Monday, 17 December 2018

Mungu Anakupenda

Usifike mwishoni mwa maisha yako ukiwa umejawa na majuto ya hasara ya maisha yako kwa sababu uliyatumia  kwa. vitu visivyo  na  maaana  kamwe.......

Wakati  ni  karama  ya  ajabu  kutoka  kwa Mungu, na ni muhimu  tuwe waangalifu  sana tunatumia  wakati  wetu kufanya nini.  Wajua, mradi tu tumeshautumia  mda, hatuwezi kuupata tena.  Kuwa na wakati  na Mungu huleta  thawabu  ya ajabu,  lakini  vitu vingine vingi huleta sisimko lisilo na thamani kwa bei ghali.

Monday, 22 October 2018

Barua

Wapendwa wangu Mama na Baba.
    Tangu Niende Chuo kikuu Najua sijachukua Muda wa kuwaandikia na Naomba msamaha kukosa kufikiria kuwaandikia paka sasa.Nitawaeleza Mambo yote katika Barua hii lakini kabla hamjasoma Tafadhali ketini chini,Tafadhali msisome paka Mketi chini.
   Naendelea Vizuri sasa,Jeraha la fuvu la kichwa baada ya kuruka kwa dirisha la Bweni langu Sasa limepona,Niliruka baada ya bweni langu kushika moto muda mfupi.baada ya kuwasili hapa sasa huwa napata maumivu ya kichwa mara moja kwa siku.

Tuesday, 25 September 2018

Mimi ni Mageuzi ya Upendo.

Ninachagua huruma na kusalimisha misamaha yangu. Ninapinga maovu na kujitolea kufanya matendo ya Upendo wa Mungu. Ninakataa kutofanya lolote. Huu ndio uamuzi wangu. MIMI NI MAGEUZI YA UPENDO.- Imani yetu.

Mageuzi ni  jambo la ghafla, kubwa  na lililo  tofauti kabisa na jinsi  mambo yalivyo kama  kawaida.  Mageuzi huchochewa  na mtu mmoja au kundi  dogo sana la watu wasiokubali  kuendelea  kuishi kama  walivyokuwa  siku zilizopita.  Wanaamini  kuwa  lazima  jambo fulani lifanyiwe mabadiliko  na  huendelea  kuimarisha  mawazo yao  hadi pale msingi wao  unapoanzia  na hilo hatimaye huleta mabadiliko kwa njia kubwa.

Wednesday, 12 September 2018

Wewe Ni Nani: Tai au Ndege Mvumaji?

Makala moja katika jarida la   Reader’s Digest  ilisema: Ndege mvumaji na tai hupaa juu ya majangwa ya mataifa. Kile  ambacho tai  wote  huona ni nyama iliyooza, kwa sababu  hicho  ndicho  wanachotafuta.  Wananawiri  kwa lishe  hiyo.  Lakini  ndege  wavumaji  hupuuza  nyama  ya mizoga  inayonuka. 

Badala  yake, hutafuta  maua  yenye rangi  za  kupendeza  ya  mimea  ya  jangwani.  Tai  huishi kwa  kutegemea  kitu  kilichokuwako  zamani.  Wanaishi kwa  kutegemea  yaliyopita.  Wanajishibisha  kwa  kula wanyama waliokufa na wasiokuwako tena.   Lakini ndege wavumaji  huishi  kwa  kutegemea  kilichoko.  Wanatafuta maisha  mapya.  Wanajishibisha  kwa  vitu  vipya  na  kwa maisha.  

Tuesday, 11 September 2018

Mungu Anampenda kila mtu.


Wakristo wengi wanapenda  kuchagua  kuhusu ni yupi wanayemsaidia  na wanayemtia moyo. Wanawatafuta watu kama wao. Baadhi  ya watu hata wanaamini  kwamba  wanapaswa kuwasaidia  watu wengine  wanaoamini  kile wanachoamini  na kufikiria  kama  wanavyofikiria.  Hiyo  siyo  njia    inayopaswa  kuwa. Siyo njia  Yesu alivyofanya. 

Miaka kadhaa iliyopita nilisoma hadithi kuhusu mtu  fulani aliyeanguka  kwenye shimo na hangeweza  kutoka  na jinsi watu wengine walivyomhudumia mtu huyo. 
Mtu mbaguzi alikuja akasema, “Ninakusikitia huko chini.”
Mtu  asiye  mbaguzi  akaja  akasema,  “Aha,  ni  jambo  la  kueleweka kwamba mtu angelianguka huko chini.”

Monday, 10 September 2018

Mpango wa Pili.

"Penzi la kweli halikosi mkwarunzo"......utahuzunika Kwa muda gani? Utaishi kwa majuto kwa Muda gani??Mwenzangu Majuto humaliza nguvu." Laiti ninge.....Laiti nisinge.......kamaa inge...."Looh

Tatizo lako si tatizo lako bali mtazamo wako ndio tatizo lako...chanzo cha tatizo ni mtazamo wala si tatizo!!Haijilishi umefanyiwa nini kwenye maisha yako, haijalishi umefanya nini kwenye maisha yako, Ujachelewa kuingia Mwanzo mpya, Ujachelewa kuingia mwanzo mpya tena.Lakini mustakabali wako huna nafasi kwa maisha yako ya kale. "Nimeharibu maisha yangu nami  Nitakaa hapa paka Yesu aje anichukue"hapana hatuwezi kufanya hivyo.

Sunday, 9 September 2018

Je, Twahitaji Ufufuo au Mageuzi?

Kila mmoja anafikiria juu ya kuubadili ulimwengu, lakini hakuna anayefikiria kujibadili yeye mwenyewe. Jimmy J

Wakati kitu fulani kinapofufuliwa, mambo  ya  zamani  yanaletwa tena kuwa hai, mawazo  mapya yanaletwa  yanaletwa kuwa kitu. Wakati jamii inaposhuhudia  maslahi  mapya  ya  kidini,  huo  huitwa ufufuo. Kamusi ya  MerrianWebster Collegiate inaelezea  ufufuo kama “mkutano wa hisia za juu  sana wa kiinjilisti  au msururu wa  mikutano.”  Katika  maisha  yangu  ya utu uzima kama  Mkristo, nimewasikia  watu wakiongea  kuuhusu  na kuombea ufufuo. Lakini sina  hakika  kwamba  ufufuo  ndio tunaohitaji.  

Tuesday, 4 September 2018

Vaa Miwani Yako Ya Mungu

Natuvae  kile  ninachoita  “Miwani  ya  Mungu,”  ili  tuangalie  mambo fulani  kwa  mtazamo  wa  Mungu.  Yeye  anaona  mambo  kwa  njia tofauti  sana kuliko  tunavyoona kwa sababu anaona mwisho  kutoka mwanzo. 

Je, Mungu anakuonaje? Anakupenda zaidi  ya  jinsi unavyoweza kuelewa,  na ana mpango mzuri kwa maisha yako. Huko  peke yako kwa sababu yuko  pamoja nawe  wakati  wote. 

Msamaha wa Mungu ni mkuu  kuliko  dhambi yoyote  uliyotenda. Huruma zake ni mpya kila siku.  Mungu amekupa wewe  kama muumini, nguvu, na huna haja ya kuishi  maisha ya kushindwa.
Umefanywa  kiumbe kipya kabisa katika Kristo, umepewa maisha  mapya, na unaweza kuyaacha yote  yaliyopita  na utazamie  kwa hamu mambo yaliyo mbele  yako. 

Monday, 3 September 2018

Usingoje Kesho

"....tazama,  wakati  uliokubalika  ndio  sasa;  tazama,  siku ya  wokovu ndiyo sasa.) 2 Wakorintho 6:2 “
Jana ni historia, kesho  ni siri, leo  ni zawadi kutoka kwa Mungu, ndiposa tunaiita present-zawadi.” —Bil Keane

Siku  moja  mwandishi  aliyeitwa  Leo  Buscaglia  alisimulia  hadithi kuhusu  mama yake na kile alichoita “chakula cha jioni  cha familia na cha mateso.” Ulikuwa usiku  ule  wa kwanza baada  ya  baba  yake kurudi nyumbani  na akasema kwamba inaonekana kana kwamba itabidi  afilisike  kwa  sababu  mwenzi  wake  kibiashara  alikuwa ametoroka na pesa  za kampuni.  Mama yake  Buscaglia  alienda kuuza  vito ili anunue chakula kwa  ajili ya karamu ya kukata na shoka.  

Sunday, 2 September 2018

MAGEUZI YA UPENDO

Mageuzi.   Neno lenyewe linaibua  tumaini, linawasha  hamu na kuvutia uaminifu  kama  neno  ambalo halijawahi kupatikana kwenye msamiati wa  binadamu. Katika historia,  wazo  la maguezi limemimina  mafuta kwenye moto na kusisimua ujasiri kwa waliovunjika moyo.

Mageuzi yamewakusanya pamoja  wale wanaotafuta  sababu kubwa  kuliko  wao  wenyewe na  yamewapa wanawake na wanaume waliokosa  mwelekeo hapo  awali, sababu ya kujitoa mhanga.
Wamewazaa  viongozi mashuhuri  na kuwalea wafuasi mashuhuri, wameubadili kabisa ulimwengu. Mageuzi ni  jambo la ghafla, kubwa  na lililo  tofauti kabisa na jinsi  mambo yalivyo kama  kawaida.  

Wednesday, 29 August 2018

Nguvu za Kuendelea Mbele

Nakumbuka  siku  moja  nilipokea  habari  mbaya  sana  muda  mfupi kabla kuaanza kongamano la siku  tatu. Ilikuwa vigumu kuendelea, lakini  nilijua  sina  budi  kuendelea.  Nilihisi  Roho  Mtakatifu  akisema, “Nyanyua  mguu  wako  na  upige  hatua  kwenda  mbele.  Endelea kwenda Mbele!”

Kuendelea  kwenda  mbele  hakukuondoa  uchungu wote  na hali ya kuvunjika  moyo niliyohisi,  lakini  kulinizuia  nisiweze kuzama katika kilindi cha kukata tamaa,  na baada ya majuma machache, hali iliweza kutatuliwa.  Moja ya dalili  za ukomavu  wa kiroho ni kuwa  na nidhamu ya kutimiza ahadi zako, hata ikiwa  unapitia wakati  mgumu.  Nilikuwa  naumia,  lakini  nilihitaji  kuendelea kuwahudumia wengine  waliokuwa wanaumia,  na nilifanya  hivyo, Mungu aliniponya na kusuluhisha tatizo langu.

Thursday, 9 August 2018

Je, Yesu Alikuja kwa ajiri ya Wayahudi Pekee ??

Ndugu   zetu   Waislamu   wanapenda  sana  kudai   kuwa   Yesu   alikuja kwa   ajili   ya  Wayahudi   peke   yao   na   sio   kwa   ajili   ya   ulimwengu  wote.   Na   andiko   wanalolitumia   tena  na  tena  ni   la  Mathayo   15:24  pale  Yesu  alipozungumza   na   mwanamke   Mkananayo:  Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo   waliopotea   wa  nyumba  ya  Israeli.  

Na   tazama, mwanamke   Mkananayo   wa   mipaka   ile   akatokea,  akampazia   sauti   akisema,   Unirehemu,   Bwana, Mwana  wa  Daudi;  binti   yangu   amepagawa   sana   na   pepo.   Wala   yeye   hakumjibu  neno.   Nao   wanafunzi   wake   wakamwendea,   wakamwomba,  wakisema,   Mwache   aende   zake;   kwa   maana   anapiga   kelele  nyuma   yetu.   Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo  waliopotea

Sunday, 5 August 2018

Je, Yesu Alikufa...??

Na KWA AJILI YA KUSEMA KWAO MV BUKOBA Ilizama; na kwa hakika MV BUKOBA haikuzama Bali ulizama tu mtumbwi uliofanana na MV BUKOBA na wale wanaosema ilizama wamo katika shaka na jambo hilo la kusema MV BUKOBA alizama mwaka 1996; hawana uhakika isipokuwa wanafuata Dhaka tu. Na wala Meli hii haikuzama Bali mtumbwi unaofanana na MV BUKOBA ndio uliozama. Na kwa yakini MV BUKOBA haikuzama”-Maalim Chaka

Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake) Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.

Wednesday, 1 August 2018

Amini Kilicho Bora

Nimeokoa  nguvu nyingi  ambayo ingetumiwa na hasira kwa  kusema, “ Ingawa  wanachosema  au kunifanyia huniumiza, nachagua  kuamini  moyo wao  uko sawa.” Naendelea kujiongelesha hadi hisia za  hasira yangu zianze kufifia.  Ninasema mambo kama, Siamini  wanaelewa  jinsi  vitendo  vyao  vinavyoniathiri. Siamini wangejaribu kuniumiza kimakusudi. Hawaelewi jinsi  ninavyojisikia wanaposema hivyo. Pengine  hawahisi vyema kimwili  leo au pengine  wana  tatizo la kibinafsi linalowafanya kutojali jinsi walivyo.”

Ninajua  kutokana  na  ujuzi nilio nao  kwamba  kuweka kumbukumbu za  kimawazo  za  makosa  hutuathiri maisha  yetu na hakumbadilishi mtu mwingine.  Mara  nyingi hupoteza  siku tukiwa tumemkasirikia mtu fulani ambaye hata  hatambui kuwa  alifanya kitu kinachotuudhi.Wanafurahia  siku yao  na  sisi  twaipoteza  yetu. Ikiwa  tutaweka  kumbukumbu hizo,  basi  ni kwanini hatuweki kumbukumbu za  mambo  mazuri  watu  wanayosema  na  kufanya kuliko makosa wanayofanya?

Ikiwa  tunataka  kuwapenda watu, lazima  tumwache  Mungu abadilishe jinsi tunavyofikiri kuhusu watu  na  mambo  wanayofanya. Twaweza  kuamini  mabaya na kushuku  kila kitu watu wengine wafanyacho  na kusema, lakini  upendo  halisi  kila mara unaamini kilicho bora. Kile  tunachofikiria  na kuamini  ni  chaguo. Chanzo cha dhiki yetu nyingi katika maisha ni kuwa hatudhibiti au kunidhamisha mawazo  yetu.  Kwa  kutochagua  kunidhamisha  mawazo  yetu, huwa moja kwa moja twachagua kuamini mabaya ya mtu au kushuku. Nabii Jeremiah aliwauliza watu haya, “Mawazo yako mabaya yatakaa ndani  yako hata lini?  (angalia YER  4:14). Mawazo  waliyochagua kufikiria yalikuwa mabaya kwa Mungu.

Wakati tunapochagua kuamini  kilicho bora,  twaweza  kuacha kila kitu  kiondoke  hasa  kile  ambacho  chaweza kudhuru  uhusiano wetu mzuri.

```Amini Kilicho Bora.```
Mtumishi

Sunday, 29 July 2018

Somo kutoka kwenye Mkahawa

Ninaamini sote  twahitaji  kufikiria makundi ya  kujumuika nayo na kuyapanua.  Twahitaji kuyapanua  vya kutosha ili  kujumuisha watu wa  aina  yote. 

Hivi majuzi nilikuwa na  Rafiki yangu Paul  mwimbaji anayehudumu huko Birmingham, Uingereza, na tulikuwa tukinywa kahawa katika mkahawa mmoja na watu kadhaa. 

Friday, 27 July 2018

Vifungo vya nafsi

Kutumia  muda mwingi pamoja na mtu au kitu  fulani,  huleta uhusiano wa karibu na mtu au kitu hicho. Kama wanadamu, sisi  ni roho, tuna nafsi, na tunaishi katika mwili. Nafsi inaweza kuelezwa kama nia, hisia na hiari yetu. Tunapojihusisha  na mtu au kitu, sisi  hutumia muda  mrefu kumfikiria,  kuwaza  juu  ya  mtu  au  jambo  hilo  na  kufanya  mipango inyayohusu uhusiano huo. Kwa kawaida, mazungumzo yetu huwa juu ya mambo ambayo tunahusika nayo katika  nia zetu, mapendekezo yetu  na hisia zetu. 

Ukiliwazia jambo hili, utaona jinsi ‘nafsi’  zetu zinavyohusika zaidi na watu au vitu tunavyotumia muda na nguvu zetu  kushughulikia. Iwapo mkono wangu ungelifungwa kwenye mwili wangu na kukaa pale kwa muda  wa  miaka  mingi  bila ya kufanya chochote, basi matokeo yanaweza kuwa ya kutisha. Iwapo ungelifunguliwa mara,  basi ungekuwa umenyauka,  bila nguvu, na tena umelemaa. Singeweza kuutumia mpaka uweze kupata nguvu tena na uwezo wa kufanya kazi. Ingenibidi nitafute njia  mpya za kuufanyisha mazoezi ili misuli ambayo imedhoofika iweze kupata nguvu.

Ukahaba wa Vijana

Makala```

Uza mwili  wako ili  kuwafurahisha wanaume waovu  au ufe njaa.  Ni chaguo baya  sana  ambalo  mtu hapaswi kufanya.
Ingawa  ana  umri  wa  miaka  kumi  na tisa,  Suzi amefanya chaguo  hili tangu  akiwa  na  umri wa  miaka  kumi na  minne. Na  kwa  kila chaguo, moyo wake huvunjika  sana  na roho yake inaharibiwa.  Kwa  yote  aliyopitia,  ni miujiza kwamba bado anahisi chochote.

Anapata  nguvu wakati anapoangalia  macho  ya  bintiye wa  umri wa  miezi  saba,  Aamina,  maana  yake ni “salama,” na Suzi ameamua kuwa atafanya chochote  awezacho kuweka ahadi yake ya kumweka binti yake salama. Hauzi mwili  wake kwa  tamaa  au kujifurahisha.  Anauza mwili wake ili aishi. 

Upendo Wajumuisha, Wala Haubagui

Dada aliyefukuzwa kanisani kwa kuvaa vibaya.
" tunavaa vizuri wakati tunapokuja  kanisani hapa  Holiness  Tabernacle. Hakuna jeans, hakuna viatu vya wazi  kama  champali,  na pia unaweza  kufikiria  kuhusu  mtindo  wa  nywele  ambao  si wa  kuvutia sana.  Unajua, switii, kwamba  Yesu  anatufunza tuwe  wanyenyekevu na sio kujivutia sisi  wenyewe. “Akamwonyesha  Jamie  tabasamu ya kejeli na kurudia kumwambia, “Unakaribishwa wakati wowote"

kiwa utawahukumu watu, huna muda wa kuwapenda. Mama Teresa

Jamie aliingia ndani  ya  kanisa kwenye kona  ya barabara ya  Spruce Avenue  na barabara ya  Twenty-Third huko Harbor, Illinois. Alikuwa akitafuta  msaada.  Alikuwa ameliona jengo la kanisa kwa muda mrefu  na aliwatazama watu wakiingia  na kutoka  mara  mbili au mara  tatu kwa  wiki. Jamie mara  nyingi  alikaa  kwenye mkahawa upande  wa  pili  wa  barabara kutoka  kanisa hilo, akinywa  kikombe cha  kahawa,  akishangaa  jinsi anavyoweza  kukubaliwa  ikiwa atakuwa na moyo wa kuingia  katika moja ya ibada za kanisa.

Thursday, 26 July 2018

Matarajio Mapya na Makubwa Zaidi

Tunasema mwanamke mjamzito anatarajia “kujifungua.”  Hivyo huanza kuandaa  mipango  mapema.  Anatenda  sawa  na  matarajio yake—hununua  nguo,  chupa,  kuandaa  chombo  cha  kumlazia mtoto, na kuandaa mahali pa kumweka ili akue.
Tunapaswa kutenda kama watu walio na matarajio. Sharti  tuamke asubuhi na tuandae mipango ili Mungu afanye  kitu cha ajabu. 

Kwa msaada  wa Mungu, tunaweza kuwaza hivi  Huenda leo ndiyo siku. Siku ni hii Bwana  amefanya, na kitu kizuri hakina  budi kutendeka  kwangu .  Hata ikiwa Mungu hatakupa kile kitu ulichokiomba,  jaribu kupanua mtazamo wako. Pengine  unaomba kitu na huku Mungu ana  kitu kingine kizuri  zaidi.  Usiombe  tu  kitu  kizuri;  amini  na  uwe  na  matumaini  ya makubwa zaidi. Amka  kila  siku  na  useme,  “Nina  matarajio  mazuri  na  ya  kwamba  kitu  cha  ajabu  kitatendeka  leo.  

Acha Kuzungumzia Shida Zako

Je,  umewahi  kugundua  kwamba  Yesu  hakuzungumzia  shida zake?  Angeweza  kufanya  hivyo;  Alikabiliana  na  mambo  yale yale  tunayokabiliana  nayo  mimi  na  wewe.  Yesu  alikuwa  na  ratiba iliyojaa  shughuli. 

Yesu  alikumbana  na  watu  wajeuri  na  wanaoudhi. Yesu  alikabiliana  na  hali  ngumu.  Bila  kutaja  kwamba  alifahamu fika  kwamba  atateseka  sana  na  kufa  msalabani  kwa  ajili  ya  dhambi za ulimwengu. Lakini  ukisoma  Injili,  hutamsikia  Yesu  akisema  chochote  cha kukashifu  au kinachoweza  kuitwa kulalamika au kunung’unika. Bila  shaka  alijua  nguvu  za  maneno.  Wakati  wa  mateso  na  kifo chake ulipokaribia,  aliwaambia  wanafunzi wake  kwamba hatakuwa akiongea  nao kwa muda mrefu  kuanzia wakati  huo na kuendelea (Yohan 14:30).  

Uchoyo

Ni dhahiri katika mawazo  yetu kuonekana tuko hali bora  kuliko wengine  au kufanya vyema kuliko wanavyofanya. Uchoyo ni  kuhusu  kuwa wa  kwanza katika kila jambo, na ingawa hakuna makosa ya kutaka  kufanya vyema  zaidi,  ni makosa  kufurahia  kuwaona  wengine wakikosa kufaulu ili sisi tufaulu.Ninaamini  kwamba  uchoyo wa aina yote ni  mbaya na kwamba unasababisha matatizo.

Katika  sehemu  hii, nataka  niyalete mawazo yako kwa  aina tatu maalum za  uchoyo ambao  kwa  kawaida unapatikana  katika  ulimwengu wa  leo na  matokeo  mabaya yanayotokana na uchoyo huo. 

Shinda Uovu kwa Mema

Kinachohitajika kuwezesha uovu kupata ushindi ni watu wema kutulia na kutofanya chochote. Jimmy J.

Kutofanya lolote ni  rahisi, lakini  pia ni  hatari sana. Mahali ambapo hakuna pingamizi ya kuzuia uovu, uovu huongezeka haraka.  Sote mara nyingi huangukia mtego wa kulalamika kuhusu mambo yaliyo kasoro  katika jamii yetu na maishani, lakini  kulalamika hakufanyi kitu isipokuwa  kutuvunja  moyo  hata  zaidi.  Hakubadilishi kitu,  kwa sababu hakuna uwezo ufaao ndani yake.


Hebu  fikiria  ulimwengu  ungekuwa vipi  iwapo yale Mungu aliyofanya ni kulalamika kuhusu  kila kitu kilicho kasoro  tangu alipouumba. Lakini Mungu halalamiki. Yeye anaendelea kuwa mzuri  na kutekeleza  haki. Anajua  anaweza  kushinda uovu na uzuri! Uovu una nguvu kwa kweli, lakini uzuri una nguvu zaidi.

Twahitaji  kukoma na kutambua kwamba  Mungu  anafanya kazi  kupitia  watu Wake.  Ndio,  Mungu ni mzuri wakati wote.  Lakini Amechagua  kufanya  kazi hapa  duniani  kupitia watoto  wake.. wewe na mimi.  Ni jambo la kunyenyekeza  kutambua kwamba  anaweza kufanya  mengi iwapo  tungejitolea kupenda na kufanya  mambo mazuri wakati wote.

Tunahitaji kukumbuka kwamba  maagizo  ya Yesu’  katika  Mathayo 5:16:  “Vivyo hivyo nuru yenu  na iangaze mbele  ya  watu, wapate kuyaona  matendo yenu  mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

Geuka Kulia, Geuka Kushoto..!

Mnamo mwaka 1987, jarida la  The Los  Angeles Times  lilichapisha kisa cha  mtu  mmoja  mwenye  umri  wa  miaka  53  aliyependa  kuteleza  juu ya  theluji.  Bwana  huyu  aliitwa  Ed  Kenan.  Kenan  alikuwa  mfanya biashara aliyependa mchezo wa kuteleza  na alikuwa anafanya mazoezi kisha ashindane katika mashindano  makubwa ya kuteleza wakati  wa    michezo  ya  Winter  Olympics. 

Lakini  kulikuwa  na  kitu kisicho cha kawaida juu ya Ed Kenan: Alikuwa kipofu. Miaka saba iliyokuwa imepita,  Kenan alipoteza uwezo wa kuona,  jicho moja nilipoteza uwezo kisha  lingine likafuata.  Upasuaji aliofanyiwa  mara  mbili haukuweza kuzuia  retina  zake zizipofushe macho yake. Katika  kukabiliana  na  matatizo hayo yasiyoneneka, Kenan  alikuwa  na  uamuzi  wa  kufanya:

Tafuta Kilicho Kizuri Katika Kila Kitu

Kuna hadithi moja niliwah sikia ya wanaume watatu waliojikuta wanafanya kazi  mahali  pa  kipekee  kabisa.  Wanaume  hawa  walikuwa  wafanya kazi wa kawaida waliokuwa wameajiriwa  ili kusaidia kujenga kanisa  kubwa la  London ambalo  ujenzi wake ulikuwa unaendelea. Kanisa  hili  kubwa  lilikuwa  nimesanifiwa  na  msanifu  majengo maarufu  kwa  jina  Sir  Christopher  Wren  na  lilikuwa  linatarajiwa kuwa kanisa  kubwa lenye  usanifu wa kipekee. Basi mwanahabari mmoja  wa  London  alipokuwa  akiandika  makala  juu  ya  kanisa  hilo kubwa lililokuwa likijengwa aliwauliza  wale  wanaume watatu  swali hili  rahisi:  “Mnafanya  nini  hapa?”  Yule  mwanaume  wa  kwanza akasema  “Ninakata  mawe  kwa  shilingi    10  kwa  siku.”  Yule  wa  pili akajibu  akasema,  “Ninafanya  kazi  hapa  kwa  saa    10  kila  siku.” Lakini  yule  wa  tatu  alitoa  jibu  tofauti  kabisa:  “Ninamsaidia  Sir Christopher  Wren  kujenga  moja  ya  makanisa  makubwa  zaidi  mjini  London.”

Ni  ajabu  sana  jinsi  mtazamo  wako  unavyoweza  kuathiri mtazamo wako  wa maisha?  Kile  unachochagua  kuamini  ni muhimu.  Yule  mfanya  kazi  wa  kwanza  aliamini  pesa  ndiyo  kitu cha msingi. Alipoulizwa juu  ya  kazi yake, jambo la  kwanza aliloliongelea  ni  kiwango cha pesa (jinsi  kilivyokuwa  cha chini) alichokuwa  analipwa. Mfanyakazi wa pili aliamini muda wake ndio uliokuwa muhimu zaidi. Alipoulizwa aeleze  alichokuwa akifanya, bila kusita aliongea  kuhusu  saa nyingi  alizokuwa anatumia kuwa kazini. 

Upendo Hutafuta Njia.

Kushindwa hakutanishinda kamwe mimi ikiwa ari yangu ya kufaulu ina nguvu za kutosha. Og Mandino

Hamu ni motisha  yenye nguvu. Imekabiliwa na ukweli  kwamba ikiwa  kwa  kweli nataka  kufanya  kitu fulani, nitatafuta  njia ya kukifanya.  Watu mara  nyingi huniuliza  jinsi  ninavyofanya  kila kitu ninachokifanya,  na  mimi  husema,  “ni kwa  sababu nataka  iwe hivyo.”  Hutambua kwamba Mungu  amenipa neema na huweka hamu moyoni mwangu,  lakini ni ukweli kwamba  nataka  nifanye mambo  fulani yanayonitia  moyo  kuyafanya.  Ninataka  kufanya  kile Mungu  anachotaka  mimi  nifanye; ninataka  kuwasaidia  watu na nataka  kutimiza  lengo langu,  au kama  mtume  Paulo asemavyo, “Nataka kukamilisha safari yangu.”

Tuesday, 24 July 2018

Endelea kwenda mbele.

Wanyama  mbalimbali  huwa na silika tofauti  wanapotishwa au wanapokabiliana  na woga.  Kushambuliwa  na dubu, kupandwa na kuchakuro, kushtuliwa  na paa anayekimbia, na fuko  anayechimbua. Muitikio  haya  yote  ya  silika  yanafanya  kazi. 
Lakini  kuna  mdudu mmoja  ambaye  huitikia  kwa  njia  tofauti:huyu ni kifaurongo. 

Kifaurongo  ni mdudu ambaye hamkimbizi mtu, hapandi, hatoroki, au kuchimbua. Kifaurongo hujigandisha tu.  Badala  ya kufanya kitu,  hujigandisha tu.  Hujifanya  amekufa—  ndipo  tunapata  ule  msemo  wa  Kiingereza unaosema  “playing  possum”  (kujifanya  kifaurongo)—na  hutumaini kwamba kwa kujigandisha atakamilisha kitu fulani. 

Monday, 23 July 2018

MATUMAINI WAKATI UNAUMIA

[Matumaini  haya] tuliyo nayo kama  nanga  ya  roho, yenye salama, yenye nguvu... Jimmy J
Waebrania 6:19 Tunahitaji  matumaini  wakati  wote,  lakini hasa wakati  tunapokuwa tunaumia.

Matumaini  huonekana vigumu kupatikana  wakati tunaposongwa na mambo magumu au tunapokumbwa na aina yoyote  ya  uchungu Hata  hivyo, si lazima  utumie  maneno “napitia wakati mgumu”  kama  kisingizio  cha kuvunjika  moyo kufadhaika, na kukosa matumaini. Ingawa ni vigumu zaidi, ni muhimu zaidi wakati  wote  kuwa na matumaini wakati  unapopitia  magumu.  Mungu  anataka  tuwe salama, si kutuacha tukiwa tumekwama.
Tunapopata  hasara  fulani,  natukabiliane  na hasara  hiyo na, katika mchakato huo tusijipoteze wenyewe.  Tunapopatwa na janga natuomboleze  vizuri na tusiache  roho ya  huzuni iweze  kubadilisha maisha yetu  yote  kuwa janga.

Ushuhuda wa Annah

"baba  yangu  alinidhulumu  mimi  kingono  kwa  miaka mingi na  matendo yake ya  uovu yaliharibu roho  yangu  na  kuniacha nimejeruhiwa  na  siwezi kufanya  kazi  kama  kawaida  hadi Yesu aliponiponya. Kusahau yale aliyonifanyia na kuweza kumsamehe kabisa lilikuwa jambo  gumu  kabisa.  Kwanza,  nilifanya  uamuzi nisimchukie  tena  kwa  sababu Mungu alinifanya  nifahamu kwamba kumpenda  Yeye na kumchukia  baba  yangu  mzazi  hakungekaa katika moyo mmoja."

"Nilimpokea Yesu kama Mwokozi  wangu  nikiwa  na umri  wa miaka tisa, lakini  sikuelewa nilichokuwa nacho  ndani Yake  au jinsi ya  kuwa  na uhusiano Naye kungebadili  maisha  yangu  kwa  sababu sikuwa na “elimu  ya kuendelea”  katika maswala  ya  kiroho. Nyumba niliyolelewa haikuwa ikifanya kazi. Baba yangu alikuwa mlevi, asiye mwaminifu  kwa  mama  yangu   huku akiwa  na wanawake wengi, na alikuwa mtu  mkali  mwenye  fujo  na hasira. Kama nilivyotaja  hapo awali, pia alinidhulumu  kingono kila mara.Annah
"Orodha hii  inaendelea, lakini  nina hakika umeipata picha hiyo. Annah anaendelea kusema "  Nilimpenda  Mungu na  nilitaka  kujifunza,  kwa  hivyo nikajiunga na masomo ambayo hatimaye yaliniruhusu kuthibitishwa katika dhehebu na kwenda kanisani kila mara.  

Sunday, 22 July 2018

Ni Kazi ya Nani..??

Ni Kazi Ya Nani??
Hii  ni hadithi niliyoisikia miaka  kadhaa  iliyopita  kuhusu  watu wanne waitwao Kila mtu, Mtu  fulani,  Mtu  yeyote, na Hapana  Mtu... Kulikuwa na kazi muhimu ya kufanywa na Kila Mtu alikuwa na uhakika  Mtu  fulani angeifanya.  Mtu yeyote  angeliifanya,  lakini Hapana  Mtu aliyeifanya.  Mtu Fulani  akakasirika  kuhusu  hayo kwa sababu ilikuwa kazi  ya  Kila Mtu. Kila Mtu alifikiri  Mtu yeyote angeliifanya,  lakini  Hapana  Mtu aliyetambua kwamba  Kila Mtu hangeliifanya.  Mwishowe,  Kila Mtu alimlaumu Mtu fulani wakati Hapana Mtu aliyefanya kile kile Mtu yeyote angelifanya.

Wakati fulani nilisoma  kuhusu kisa  cha  kushangaza kinachoonyesha mambo muhimu  ya hadithi hii  ya kusikitisha ya ukweli.  Mnamo mwaka  1964 Catherine  Genovese  alidungwa kisu na  kufariki  katika  kipindi  cha  dakika thelathini  na tano  ilhali majirani thelathini na nane wakitazama.  Hatua  waliyochukua ilielezewa  kuwa  baridi na  ya  kutojali,  matokeo  ya  ubaguzi  wa mijini. 

Friday, 20 July 2018

Tazama Baraka zako Badala ya Matatizo yako

Siku moja nilisikia  hadithi ya mwanamume mmoja aliyepoteza funguo jioni moja. Basi akawa anazitafuta  sana, alizitafuta  kwa hasira nje  pembezoni mwa moja ya  barabara,  chini ya  mlingoti wa taa  za barabarani.  Mpita njia mmoja  aliona jinsi  alivyokuwa akizitafuta  kwa bidii na akasimama  kumsaidia  kutafuta  funguo hizo.

Baada  ya  dakika chache  za kutafuta  kwa bidii, yule  mgeni aliyekuwa anamsaidia alimwuliza akasema, “Sasa, hizo funguo umeziangusha wapi haswa? Kama tukijua ni wapi haswa,  huenda tukawa na bahati  tukaziona.” Bila  kusita, yule mwenye  funguo zilizopotea  alijibu,  “Niliziangusha  wakati  nilipokuwa  nyumbani kwangu.” Yule mgeni aliyekuwa anamsaidia akapigwa na bumbuazi kusikia  jibu hilo, akasema kwa  mshangao, “Ikiwa umeziangusha nyumbani  kwako, mbona unazitafuta  hapa chini ya mlingoti  wa taa?”  Yule  aliyepoteza  funguo  akajibu,  “Kwa  sababu  hapa  kuna mwangaza zaidi.”

Wednesday, 18 July 2018

Mungu Hutumia Vyombo Vilivyovunjika

Huenda  unasoma sura hii na unafahamu kwa uchungu ni mara ngapi  umekosea wakati  ulipokuwa unachukua hatua  hapo zamani. Huenda  kulikuwa na  wakati  ulipata  nafasi ya  kuchukua hatua huku ukiwa na malengo  makubwa, na ari  ya  kuchukua hatua  kwa ujasiri na kutimiza  jambo fulani, lakini  mambo  yakaenda mrama. Ikiwa  hivyo ndivyo unavyohisi,  ninaweza kuelewa  kule unakotoka. Mara nyingi nimejaribu kufanya kadri nilivyoweza, lakini badala ya kuyafanya mambo kuwa  mazuri zaidi, nilihisi kana kwamba  niliyaharibu mambo  kabisa. 

Nadhani  sote  tumewahi kupitia  siku  kama  hizo.  Lakini  hatupaswi kuruhusu kushindwa  kwetu  wakati  wa nyuma kutuzuie kujaribu tena siku zijazo. Mungu anajua  kwamba  tunayo mapungufu  na  udhaifu. Kushindwa kwetu  hakumshangazi, na hakumzuii  kufanya kazi katika  maisha yetu.  Kusema  kweli,  mara  kwa mara  Mungu hutumia mapungufu  yetu  kudhihirisha  nguvu  zake.  Niliwahi  kusoma  hadithi moja inayoonyesha vizuri vile ninavyosema:

Monday, 16 July 2018

Iache Hali Yako Ya Zamani

Yale  yaliyokuwa  kweli  katika  maisha  ya  Paulo  ni  kweli  katika maisha  yako  vile  vile.  Wewe  pia  ni  “kiumbe  kipya  [ambayo  ni matokeo ya kuzaliwa mara  ya pili na asili mpya katika Kristo Yesu,  Masihi],”  na  pia  unaweza  kupokea  “mapya  sasa  yamekuja.” Huko  jinsi  ulivyokuwa  awali. Mungu amefanya mengi sana katika maisha yako—amekubadilisha. 

Nina  hakika,  wewe  kama  mimi, uko mbali  sana na kuwa mkamilifu, lakini pia nina hakika  kwamba umeendelea  na kwamba umepiga hatua Kama ungetulia na kufikiria juu ya jinsi ullivyokuwa zamani— mambo yaliyokuwa yanakusumbua — ungesisimka sana juu ya jinsi Mungu alivyokutoa mbali. kubwa katika kuyafikia mabadiliko mazuri. Kama  ungetulia  na  kufikiria  juu  ya  jinsi ulivyokuwa  zamani—mambo  yaliyokuwa yanakusumbua  —ungesisimka  sana  juu  ya jinsi Mungu alivyokutoa mbali.

Kumjua Mtu Mpya Aliye Ndani Yako.

"Wanawake  wengi  walioolewa  wanajua  kwamba  kubadilisha jina kunahitaji mazoea.  Ulikuwa unaitwa Yasinta Makokoto, lakini sasa unaitwa Yasinta Mapunda. Ulikuwa waitwa  Sally Edward, lakini sasa  unaitwa  Sally Joseph.  Inachukua  muda kuweza kuzoea jina jipya, lakini kumbuka, Paulo alikuwa anakabiliana na tatizo lililokuwa  zaidi  ya  mabadiliko  ya  jina—  Paulo  alikuwa  anapokea mabadiliko  ya  moyo  na  pia  asili. " -Nukuu

Lakini  sisi  sote, kwa uso usiotiwa  utaji, tukiurudisha  utukufu  wa Bwana,  kama  vile  katika  kioo,  tunabadilishwa  tufanane  na mfano uo huo,  toka  utukufu  hata  utukufu, kama  vile  kwa  utukufu  utokao kwa Bwana, aliye Roho. 2 Wakorintho 3:1

Sunday, 15 July 2018

Jibu la Mungu Wakati Unapofikiri Siwezi

Mojawapo  ya  vizuizi  vibaya  zaidi  vinavyotuzuia  kuishi maisha ambayo Mungu anataka  uishi  ni ule  mtazamo wa kiakili wa  siwezi. Siwezi  ni tundu lisilokuwa na msamaha lililotengenezwa ili  likuzuie  kuinuka  na  kufikia  kilele  cha  uwezo  wako. 
Hebu  piga taswira  ya  tai  anayependeza  na  asiye  na  manyoya  mengi—ndege ambaye  aliumbwa  ili  apae  kwenye  mabawa  ya  upepo—akiwa amejibanza  kwenye  tundu,  akiwatazama  tai  wengine  wakipaa  juu. Haya  ndiyo  yanayotokea  ukiishi  na  akili  yenye  mtazamo  wa    siwezi. Badala  ya kuishi  maisha uliyoumbwa kwayo, umekwama katika kifungo cha kuwekewa  mipaka na mapungufu. 

Siwezi kuidhibiti hasira  yangu.  Siwezi  kupata  kazi. Siwezi  kusahau  mabaya  niliyotendewa. Siwezi  kuendelea.  Sielewani  na  mke/mume  wangu.  Siwezi  kuruhusu  mtu aniumize tena.  Siwezi  kutatua  tatizo  hili.  Siwezi  kulea watoto  hawa  peke yangu.  Siamini  haya yamenipata.  Siwezi...Siwezi...Siwezi. Tunaweza kuongea mpaka jioni. Hakuna mwisho  wa mambo ambayo watu hufikiria hawawezi kuyafanya. Lakini  umetambua  kipengele  muhimu  katika  orodha  ya  mawazo iliyopita?  

Thursday, 12 July 2018

Good intentions are not Enough

I heard one story about one man who went to Russia with a good intention to tell people about the Love of Jesus Christ.During his visit,many people were facing hunger.when he got the queue of people waiting for the hope of getting the bread of the day,he followed him when he is holding the gospel of the gospel in the hand and bega to walk following the queue to tell them that Jesus loves him and give each one of the news of salvation message.In fact,he was trying to help,but one woman took him in his eyes of salvation message.

In fact,he was triying to help,but one woman took in him in his eyes and said to the pain,"your words are sweet,but he doesn't have my own stomach"
I have learned that some people are really suffering to hear good news that God loves you,it must witness that love and one way the best of the matter is through us to fulfill their needs with actions And as well as telling them that they a loved.

Wednesday, 11 July 2018

Nia Nzuri Haitoshi

Nilisikia  hadithi moja kuhusu  mwanaume mmoja  aliyekwenda nchini  Urusi  akiwa  na nia nzuri  ya kuwaambia  watu kuhusu  upendo wa  Yesu Kristo. Wakati wa  ziara yake, watu wengi walikuwa wanakabiliwa na  njaa.  Alipopata  foleni ya  watu wakisubiri kwa matumaini  ya kupata  mkate wa  siku, aliwafuata  akiwa  ameshika vijikaratasi  vya  habari ya  injili  mkononi na akaanza  kutembea akifuata  foleni  hiyo akiwaambia  kwamba  Yesu  anawapenda na kumpa kila mmoja kijikaratasi  chenye habari ya  ujumbe  wa wokovu. Kwa  kweli, alikuwa  anajaribu kusaidia, lakini mwanamke mmoja akamwangalia  machoni  mwake na akasema  kwa  uchungu, “Maneno  yako ni  matamu, lakini  hayajazi  tumbo langu lililo  tupu.”

Nimejifunza  kwamba  baadhi  ya  watu wanaumia vibaya  mno kusikia habari njema kwamba  Mungu anawapenda,  ni lazima washuhudie upendo huo na  njia moja  bora  ya  jambo  hilo kutendeka ni  kupitia sisi ili  kutimiza  mahitaji yao  kwa  vitendo  na vile  vile kuwaambia kwamba wanapendwa. Ni lazima  tujihadhari  juu ya  kufikiri  kwamba  maneno yanatosha. Yesu vile vile alihubiri kuhusu habari njema, lakini mahali alikokwenda alitenda mema na  kuwaponya  wote  waliopondeka mioyo (angalia MDO 10:38).

Uchoyo ni Chaguo

Wengi wetu hutumia muda  mwingi kufikiria, kuongea  na  kufanya mipango yetu wenyewe. Ingawa  ninafunza kwamba  twapaswa kujipenda  sisi  wenyewe katika njia ya uwiano, siamini  kuwa tunapaswa  kujipenda sana  hivi kwamba  tuwe katika  ulimwengu wetu na  kujali tu kile  tunachotaka  tupate. Kwa  njia zote  lazima tujitunze   kwa  sababu sisi  ni  wa  thamani kuu  kwa  mpango wa Mungu hapa  duniani.

Alitupa uhai kwa  hivyo  lazima  tuufurahie (angalia  Yohana  10:10). Kwa  hivyo tunahitaji  kuutafuta,  lakini lazima  tusikose kutambua  kwamba  njia ya  kweli ya  kupata  furaha ni kuyatoa  maisha  yetu kuliko  kujaribu kujiwekea  maisha  hayo  sisi wenyewe. Yesu anasema  kwamba ikiwa  tunataka  kuwa  Wanafunzi wake,  lazima  tujisahau,  tukose kujionea sisi wenyewe na  maslahi yetu yote  na  tumfuate Yeye (angalia  Marko  8:34).  Sasa  nakubali kuwa hili  ni  wazo  la kutisha, lakini  nina  nafasi maana  nimeishi  kwa muda mrefu  wa  kuweza  kulijaribu na  nimegundua  kuwa  linafanya kazi. 

What have you done to announce Jesus?

The servant of God Jimmy J is best writing of books and Author of the Article and run of blog as mawaidhapopote.blogsport.com , moslemstojesus.blogsport.com ,yesuninjia.blogsport.com I thank God for these blogs that the people of the people to learn and know Jesus...also on the side of facebook there are many page that have been with many followers of learning News of Jesus. .I thank God to teach me to write five books: Get your Hopes Up,Qur'an says about Jesus,the origin of Allah,the secret of the heart...these books have been helped Many and build the kingdom of God,and any of the concerns and continued to move forward...

It seems to me that the world system has a crack on its foundation,and we are all sitting without doing anythng and watch the World.when you listen carefully,you will hear the people saying that everywhere.."ulimwengu unasarambatika."tunasikia mambo haya kwenye taarifa za habari na mazungumzo kwa ujumla. It looks like everyone is taking about the ongoing evil of the world.But talking without actions doesn't matter anything.My question is, "who will be cle to oppose these evil and fix what is whrong?"

Tuesday, 10 July 2018

Mungu, Huu sio wakati Mnzuri

Biblia  inaelezea  hadithi kuhusu mwanaume  mmoja  ambaye hakumfuata  Mungu  kwa  sababu kufanya hivyo lilikuwa  ni  jambo la usumbufu  kwake. Mwanaume huyu  aitwaye Feliki,  alimtaka  Paulo aje  na  amhubirie injili.  Lakini wakati Paulo  alipoanza  kuzungumza naye kuhusu  maisha  yaliyonyooka,  usafi wa  maisha,  na  kudhibiti hamu alizo nazo, Feliki alishangaa  na kuogopa.  Alimwambia Paulo aende  zake  na kwamba  atamwita  wakati ufaao zaidi (angalia      MDO  24:25). “Na Paulo alipokuwa akitoa  hoja zake  katika habari ya  haki,  na  kuwa  na  kiasi na  hukumu itakayokuja,  Feliki  akawa na  hofu akajibu,  Sasa  enenda  zako,  nami nikipata  nafasi  nitakuita.” 

Ninashangazwa  mno na  jambo  hili, sio kwa  sababu linafurahisha, bali kwa  sababu laonyesha  wazi  jinsi  tulivyo. Hatujali kusikia kuhusu jinsi Mungu alivyo  na  upendo mwingi kwetu na  kuhusu mipango mizuri  aliyo nayo katika  maisha  yetu,  lakini wakati anapoanza  kutulaumu   kwa  makosa  tunayofanya au kuturekebisha.

Yesu - nitoe humu kuzimu!

Ndugu msomaji, wako watu wengi sana wanaopita kwenye lindi la huzuni ambazo zimesababishwa na aina ya maisha au familia walimojikuta kiasi kwamba inaonekana kama kila kitu kimekwama. Haijalishi tunapita kwenye hali ngumu kiasi gani. Wito wa Bwana wa mabwana, Yesu Kristo bado uko palepale: Njoni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha (Mt 11:28). Bwana Yesu yuko kazini saa ishirini na nne. Karibu utiwe moyo na ushuhuda huu wa dada ambaye alishakata tamaa kabisa na kuamini kabisa kuwa tayari alikuwa kuzimu. Lakini Yesu anapoingia, kila kitu kinabadilika.



...............................

Nyumba niliyokulia ilikuwa na fujo nyingi. Maisha yangu yote nilikuwa nikitamani kuwa na familia, mahali penye usalama na ambako ninaweza kupendwa. Baba yangu mara nyingi alitutelekeza huku akimuacha mama atulee sisi binti zake watatu peke yake. Kila baba alipokuwa nyumbani, mara zote nilikuwa nikinyanyaswa kiakili,kihisia, kimwili na kingono. Japokuwa nilijitahidi sana kuwa mtoto mzuri, hakuna nilichofanya kikawa kizuri kiasi cha kutosha.

Sex In Paradise


 

Sheikh Muhammad Galal Kishk
God of the Muslims in his book, the Quran in Surah 52:24 says the following about Muslims who will go into his paradise:

“Round about them will serve, (devoted) to them, Youths (handsome) as Pearls well-guarded.” (according to Yusuf Ali’s translation)
“And there shall wait on them, young boys of their own, as fair as virgin pearls.” (according to Dawood’s translation) 
………….
That in this paradise, Muslims will be served by boys that will be handsome and are like virgin pearls.


What bothers people like me is the following:
·      Why reference to handsomeness?
·      They are they like pearls?
·      Why even hint on virginity here?