wako kuhusu Yesu na kujua kile ambacho amekufanyia. Baada ya hayo uamuzi wako utakuwa ni kuamua endapo utaamini na kupokea au utataka kuendelea katika giza jinsi ulivyo (ikiwa hujazaliwa mara ya pili). Sasa niko tayari kukuelezea kitu ambacho kwa akili yako hutaweza kukielewa bali moyo wako utataka kuamini. Kwa hiyo uwe tayari kusoma hadithi hii ya kweli ambayo inaweza kugeuza maisha yako milele.

Biblia inasema katika kitabu cha Mwanzo mlango wa kwanza na wa pili kuwa hapo mwanzo, Mungu alimuumba mtu wa kwanza na akamwita  Adamu. Mungu akautengeneza  mwili wake kutoka kwa mavumbi ya ardhi  na akampulizia puani pumzi ya uhai; na mtu huyu akawa nafsi hai. Kwa maneno mwengine tutasema alianza kuwa hai Mungu alipompulizia baadhi ya sehemu yake. Pumzi ya Mungu iliingizwa ndani ya mwanadamu naye akawa hai.  Alijaa “uhai wa Mungu.”
Mungu alimwita “Adamu”. Biblia inasema   Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. (Mwanzo 1:26). Kuna mambo kuhusu  Adamu ambayo yalikuwa sawa na Mungu. Alikuwa na asili, tabia na pumzi ya Mungu.
Alikuwa mtakatifu na mwema  kama Mungu. Hakuna uovu wa aina yoyote uliokuwa ndani ya  Adamu.  Yeye na Mungu walikuwa na ushirika kwa sababu walikuwa wamefanana. Biblia inasema nuru haiwezi kushirikiana na giza.Mungu na Adamu, wote wawili walikuwa nuru kwa hivyo walikuwa wanaweza kushirikiana.   Adamu hakuwa na shida na Mungu.

Je, Kuna utulivu katika uhusiano wako na Mungu?
Adamu aliumbwa akiwa na “hiari” pia – yaani ule uhuru wa kuchagua kufanya chochote alichotaka. Mungu alimuambia yale yaliyokuwa ya haki lakini akampa uwezo wa kuchagua pia:  Adamu alikuwa mwema, lakini ili kuendelea kuwa mwema  ilimbidi awe akimfuata Mungu na  njia zake. Mungu aligundua kwamba  Adamu alihitaji  msaidizi, mwenzake. Kwa hiyo akamletea usingizi na akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake. (Mwanzo 2:21,22). Mungu akaufanya ubavu wa  Adamu mwanamke ili awe msaidizi, mwenzi. Tazama, mwanamke hakutolewa kwa miguu ya Adamu kwa sababu Adamu hakuwa amkanyage na kusimama juu yake. Hakutolewa kichwani mwake ili awe juu ya mumewe bali alitolewa ubavuni ili awe mshirika wake katika maisha.
Kufikia sasa katika hadithi yetu tuna jamaa inayoishi duniani katika 
bustani ya Edeni, Mungu akiwa amewatengenezea shamba nzuri kwa wao kuishi. Ni dhahiri kwamba Mungu alitaka wafurahie maisha.

Je unafurahia maisha?
Kulikuwa na kiumbe kingine duniani kisicho cha kufurahikia, Shetani, ambaye hapo awali alikuwa ameasi mpango wa Mungu kwake wa kuwa malaika anayeongoza sifa na kuabudu. 
Alipotoka na kuanguka kwa kuasi na kutaka zaidi ya yale Mungu alikuwa amempa.  Alitaka kuwa msimamizi na wala sio chini ya uongozi wa Mungu. Alisema   atakiinua kiti chake juu kuliko enzi ya Mungu, naye Mungu  akamtupa yeye pamoja na malaika  waliokuwa wamejiunga katika uasi wake kutoka Mbinguni. Jehanamu ikatengenezwa kwa ajili yao lakini shetani na mapepo wengine wengi walipewa nafasi ya kuingia duniani.

Kuna wakati uliotengwa katika mpango wa Mungu ambapo  wote hao watafungiwa Jehanamu milele, lakini kwa wakati huu, Mungu anamruhusu Ibilisi (Shetani, Lusifa) kuingia duniani kwani waume kwa wake bado wangali katika hali ya  kuchagua  ni nani watakayemtumikia. Ni wazi kwamba ili kuweza kuchagua, sharti kuwe na zaidi ya kitu kimoja kilicho mbele ya yule anayehitajika kufanya uchaguzi. Mungu ameleta uzima, furaha, imani, amani, haki, tumaini na mambo yote mazuri.
Shetani analeta kifo, giza, kukata tamaa, kufinyiliwa chini, kuharibu, hofu, woga na kila kitu kibaya. Hata ninapoandika mambo haya, ninashangaa ni kwa nini  mtu atamchagua shetani na njia zake? Ukweli ni kwamba wengi hufanya hivyo. 
Watu wengi wamedanganyika.  Wanachagua njia isiyofaa kwa sababu hawana ufahamu.  Hosea 4:6 inasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.” Huenda hujapata ufahamu wa kutosha kufanya chaguo bora hadi wakati huu.
Nakutolea  ukweli huu nikitumaini kwamba maelfu na maelfu ya watu watapata ufahamu unaohitajika kufanya uchaguzi unaofaa.

Tuendelee na hadithi yetu.  Adamu na Hawa (ndilo jina  Adamu alilomwita mkewe) walikuwa wanafurahia maisha katika bustani ya Edeni. Mungu aliwapa mamlaka ya kumilki ardhi. Aliwaambia kile walichostahili kufanya na kile ambacho hakikustahili; kumbuka, walikuwa huru kujichagulia kile walichoona kinawafaa. Mungu alikuwa akiwaambia yale aliyotaka wayafanye, jinsi maisha yao yangebarikiwa lakini hakuwalazimisha kuyafanya. Katika Bustani hiyo ya Edeni Mungu alikuwa ameweka miti mingi ya matunda ya wao kula kwa uhuru lakini kulikuwa na mti ambao matunda yake hawakupaswa kula- “mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” (Mwanzo 2:17). 

Huenda unashangaa ni kwa nini Mungu aliweka mti mmoja katika shamba hilo na kuwaambia wasile matunda yake. Kumbuka, ili uweze kujichagulia, lazima uwe na zaidi ya kitu kimoja. Ikiwa walikuwa wachague kumtii Mungu basi sharti kungalikuwa na kitu ambacho kukichagua matokeo yake yangekuwa ni kutomtii Mungu.
Mungu alitaka upendo na utiifu wao. Ukweli  ni kwamba utiifu ni tunda la upendo.  Alilitaka tunda hilo la utiifu, lakini lisingekuwa na manufaa kwa Mungu ikiwa halikutolewa kwa uhuru kama tendo la hiari, kwa kujichagulia wao wenyewe.

Je utafurahia na kubarikiwa ikiwa wengine watakupenda kwa sababu umewalazimisha kwa kutowapa uhuru wa kujichagulia? Mungu alimuumba Mwanadamu na kumpa hiari, na akamwaachia mambo machache muhimu ya kujichagulia. Hata leo uko katika hali hiyo hiyo. Una hiari, uko huru kujichagulia na una uamuzi muhimu wa kufanya.

Tuendelee na hadithi yetu,  Adamu na Hawa walikuwa wakifurahia maisha, wakimfurahia Mungu, bustani, matunda mazuri na vitu vingine vyote vizuri ambavyo Mungu alikuwa ametengeneza. Mwanzo 3 inatuambia kwamba Shetani alimtokea Hawa kwa mfano wa nyoka. Hakuogopa nyoka kama wewe na mimi tunavyofanya leo.

Nyoka hakuwa mnyama mbaya. Shetani aliitumia, au alijitokeza kwake kwa mfano wa nyoka. Kupitia nyoka, alianza kumuuliza Hawa maswali ambayo yalimfanya kuanza kufi kiria (kuwa na “fikra” kama zile zinazungumziwa katika waraka wa pili wa  Wakorintho 10:4,5 ambazo hujiinua juu ya elimu ya kweli ya Mungu) ni kwa nini Mungu aliwaambia wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kwa kweli Mungu kamwe hakutaka wajue chochote kuhusiana na uovu. Lakini kumbuka walikuwa na chaguo la kufanya.

Mungu alimwambia  Adamu kwamba ikiwa angalikula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya  basi hakika atakufa. (Mwanzo 2:17.) Alimaanisha watakufa ndani sio miili yao.  Alimaanisha uhai ulio ndani yao utakufa. Nuru itaondoka  na watakuwa giza.
Hivi majuzi mtu mmoja aliyeishi maisha ya uovu mwingi alikuwa anafanyiwa upasuaji. Alidhani atakufa, na alitaka kulainisha maisha yake na Mungu. Tulipokuwa tukizungumza naye mimi pamoja na Joel rafiki yangu, alisema “Nahisi nimekufa ndani.” Hebu litafakari jambo hili.

Alitaka kuzaliwa mara ya pili kwa sababu alikuwa anahofu atakufa kimwili akiwa angali anafanyiwa upasuaji hata ingawa ukweli ni kwamba alikuwa mfu ndani yake maisha yake yote, na aliyakiri hayo kwa kinywa chake mwenyewe.
Je uko hai au umekufa?
Nyoka  alimdanganya Hawa. Alisema “hakika hamtakufa” (Mwanzo 3:4). Kile alichosema kilikuwa kinyume na kile Mungu alikuwa amesema; hivyo basi, ilikuwa ni uongo. Neno la Mungu ni kweli. Na hapa mwanzo unaona asili ya Shetani.  Yeye ni kinyume na yote yaliyo ya Mungu.Mungu anataka wewe uwe na yale mazuri. Shetani anataka kukuharibu.  Hata wakati huu hutekeleza haya kupitia uongo na udanganyifu, sawa na jinsi alivyomfanyia Hawa.
Aliendelea kumlaghai na kumdanganya na kumuuliza maswali ambayo yalimfanya aanze kufi kiria  (“fi kira” ambazo zinajiinua kinyume cha ukweli wa Mungu). Hatimaye alikubali ushauri wa Ibilisi na  kumshawishi mumewe kufanya vivyo hivyo. Wote wakamuasi Mungu kwa kula tunda ambalo alikuwa amewaagiza wasile. Matokeo yake yalikuwa jinsi Mungu alikuwa amesema- walikufa kiroho.

Mungu alipokuja tena katika bustani ya Edeni kuwatembelea Adamu na Hawa, walijifi cha kwa sababu walikuwa wameogopa.

Je umekuwa ukijificha kumhepa Mungu kwa sababu ya uoga?
Mara tu Mungu alipogundua wanaogopa,  Alitambua kwamba walikuwa wamefanya dhambi.  Walikuwa wameamini uongo wa Shetani. Walikuwa wamejaribiwa na kuanguka na sasa walikuwa wamepata matokeo ya kile walichokuwa wamechagua.  Woga unatokana na dhambi; ni tunda la dhambi.

Unaweza kuwa na matokeo ya chaguo lako. Lakini Kumbuka, baadhi ya matokeo hayo ni machungu kinywani mwako!
Mungu alianza kukabiliana nao kuhusu dhambi yao, lakini pia papo hapo alikuwa na mpango wa ukombozi na wokovu wao kutokana na hali waliyojikuta wameingia.Katika Mwanzo 3:15, Mungu alimwambia nyoka kwamba uzao wa mwanamke (mbegu yake)  utaponda kichwa chake, naye (Shetani) ataponda kisigino cha uzao wa mwanamke. Mungu alikuwa akizungumza kuhusu  Yesu, Mwanaye wa pekee ambaye alikuwa tayari anaishi katika ulimwengu wa Roho.

Mungu ni wa utatu. Huwa tunamtaja kama “Utatu”: Mungu mmoja katika watatu - yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kila mmoja wa utatu ana jukumu muhimu la kutekeleza maishani mwako.
Tayari  Yesu alikuwa anaishi katika ulimwengu wa kiroho, lakini ili kumsaidia mwanadamu kutokana na hali yake mbaya, ilibidi Yesu aje duniani. Ilimbidi aingie katika mwili wa binadamu, mwili kama wako na wangu.  Alihitaji ajinyenyekeze na kuwa binadamu. Kumbuka  Yesu ni Mungu kikamilifu, Mwana wa Mungu. 

Kwa usemi mwingine  yeye ni Mungu halisi kutoka kwa Mungu halisi. Alikuwa  Mungu na anabaki kuwa Mungu hata sasa. Mpango ulibuniwa, lakini usingaliweza kutimizwa hadi kufi kia wakati kamili wa Mungu,  kulingana na mpango wake kuhusu mambo yote.   Waefeso 3:10 (Tafsiri ya  AMPLIFIED) inadhihirisha kusudi la Mungu, ambalo ni kwamba sasa, kwa njia ya kanisa  (1), hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi na  ya sehemu nyingi tofauti isiyoweza kuhesabika ijulikane kwa falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho wa mapepo na mtawala wao Ibilisi, ambaye aliasi.
Kwa lugha rahisi,  tuko vitani- vita kati ya Shetani na Mungu! Tayari imekwisha thibitishwa, na tangu jadi, imethibitishwa ni nani atakeyeshinda vita hivyo. Ni Mungu atashinda. Sherehe ya ushindi imepangwa. Je, Unapigania nani katika vita hivyo? Ikiwa unamtumikia Shetani na unaamini uongo wake, basi unamfanyia kazi mtu aliyeshindwa. Mungu ndiye aliye na kikundi cha washindi.

Hata hivyo huu ndio mpango kamili wa Mungu: atawatumia watu waliozaliwa mara ya pili - watu wanaompenda, wanaomtii na (1)  Kanisa sio jengo. Kanisa linajumuisha waumini wote waliozaliwa mara ya pili ambao wamewahi kuishi. kumtumikia kwa  hiari  yao - kushinda na kumwangamiza kabisa Shetani na mapepo yake.

Huenda ukashangaa ni kwa nini Mungu alituhusisha katika vita hivi. Kumbuka, Shetani alimshinda mtu wa Mungu katika Bustani ya Edeni na kumwibia alichokuwa amepewa na Mungu.Ukweli ni kwamba mwanadamu, kwa sababu ya kudanganyika, ndiye aliyempa shetani kile alichokuwa amepewa na Mungu. Itakuwa hatia kwa Mungu kuvichukua vyote mwanadamu alivyompa shetani, na kumrudishia mwanadamu. Kile ambacho Mungu anafanya na amekuwa akifanya tangu shamba la Edeni na ambacho ataendelea kufanya hadi kazi itakapokamilika ni hiki:   Anampa mwanadamu ujuzi na maarifa ili aweze kutwaa kile Shetani alimwibia. Yesu ndiye ufunguo Kwa mpango huo wote Hebu niendelee na hadithi yetu kutoka Mwanzo 3 Mungu alipomwambia Shetani kwamba hatimaye kichwa chake kitapondwa.  (Hii inamaanisha mamlaka yake yataharibiwa). 

Mungu tayari alikuwa amesema kile kitakachotimia na ikiwa Mungu amesema kitu, lazima kitatendeka. Kabla jambo hili halijatendeka, miaka 2000 ilipita huku wanaume na wanawake wakiendelea kuongezeka. Dhambi ilizidi na matatizo kuongezeka duniani. Mahali ambapo dhambi inazidi, kawaida matatizo huongezeka. Mwanadamu sasa alikuwa mwovu na mdhalimu na hakuwa sawa na Mungu. Kanuni ya dhambi ilidumu ndani ya mwili wa mwanadamu. Alikuwa na asili ya dhambi. Kwa matamshi mengine  lilikuwa jambo la kawaida mwanadamu kufanya dhambi sasa.

Haikumbidi eti ajaribu kufanya dhambi, alikuwa na asili yake ndani yake. Ukweli ni kwamba hangeweza  kuepuka kufanya dhambi. Kila mara watoto walipozaliwa, walikuwa na asili ya dhambi ndani ya miili yao.(2)  Watoto hawahesabiwi dhambi hadi wanapofi kia umri fulani wa kujua mema na mabaya. Hii inaelezea wakati wanapofi kia kiwango cha kutambua matendo yao ni dhambi mbele za Mungu, na wana fursa ya kuchagua kumtii Mungu au kukataa kumtii. Nina asili ya dhambi; nawe pia unayo asili hiyo; kila mmoja anayo asili hiyo. Tunazaliwa nayo.
Tunawajibika mbele za Mungu kadri tunavyotambua dhambi yetu.

Sheria
Mungu anawapenda watu wake sana, na alibuni mpango wa muda ambao utawafaa wale wanaompenda na kuchagua njia zake-mpango ambao utamwezesha kuwa na ushirika na watu wake tena. Unaona wakati dhambi iliingia na mwanadamu akafa kiroho, mwanadamu hangeweza kuwa na ushirika mzuri na Mungu. Mungu ni roho na lazima tuwe na ushirika naye rohoni mwetu. Mungu ni nuru. Mwanadamu sasa alijaa giza, kwa hiyo ushirika, ule upamoja, umoja na uhusiano kati yake na Mungu ulivunjika. Biblia inasema sasa kulikuwa na pengo kati ya Mungu na mwanadamu - kuvunjika kwa uhusiano wao. Unaweza kusema ukuta wa dhambi ulijengwa kati yao. (2)  Mwili wa mwanadamu unajumuisha  nyama na nafsi.
Mungu akabuni sheria, mfumo wa maagizo na taratibu zilizoandikwa ambazo mwanadamu alipaswa kuzingatia maishani mwake endapo angependa kuwa mtakatifu, na sawa kuwa rafi ki wa Mungu. Sheria hii ilikuwa kamili na  takatifu, ya haki na ya kupendeza. Ilielezea wazi kile ambacho mwanadamu alipaswa kufanya ili awe mtakatifu.

Kabla ya  Adamu kutenda dhambi, alijua bila kuwaza kokote kile Mungu alitaka afanye na kile ambacho hakustahili kufanya. Walikuwa kitu kimoja katika Roho, moyo mmoja, pamoja katika lengo. Baada ya kutenda dhambi, mwanadamu hakuwa tena na hisia za kumjua Mungu. Dhambi na matokeo yake yalimfanya kuwa mgumu. Hakujua tena yaliyokuwa katika moyo wa Mungu. Ilibidi yaandikwe.

Mwanadamu hangeweza tena kufanya mapenzi ya Mungu kutoka moyoni au rohoni mwake. Ilibidi ajaribu kumpendeza Mungu kwa uwezo wake wa kibinadamu. Lakini mwanadamu alishindwa kutimiza sheria yote kikamilifu kwani yeye hakuwa mkamilifu na kamwe hangeweza kuishi kama hapo mwanzoni akiwa angali hapa duniani. Sheria ya Mungu ilisema, ukivunja moja, basi umevunja zote (Waraka wa  Yakobo 2:10). Sheria ni kamilifu na ili aitimize, mwanadamu anahitaji kuwa mkamilifu pia.

Dhabihu
Japo walikuwa na sheria, hawangeweza kuitimiza licha ya juhudi zote walizofanya. Kwa sababu hiyo, Mungu alibuni  utaratibu wa kutoa dhabihu za kulipia au kufunika makosa yao na kushindwa kwao. Dhabihu hizo zilikuwa za umwagaji wa damu. Ililazimu kuwe na umwagaji damu. Hii huenda ikaonekana kama jambo lisilopendeza lakini sababu zake zaifanya  kueleweka. Mungu alipompulizia  Adamu pumzi ya uhai , alifanyika nafsi hai na damu yake ikajaa uhai. Damu yake ilianza kuzunguka mwilini. 

Biblia inasema “ Uhai wa mwili u katika damu” (Mambo ya Walawi 17:11). Wajua hii ni kweli. Hakuna mtu anayeishi bila damu. Ukisimamisha mzunguko wa damu basi maisha yako yatakoma papo hapo. Shetani alipowajaribu  Adamu na Hawa na wakachagua kutenda dhambi, dhambi ilileta kifo (Warumi 5:12) na kifo hicho kinawakilishwa na  magonjwa, maradhi, umaskini, vita, hasara, tamaa na wivu.  Kitu pekee chenye uwezo wa kufunika mauti ni uhai. Mwanadamu alipovunja sheria na kufanya dhambi, ilikuwa aina ya kifo. Dhabihu pekee iliyokuwa na uwezo wa kufunika dhambi ilikuwa ni dhabihu inayoambatana na umwagikaji wa damu kwani uhai upo ndani ya damu. (Mambo ya 
Sababu nyingine Mungu alifanya haya ni kwamba ilikuwa ni njia ya “kutazamia mbele” mpango bora aliokuwa nao katika mawazo Yake, mpango ambao ungetekelezwa kwa wakati utakaofaa kwa ajili ya wanadamu wote. Manabii waliendelea kutoa unabii kuhusu kuja kwa Masihi, Mwokozi, Mkombozi Mmoja ambaye atawakomboa watu wake. Mungu alikuwa anautangaza ujumbe wake. Kumbuka Mungu akisema jambo, lazima mwishowe  atalitimiza. Masihi huyu atafanyika dhabihu yao, dhabihu ya mwisho, dhabihu kamilifu. Atakuwa dhabihu, kamilifu, kondoo wa Mungu asiyekuwa na mawaa.

Hawakuhitaji kuendelea kuchinja kondoo asiye na mawaa katika madhabahu ya hekalu kama dhabihu ya dhambi zao. Yesu alikuwa aje kuwa dhabihu ya kutosha na ya mwisho. Dhabihu yake ndiyo ingeliweza kukomesha utaratibu wa sheria. Hebu nikunukulie mojawapo wa unabii kumhusu Masihi huyu: 

  • Isaiah 53:3-7 (Tafsiri ya  AMPLIFIED) “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humfi cha  nyuso zao,   Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. “Hakika ameyachukua masikitiko, magonjwa, udhaifu, na masumbuko yetu,   Amejitwika huzuni zetu; (za kuadhibiwa) Lakini kwa kutojua tulimdhania ya kuwa amepigwa,  Amepigwa na Mungu, na kuteswa (kana kwamba ana ukoma).“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,  Alichubuliwa kwa maovu yetu;    Adhabu ya (iliyohitajika kutuletea) amani yetu ilikuwa juu yake,  Na kwa kupigwa kwake (kulikomjeruhi) sisi tumepona. “Sisi Sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake  Maovu yetu sisi sote.“Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake;  Kama Mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo. Mbele yao wakatao manyoya yake;  Naam, hakufunua kinywa chake.”
Unabii kumhusu Mkombozi huyu uliendelea kutolewa.  Watu walikuwa wakimsubiri  Yeye, Mwokozi na Mkombozi wao. Siamini ikiwa kweli walielewa kile walichokuwa wanakingoja. Hawakuelewa kwamba atawakomboa kutoka kwa sheria, kutokana na “kazi” zilizohusika katika kujaribu kumpendeza Mungu kwa ukamilifu wakati haiwezekani.
Hawakuelewa kwamba  Yeye,  Yesu, Masihi, Mwokozi wa ulimwengu, angemwaga. Damu yake Msalabani, aache damu yake  imwagike, akimwaga uhai wake  kuondoa dhambi yote  kutoka kwa kila kizazi  (3). Walikuwa wakingoja, lakini hawakufahamu kile walichokuwa wanakingojea.

Yesu Aja
Wakati wa Mungu ukafika. Roho Mtakatifu akamtokea bikira mmoja aitwaye Mariamu. Akapata mimba kwa miujiza ya nguvu za Mungu – akawa mjamzito na mimba ya  Yesu, Mwana wa Mungu. Ilibidi itokee hivyo. Yesu alikuwa tayari akiishi kiroho huko mbinguni.  Alikuwa na Mungu tangu mwanzo. Lakini sasa alikuwa avae mwili ili aweze kusaidia wanadamu wote walio katika mwili na ambao walikuwa wamepotoka na hawakuwa na njia yoyote ya kujitoa taabani bila Mwokozi. Yohana Mtakatifu 1:1, 14 inasema kwamba  Yesu ni neno la Mungu na kwamba neno la Mungu lilifanyika mwili na likaishi miongoni mwa wanadamu. Waraka kwa  Waebrania 4:15 inasema  Yesu ni Kuhani  Mkuu anayeelewa udhaifu na kushindwa kwetu kwa sababu yeye alikuwa na mwili  kama wetu na nafsi kama sisi na alijaribiwa kwa kila njia (3)  Kumbuka uhai uko katika damu (Mambo la Walawi 17:11)lakini hakufanya dhambi.

Mpendwa hii ndio tofauti kubwa. Yesu alikuwa na uhai wa Mungu ndani  Yake, alikuwa kitu kimoja na Mungu kabisa.  Alikuwa kitu kimoja naye, sawa na jinsi  Adamu alivyokuwa kabla ya kufanya  dhambi. Biblia inamwita  Adamu wa pili. (angalia 1Wakorintho 15:45,47.)  Warumi 5:12-21 inasema ikiwa kwa kosa la mtu mmoja (Adamu) mauti  ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, basi si zaidi sana kipawa kile cha haki ya yule mmoja (Yesu) kitawafanya wanadamu wote kuwa na haki mbele za Mungu? Dhambi ya  Adamu ilikufikia kupitia kwa kuja kwako kizazi hadi kizazi. Sasa ikiwa utaamini  Adamu wa pili,  Yesu, anasubiri kukuvika haki yake.  

Adamu alikuwa mtu aliyejaa Mungu akiwa na uhai wa Mungu tele ndani yake. Dhambi ilikuja na mwanadamu akajaa giza. Nuru iliyokuwa ndani yake ilitoweka.

Je umejaa giza au nuru?
Yesu pia alikuwa mwanadamu, aliyezaliwa na mwanamke lakini alikuwa amejaa Mungu.  Adamu alifanya dhambi.  Yesu kamwe hakufanya dhambi; alikuwa dhabihu kamilifu ya dhambi. Waumini wa Agano la kale walikuwa wakitoa dhabihu za mara kwa mara kwa ajili ya dhambi zao, lakini dhabihu hizo hazingeweza kuondoa kule kujihisi kuwa na hukumu. Je unajihisi kuwa na hatia au uko huru? Mchafu au msafi ? Yesu alifanyika kondoo asiyekuwa na dhambi, kondoo wa kafara wa Mungu ambaye alichukua dhambi za ulimwengu.  Waraka kwa Waebrania 10:11-14 inasema:
“Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. “Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
“Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.”
Makuhani wa agano la kale walitoa dhabihu kwa niaba ya watu. Ilibidi wafanye hivyo mara kwa mara, kila wakati wakijibidiisha kuwa wema huku wakishindwa, na kukosa kufi ka mahali pa kujihisi kuwa wema (ndani yao), wakijaribu  kuwa  wema, ili  wajihisi wema. Lakini waraka kwa  Waebrania unatudhihirishia kwamba  Yesu alijitoa mara moja na kwa ajili ya wote akiwa dhabihu kamilifu. Alitimiza sheria zote.  Ushindi wake unaweza kupokelewa na wote wanaomwamini.
Soma inayofuata kwa Blog kwa makala inayosema Kilichotokea Msalabani.
Imeandikwa na Mtumishi wa Mungu
Jimmy J.

6 comments:

  1. Asante kwa makara nzuri namna hii.imenifanya nizidi kuogopa dhambi maana ni mateso na mzigo mzito.Asante Yesu kwa kutukomboa kutoka kwenye dhsmbi.na ambao bado hawajampokea Yesu wakisoma makala hii watampokea Yesu maana imeshiba mambo yote.asante Jimmy J.

    ReplyDelete
  2. Namuhitaji Yesu mtumishi

    ReplyDelete
  3. Tuwasiliane kwa no hii 0762402422

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimesoma makala hii nimesikia uchungu moyoni.nahitaji kuanza maisha mapya sasa.

      Delete